Elections 2010 Iandaliwe Sherehe Kubwa ya Kumpongeza W.P. Slaa (PhD)

mudushi

Senior Member
Oct 19, 2010
151
84
Kwa mafanikio makubwa kabisa ya W.P. Slaa (PhD) aliyoyapata ktk siasa za Tanzania, Napendekeza sote tumwandalie sherehe kubwa kabisa ya kumpongeza. Pia yawepo maandamano kila mkoa ya kumpongeza Slaa (PhD) kwa mafanikio hayo.
 
ndugu yangu mudushi....hiyo sherehe utafanyia wapi na hayo maandamano utapita wapi katika nchi hii ya kidikteta.....sisi tuzidi kumuombea kwa Mungu ndio sherehe iliyobaki
 
Inawezekana Preta. Wazo zuri sana hilo pia litajenga taswira mpya ya ustaraab pamoja na matamko mengine mhimu yanayojenga chama huku wazee akina shibuda na akina kahigi wakichagiza umhimu wa kutokumbatia chama maana sio maa wala baba
 
Ni kweli amefanya vizuri sana lakini inatakiwa mikakati ya 2015 ianze sasa tuingie hadi vijijini na ss twende tukagombee hata udiwani au uongozi wa mitaa na vijiji. Najua CCM 2015 watatafutana sana hasa na watu wa Zanzibar kwani wazanzibar wanaweza kutaka mgombea urais wa Jamhuri atoke Zanzibar maana mara mbili mfululizo ametoka Bara. Sasa hapo sijamuona mtu wa Zanzibar atakeyeweza kupambana na Slaa. Cha muhimu tuanze sasa maandalizi ya 2015 sisi tujitahidi kuwaelimisha hadi ndugu zetu walioko vijijini
 
Kwa mtazamo wangu sherehe nzuri ni mimi na wewe, kokote tuliko, tueneze itikadi ya CHADEMA hatimaye tuwe na wanachama wengi, tuwajulishe Watanzania wenzetu ni wapi tulikotoka, wapi tuliko na wapi tungetakiwa TUWE. Tuwasimulie raslimali tulizokuwa nazo. Tuwajulishe Israel haina ardhi lakini ni nchi inayoongoza duniani kwa Kilimo. Wadanganyika hawa wataelewa na natumaini hata chaguzi ndogondogo zote zitakuwa zetu. Sherehe njema
 
ndugu yangu mudushi....hiyo sherehe utafanyia wapi na hayo maandamano utapita wapi katika nchi hii ya kidikteta.....sisi tuzidi kumuombea kwa Mungu ndio sherehe iliyobaki

Ndungu (kaka/dada), ninakubaliana na wewe kwa 1000% I mean unity! kama walikataa Dr W P S kutumia uwanja wa Samora pale Iringa na wa Sokoine kule Mbeya kufanya mkutano wa kampeni, je wataturuhusu kufanya sherehe hata kwenye hoteli ya Mbowe kule Machame (Protea Hotel)? siyo tu kwamba watauzuia na kutuambia kuwa tunahatarisha amani, inawezekana kabisaaa watatupiga virungu.
Cha msingi, Tupige magoti kila mmoja wetu ktk imani na Mungu wake tuzidi kuomba kufunguliwa kwa watanzania ktk kifungo cha umaskini wa mawazo na kuwa huru kufahamu haki na stahili zao. Mungu atupe ujasiri wa kumuombea Dr na Rais wetu (Slaa) Mungu ampe afya njema na ujasiri wa kuendeleza mapambano.
 
Kwa mafanikio makubwa kabisa ya W.P. Slaa (PhD) aliyoyapata ktk siasa za Tanzania, Napendekeza sote tumwandalie sherehe kubwa kabisa ya kumpongeza. Pia yawepo maandamano kila mkoa ya kumpongeza Slaa (PhD) kwa mafanikio hayo.

si wengine wanachuo, ulishaambiwa na dr kuwa usalama wa taifa aka. uwccm wajijumuika kuchakachua unataka watugundue alafu tupigishwe sap kwenya test zetu?
 
Mi hapa naona jambo moja tuu, dawa ya moto ni moto tuu. Tujipange mapema kama wenzetu SI SI EMU ( japo wanatumia hela za serikali kuchakachua) ili na sisi next time we stand out from the crowd pia, tumejifunza kutoka kwenye hili pia.
Dr. Slaa oyeeee............:smile-big:
 
Jamani pongezi ni muhimu sana, kwanini wakate! kwani watu wnaandamana? si sherehe iwe ya siku moja nchini kote
 
kwa kweli MUNGU AMBARIKI SANA - AMPE NGUVU MPYA - AMPE MAWAZO MAZURI ZAIDI - KWANI NAAMINI IKO SIKU ATALIONGOZA TAIFA HILI LA TANZANIA - IKO SIKU NDOTO ZETU WAPENDA MAENDELEO NA MABADILIKO ZITATIMIA - TUMWOMBEE ASIKATE TAMAA KWANI TUKO NYUMA YAKE - NAAM SIKU AMBAYO TANZANIA ITAKUWA NCHI YENYE NEEMA KI-MATENDO NA SI MANENO MATUPU.

PAMOJA NA MAWAZO YA KUMPONGEZA KWA VITENDO - LAKINI TUMWOMBEE SANA MUNGU AMPE AMANI - KWA MAANA INAUMA KUONA UNAIBIWA HAKI YAKO NA BARAKA YAKO ALIYOKUPA MUNGU - KAMA WALIVYOMFANYIA DR. SLAA KWA KUCHAKACHUA KURA ZA UCHAGUI! LAKINI UKWELI UTABAKI PALE PALE -[SIKU ZA MWIZI AROBAINI ..................NA NDIO INAKUWA SIKU YAKE YA KUSAGA MENO KWA WALIOMFANYIA HIVYO] - MUNGU MBARIKI DR. SLAA, MPE MAISHA MAREFU SIKU MOJA AIONE NDOTO YAKE - MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom