Ian Smith aaga dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ian Smith aaga dunia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MzalendoHalisi, Nov 20, 2007.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Waziri Mkuu wa zamani wa Rhodesia- Ian Smith amefariki dunia! Hali ya Zimbabwe kwa sasa ni tete na ngumu kwa watu wengi. Je huyu Mzungu atakumbukwa Zimbabwe kwa lipi? Smith never believed Africans can rule themselves in 1000 years to come!

  http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7104552.stm
   
 2. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Obituary: Ian Smith

  more from the Times
  Huyu ni mzungu aliyehakikisha wazungu wenzake wanaishi kwa jasho la waafrika wa Zimbabwe na kuendeleza dhuluma kwa kujiona wao ni bora kuliko binadamu mwingine yoyote.

  Viongozi wetu wa kiafrika wanaona sifa kujipendekeza kama malaya kwa wazungu na kuendelea kuwapigia magoti na kuwaona wao ni bora kuliko sisi waswahili. Wanakubali kutumia rasilimali zetu kwa sababu ya peremende wanazopewa na kuingia mikataba ambayo inaendelea kuwanufaisha hawa vibaka. Ukuwadi wao inabidi tuupigie kelele.

  Je, wanaweza kuiga mfano wa huyu mzungu na kuwawezesha waafrika wenzao?
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2007
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Acha UPUUZI, huyu alikuwa BORA na bado ni bora hata akiwa amekufa kuliko MUGABE!
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ahhh bana wee acheni aende akasalimie akina nyerere, iddi amini huko !
   
 5. t

  tauphiq Member

  #5
  Nov 21, 2007
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani let him go in peace regardless of whatever bad he has done but he was in power by that time.

  In deed he has done nothing good to be recalled by all africans apart from Zimbabwe people at large
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kweli ni lazima tuelimishane, tusiwe wapuuzi wa kuchukia watu kutokana na rangi zao, racism is stupid. Smith ni binaadamu alikuwa na ushenzi wake, hata leo fanya Smith, lakini huwezi kumlinganisha Smith na Mugabe hata tone, Rhodesia ya Smith ilikuwa inazalisha chakula kilichokuwa kinaliwa na watu wa nchi nyingi tu za Afrika hata Ulaya kwenyewe, na Zimbabwe ya Mugabe watu wake wanakula Panya na haina chakula cha kutosha, export yake kubwa kwa sasa ni wakimbizi. Zimbabwes economy has been brought to its knees by ujinga wa Mugabe, watu wanasingizia Vikwazo vya uchumi(ukweli ni targeted sanctions), wanasahau kuwa hata Smith alikuwa kwenye vikwazo vya kweli na kwenye vita vya ndani, lakini he deliverd the goods. Let us be fair. Rest in peace Ian, God will bless you!
   
 7. K

  Koba JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Huyu alikuwa bora kuliko huyu mmachinga Mugabe na lip service zake kwa wamandingo wa zimbabwe anawaambia wako huru huku hawana chakula na wakijikuta wakimbizi,Zimbabwe ilikuwa kama nchi nyingine tuu za Ulaya ingawaje ubaguzi ulikuwepo lakini naamini ubaguzi ungepigwa vita kwa style ya America(civil rights movements) na kushare madaraka Zimbabwe ingekuwa mbali sana na ubaguzi ungeisha tuu...South Africa iko vile kwa ajiri ya hao hao makaburu na ubaguzi unaishia!
   
 8. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Atakumbukwa kwa hizi quotes
  "In 1976 declared he didn't believe in black majority rule, "not in a thousand years"

  "There will be no black rule in my lifetime,"
   
 9. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2007
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  He may be right....look at Mugabe...the guy is not too black to feel the pain of his people.....inflation, hunger, starvation all in the modern Zimbabwe....people remember having enough food when this Ian Right was in power....Mugabe should move out and retire for good, hapa TZ napo ndipo panapoelekea yaani uzungu umetawala.....Look at the president he cant hardly sit and feel our pain, he is handsome in person and ugly at work!!! Lowassa u r just another scumbag!!!Shein is Ok so far!!
   
 10. J

  Judy Senior Member

  #10
  Nov 21, 2007
  Joined: Aug 13, 2007
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tangu niwe mtu mzima kuna kitu kimoja nimejifunza. Ukishakuwa kiongozi wa nchi no matter what you will do, expect criticism.Kuna wakati hua najiuliza kama kuna kiongozi anaweza kurest in peace bila lawama pamoja na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. simaanishi huyu smith coz i dont know alot about him, just a thought.
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. Yaani Judy umeongea ukweli tupu! Hata unfanye nini wanadamu watakulaumu tu! I think it is a human nature to critisize viongozi- ni vigumu kweli kutaja jina 1 la kiongozi ambae halaumiwi!

  2. Mugabe kweli ana makosa yake, Smith pia alikuwa na makosa yake.

  3.Leo hata akichunkua Changivrai wa upinzani watu watamlaumu tu!
   
 12. M

  Mtu JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2007
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pumzika kwa amani Ian
   
 13. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Zimbabwean: 'We were the enemy'
  Kutoka jikoni.
   
 14. R

  Rubabi Senior Member

  #14
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  --------------------------------------------------------------
  Huyu alikuwa bora kuliko huyu mmachinga Mugabe na lip service zake kwa wamandingo wa zimbabwe anawaambia wako huru huku hawana chakula na wakijikuta wakimbizi,Zimbabwe ilikuwa kama nchi nyingine tuu za Ulaya ingawaje ubaguzi ulikuwepo lakini naamini ubaguzi ungepigwa vita kwa style ya America(civil rights movements) na kushare madaraka Zimbabwe ingekuwa mbali sana na ubaguzi ungeisha tuu...South Africa iko vile kwa ajiri ya hao hao makaburu na ubaguzi unaishia!
  ---------------------------------------------------------------

  Du! Watu mna kumbukumbu ndogo kweli, hivi ni bora tuwe watumwa tulioshiba au huru wenye njaa?

  Ndio Zimbabwe kuna na matatizo,lakini ikumbukwe kuwa Mugabe ndiye aliyeleta democrasia Zimbabwe.

  Wafrika tuna kazi.
   
 15. P

  Pedro Senior Member

  #15
  Nov 22, 2007
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 114
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uhuru una maana gani kama umekufa na njaa? ukiwa mtumwa halafu umeshiba utaweza kufikiria jinsi ya kujikomboa, ukiwa huru lakini una njaa huwezi kufikiri chochote maana yake ata uhuru wako wakufikiria unachotaka unakuwa umenyang'anywa. Matatizo ambayo mnayatukuza eti mimi niko huru wakati mwanao amelala na njaa hivi waafrika tumelaaniwa nini? hivi wewe Rubabi unasuuzika roho vipi kuona watoto wadogo kule Zimbabwe wanalala na njaa? eti fahari yako anayeleta njaa hiyo ni mtu mweusi mwenzetu!

  Si ndio hayo hayo mtu kule kwetu anatuingiza kwenye mikataba ya kutuua na watu wanafurahia kisa aliyefanya hivyo mwenzetu? Mimi bwana realistic kama mtu anaweza kutuendeleza tukasoma tukapata ajira na kuwa na maisha bora mimi nafuraia bila kujali rangi ya ngozi yake, na kama mtu anapora mchana kutwa ninakasirika na kuja juu hata kama huyu mtu ni mweusi mwenzangu.

  Ushauri wa bure kuwashangilia washenzi eti kisa wana rangi nyeusi ya ngozi, upuuzi mtupu huu.

  Halafu eti Mugabe ndie aliyeleta demokrasia Zimbabwe!? hivi unajua demokrasia wewe? kuna democrasia Zimbabwe?
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Nov 22, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FD,
  Kumbe unakubaliana maneno ya Mbowe aliposema afadhali ya Mkoloni! - tena basi Mbowe alikuwa very specific kwa kitu gani - HUJUMA YA UCHUMI.

  Wanabodi pleease!
  kama mlikuwa hamfahamu masiuha ya Wazimbabwe weusi chini ya Utawala wa Kaburu Ian Smith bora kukaa kimya kabisa.
  Proganda nyingi zimesemwa kama zilivyokuwa zikisemwa chini ya Utawala wa Kaburu huko South Africa eti toka Mandela kaingia Ujambazi umekuwa kwa asilimia 100 na nchi sio salama tena. Bahati tu Mandela hakubeba Uchafu kama wa Mugabe.

  Mugabe ni kiongozi aliye wasaliti wananchi wake lakini napokluja sikia watu mkisifia Ian Smith kwa sababu kuna baadhi vijana wa Kizombabwe waliozaliwa miaka ya 70 wakimsifia.. What do they know really?.
  Guys, Hivi kweli ni afadhali mtu kuwa jela penye Uhakika wa chakula kuliko kuwa huru lakini huna chakula!...
  I mean, tusijaribu kabisa kulinganisha washenzi wawili ambao wote wanaua kwa njia tofauti. Nilikuwa mmoja kati ya Watanzania wa kwanza kwenda Zimbabwe siku ya Uhuru wao, na sidhani kama kulikuwa na mweusi hata mmoja aliyekuwa na madaraka/cheo ama nafasi kuongoza sehemu yoyote ile, kifupi hakuna mweusi aliyeweza ku shop ktk maduka yao iwe kwa uwezo ama ruksa!
  Acheni jamani hata kama hapakuwa na Apartheid kama South Africa lakini huyu mshenzi aliua waafrika vibaya sana na dharau yake ya mtu mweusi huwezi kuipa kipimo hata kidogo tena inasikitisha zaidi sifa zinapotoka kwa weusi wenyewe!..
  Mugabe ni mshenzi na tutamhukumu kwa mabaya yake lakini sio kwa kulinganisha na Simba mla nyama mwingine!
  Nakuombeni isomeni Hotuba ya Mugabe - UN. Ondoeni picha ya nani kayasema bali chukueni ukweli aliozungumzwa.
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135


