#COVID19 Ibada ya Hajj yafanyika kwa utaratibu mpya kufuatia COVID-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Maelfu ya mahujaji waliochomwa chanjo ya COVID-19 wamekusanyika mji mtakatifu wa Mecca kwa ibada ya Arafa, huku Wakizingatia umbali wa mtu na mtu na kuvalia barakoa wakati virusi vya corona vikiiathiri kwa mwaka wa pili mfululizo ibada ya Hijja.

Ibada hiyo iliyokuwa inawaleta pamoja mahujaji zaidi ya milioni 2.5 kutoka kote ulimwenguni, sasa imeonekana kuwa na mistari michache na watu wachache kutokana na wimbi la COVID-19.

Ibada hiyo haiwanufaishi tu watu kutoka nje ya Saudi Arabia, lakini pia taifa lenyewe kutokana na mabilioni ya dola iliyokuwa ikiingiza kila mwaka kutokana na maeneo yake matakatifu ya kuabudu kwa waumini wa dini ya kiislamu.

Mahujaji 60,000 kutoka ndani ya Saudi Arabia ndio walioruhusiwa kuhudhuria ibada hiyo mwaka huu.

IMG_20210719_074126_109.jpg
 
Back
Top Bottom