i warakak wa mheshimiwa raisi...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

i warakak wa mheshimiwa raisi......

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by PapoKwaPapo, Jul 9, 2011.

 1. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwako mh. raisi

  Salamu nyingi sana zikufikie popote pale ulipo. Nasema popote pale ulipo kwani sijui nifikishe salamu hizi hapo magogoni au tayari umeshaelekea safarini. Tuyaache hayo nakuombea kwa Mwenyenzi Mungu uwe mzima wa afya ili uweze pata waraka huu, nijitofautishe na wengine kwani mi si kama wale wanaokuombea mabaya udondoke kama ulivyodondoka pale jangwani, kwani kunawengine limekuwa swala la kisiasa na kujipatia mtaji wa umaarafu kupitia hilo.


  Dhumuni hasa la waraka huu nikutaka kukumbusha machache tokea kipindi chako cha awamu ya pili ianze yamkini yakaribia mwaka mmoja sasa.
  Mh. tukubaliane kwa pamoja ulivaa joho hilo la utukufu si kwa ridhaa ya watanzania bali kwa kutumia familia yako, jeshi la polisi, bila kusahau Tume ya uchaguzi iliyo kutangaza mshindi angaliwanajua hukushinda kwani tunaye raisi wetu wa moyoni Dr wa ukweli W. Slaa. Hilo halina shaka kabisa kwani naamini na wewe walifamu.

  Kwasasa tuyaache hayo kwani kama ni utukufu tayari umeshaupata, ila Mh. huku ulipopita kunamajeraha mengi uliyoyaacha, udini ndio umekuwa wimbo wetu wa taifa, ukabila na utanganyika na uzanzibari ndio yamekuwa mapambio yetu. Napata sana mashaka historia yetu itakukumbuka kwa lipi. Oh labda lile la babu Seya kwani hata watoto wa msingi wanajua haki haikutendeka.

  Mh. nadhani unakumbuka vyema ulivyosherekea wanaopata mimba ni viherehere vyao, hilo sina ubishi nalo hata kidogo kwani yule dada yangu kule kijijini sasa ana mimba ya pili ile ya kwanza haikuwa bahati kwani iliharibika akiwa juu ya bajaji kuelekea hosipitali ya kata kujifungua. Zile bajaji zimesaidia sana kwani wengi wao hawafanikiwi hata kufika hosipitali kama ilivyotokea kwa dada.

  Nakuheshimu sana Mh. lakini hata ile dhana ya kujivua gamba ilikuwa usanii????? Kila siku nawaona waliotuibia wakiwa mitaani wakitesa ama kweli hili ni shamba la bibi.

  Kunakitu kilinifurahisha sana Mh, ni lile la kukuona kwenye runinga ukilia lia eti wanataka kunipindua ohhh mara ivi mara vile. Mh kumbe na wewe muoga eeh. Ila ukweli ni huu Mh, hilo lilikuwa siyo lengo letu kwani tukitaka kulitimiza hilo wala hutojua kwani mamlaka ya utawala wowote ule upo kwa uma. Lengo letu lilikuwa kufikisha hisia zetu kwako.
  Kwahili sikutishi Mh, nakuambia mapema ili uweze kujiandaa na sema ipo siku na hiyo siku yaja tutaanzaa kuingia majumabani mwenu na kuwatoa mmoja mmoja,kwani wastani wa masikini na matajiri umekuwa mkubwa kupita kiaasi na sisi makabwela mmetusahau kabisa.
  Jinandae vyema mkuu kwani siku hiyo itakuwa ya kulia na kusaga meno.

  wako katika ujenzi wa taifa,

  J J Pikawaka.
   
 2. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asanteni waungwana......mawazo yangu hao
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tunashukuru kwa waraka wako:pound:
   
Loading...