  Mkandara hapa unatwist mambo, hakuna anayesema kuwa Smith was God, Smith naye alikuwa na ushenzi wake. Alichokuwa akisema wakiti ule kilikuwa na ukweli wake japo hakukisema ina a civilized manner. Wazimbabwe wengi hawakuwa in a position ya kuchukua nchi na kuiendeleza kama ilivyokuwa, na ukumbuke kuwa wakatu ule racims ilikuwa ni fashion kwa watawala. Hakuna anayesema kuwa alikuwa sahihi kwa asilimia zote, na yeye alikuwa na ushenzi wake.
  Lakini ukiangalia kipindi chake cha utawala cha miaka 15, na kipindi cha utawala cha Mugabe toka nchi hiyo ipate uhuru utaona huge difference. Usijidangaye na hotuba iliyosomwa na Muagabe UN, Mugabe amefilisika kisiasa na anahofu kubwa ya kuhukumiwa kama akiondoka madarakani, ndiyo maana anang'anania madaraka.
  Smith aliua watu kama 30,000 kwenye mapambano na kina Mugabe, wengi walikuwa waafrika, Lakini Mugabe ameuua weusi wengi vilevile wanaokaribia nusu. In my Opinuion wote ni wauaji, lakini muuaji mmoja aliweza kuendeleza uchumi ulibenefit wote weusi na weupe, lakini uchumi wa sasa wa Mugabe unawabenefit viongozi wenzie tu.
  Mbowe alisema ni heri mkoloni nadhani wakati wa ukoloni watanganyika walikuwa na better life kuliko sasa, hata ukiangalia shule walizosoma, hospitali walizokwenda, mishahara waliyopata watanganyika wakati wa ukoloni inaonesha kuwa kiuchumi walikuwa free from the government and from poverty kuliko sasa. Sasa hiviTanzania ina freedom from political domination lakini uchumi wanafaidi watu wachahce sana, kwa hiyo Mbowe had a point, he is no fool. Ukumbuke anaongoza chama cha siasa waliomchagua hawakuchagua mjinga.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Nov 22, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bongolander,
  Nadhani hujaupata ujumbe wangu vizuri. Nacho twist hapa ni kitu gani?... wapi nimesema kuwa mnamfananisha Ian Smith na God. Hivi kweli unajua maana ya Uungu hata kutumia neno hilo?.
  Ndugu yangu maelezo yako hapo juu yanaonyesha wazi kuwa wewe ni kijana mdogo, kufikira Rasicm ilikuwa fashion ni jambo la kusikitisha zaidi hasa kutoka kwa mtu mweusi. Kifupi ndugu yangu nachojaribu hapa ni kuwa moderator wa kiaina ktk baadhi ya hoja zinazotolewa humu kiasi kwamba sasa hivi tunapoteza kabisa umuhimu wa kijiwe hiki. Utanisamehe sana, ila kumbuka kuwa kijiwe hiki wanasoma watu wa kila aina na mengi tunayoyazungumza humu hupokelewa na baadhi ya watu kama ndivyo tunavyofikiria. Nia na madhumuni hasa ni kutaka watu muwe makini kidogo na hasa maswala kama haya, sio lazima uchangie ikiwa huna uhakika na kile kilichotokea huko nyuma.
  Labda niweke maelezo yangu kwa kifupi, ni kwamba siku zote tunapojaribu kulinganisha kitu ni bora zaidi tukichukua mfano bora dhidi ya mbaya. Ian Smith hawezi kuwa mfano mzuri hata kidogo pamoja na kwamba sote tunakubaliana kuwa Mugabe ni kiongozi mbaya. hayo mazuri waliyokuwa nayo Wazimbabwe ni yapi?...kama sio story za vijana waliozaliwa miaka ya 70 baada ya kukuta kina Mugabe hao hao wabaya wameingia mwituni kuwasafishia njia. Sasa labda tuseme hata mateso ya Mugabe ni fashion maanake ndio nayaona toka kwa viongozi wengi wa kiafrika.
  Ni maajabu makubwa ya mtu mweusi kila siku kutafuta njia za kuupamba utumwa ama Mkoloni kiasi kwamba ktk kuficha aibu zetu tumefikia hata kujaribu kubadilisha historia. Ukienda leo Zanzibar kule walikokuwa wakiuzwa watumwa wamekubadilisha kabisa na sehemu hiyo leo hii ana own mzungu ambaye kaondoa minyororo na vitu vyote vinavyohusiana na historia ya utumwa, tena kwa fahari zaidi sisi tunajivunia kuonyesha majumba ya Sultan na jinsi alivyoitawala nchi yetu sio utumwa kwani ni aibu na kutaliwa ni fahari.
  Nina hakika ni wachache humu wanaofahamu kuhusu Majimaji, watemi wetu na jinsi walivyokuwa against Ukoloni lakini yote haya tumeisha yazika na kukumbatia zaidi kina Livingston..
  Kwa mtaji huo kweli kizazi kijacho kinakuwa na kumbukumbu gani zaidi ya kutukana mtawala yeyote anayekuja na kusifia wakoloni.
   
 19. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2007
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mkandara,

  Al in all ila mi naona UWEZO wa kujitawala hatuna. Tuna matatizo mengi mnnoo!
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Nov 22, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FD,
  Nimekuelewa vizuri sana hapo kama hutatumia mfano ule pale nyuma. Kifupi kilichotufanmya kuombe Uhuru wetu ni kuondokana na Kutawaliwa, iwe na mzungu ama mtu mweusi lakini kwa bahati mbaya viongozi na wanasiasa wetu wametaka kuchukua pale alipoachia Mkoloni, Leadership kwao ni RULE... hakuna kabisa nafasi ya rule of law.
  Hata hivyo bado nina matumaini na kizazi hiki kipya ikiwa wataweza kuipokea historia yetu na kuitazama mapungufu yake kisha kutafuta ufumbuzi badala ya kufungiwa elimu ktk pakacha bila kufahamu kilichomo.
   
Loading...