I noti nyingi za shilingi 1000 na 2000 za tanzania zina nini ?

MAHENDEKA

JF-Expert Member
Jul 9, 2010
306
152
p { margin-bottom: 0.08in; } Kwa wale waishio tanzania sijui kama uchunguzi huu mlishaufanya ama vipi ni kwamba ukitazama kwa makini noti ya shillingi elfu moja na noti ya shilingi elfu mbili(ila sio ya sh 5000/10000)sijui kwa nini, mara nyingi utakuta ule mstari wa kung'aa-ng'aa uliopo kwenye pesa hizo huwa umekwanguliwa na kufutika kabisa, na katika pitapita zangu za hapa na pale kuuliza kulikoni niliambiwa kuwa eti hiyo ni bidhaa muhimu kwa wale mateja(watumiaji wa madawa ya kulevya) na wanayoyauza pia...Nimejitahidi kuuliza jina la hiyo bidhaa na kwa madhumuni gani huwekwa kwenye pesa hizo bila mafanikio yeyote..Sasa swali nalojiuliza ni kwa nini bidhaa hiyo haramu ipatikane katika pesa halali za nchi?,na kwa jinsi inavyoonekana kama kweli kuna biashara chafu inafanyika kwa bidhaa hiyo basi soko lake litakuwa kubwa sana manake kila noti nayokutana nayo huwa imekwanguliwa!!manake inawezekana tukawa tunamtafuta mchawi kumbe ni sisi wenyewe
 
good one....mi mwenyewe nilishawahi kusikia kuwa huwa zinakwanguliwa halafu zinachanganywa na bangi......sasa kama serikali inalijua hili....ni hatua gani inachukua coz kila siku tunasikia vita dhidi ya madawa ya kulevya.......sasa cha kushangaza noti zetu wenyewe ni madawa ya kulevya......hainiingii akilini hii
 
Soi kwamba ni dawa ya kulevya lakini hutumika kuikoleza wanadai ina kitu ambacho ukiiongeza kwenye bangi au mihadharati mingine inakuwa kali zaidi.
 
Hiyo si bidhaa haramu!!!!!! anayetumia kuchanganya na dawa za kulevya ndy mhalifu. Ingredients nyingi za madawa ya kulevya si haram,uharamu wake unaanzia pale zinapochanganywa na kupata kokitaili! teh teh. Ndy maana kuna dawa zingine ukikutwa nazo bila maandishi ya daktari ni haramu!
 
Hilo suala lilishatolewa tamko na wenye dhamana ya noti hizo kwenye vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom