Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Wana JF naomba mnishauri kitu mimi kuna dada mmoja ninampenda sana na yeye analifahamu hilo maana nimewahi kumueleza kwamba nina mpenda sana ningependa tuoane, akaniambia hapana maana yeye hana mpango wa kuwa na mimi na kuishi nami kama mkewe japo, huwa ananitumiaga meseji mara kwa mara kwamba ananipenda, mpaka sasa amenitumia meseji kumi na nne zinazosema ''I love you'' siku tofauti tofauti, mara tatu nilimuomba tutoke alikubari lakini nikimueleza suala la kuoana anakataa, nikiomba kufanya naye mapenzi hataki, kumbuka ninampenda kweli, huu ni mwezi wa sita ananifanyia hivi. nifanyeje na huyu dada?