I intend tume huru ya uchaguzi na katiba mpya

MSN TZ

Member
Feb 13, 2019
10
45
Wapendwa Wana JF,

Kama thread title inavyojieleza, in the coming election 2020, nafikiria kupambana na 'Mzee baba' katika kupeperusha bendera ya Chama chetu ....CCM.

Wengi nadhani watachukulia hili jambo ni 'utani'....hata mzee baba mwenyewe naamini atajua ni utani LAKINI napenda kumfahamisha kuwa kijana wake nataka kumuondoa katika nafasi yake kupitia sanduku la kura ndani ya chama chetu, hivyo atakapoona napata 'mass support' ukumbini wala asichanganyikiwe kabisa.

Kipaumbele changu ni hiki:
1. Katiba mpya.....hiki ni kilio chaa muda mrefu na ndio jambo la kwanza nikiingia mjengoni.
2. Tume huru ya Uchaguzi ..NEC ...hili nitalifanikisha mapema sana kwa kupitia Katiba mpya maana kila kitu kitakuwa kimeainishwa vizuri.

NB: Kwa kuzingatia mawazo yenu na watanzania kwa ujumla, nitaangalia katiba pendekezwa ya Jaji warioba na maboresho mengineyo kabla ya kupigiwa kura na watanzania wote.

TAHADHARI: Najua wapo wana CCM wenzangu wachumia Tumbo....naomba mkae mbali, nikiingia mjengoni basi chama kinakuwa ni cha wananchi, na watanzania wote ni sawa.

Nahitaji kuona kila mtanzania akifaidika na rasimali za nchi hii, na wawe na uhuru kamili wa kuongea watakacho so long as hawavunji sheria....Lazima kuwe na demokrasia ya kweli.

No ukabila wala ukanda wa ziwa.....'all Tanzanians are equal'.

Wale wote wanaomuimbia mapambio 'Mzee baba muda huu' na kumtukuza kama Mungu...tayari dawa yao inachemka and they should not expect to continue to hold all such position after being sworn as 'President'.

Mwisho, nakaribisha maoni na michango huru ya mawazo namna ya kuijenga nchi yetu na vipaumbele ambavyo wewe kama Mtanzania unadhani ingefaa vishughulikiwe after October, 2020 . Naomba usiongelee suala la katiba Mpya wala tume huru ya Uchaguzi hivyo no core kwangu.

Ikimpendeza Mungu, in 2025 nitaachia mtu mwingine na nitahakikisha uchaguzi wa kwanza wa tume huru unafanyika kwa haki kadiri ya katiba mpya itakavyotuongoza.

Naipenda Tanzania, nawapenda watanzania wote.

Karibuni kwa michango ya mawazo.

Moods...naomba uzi wangu usiondolewe.....wala msiogope....after October, 2020 nitawalinda kwa nguvu zote !
 

MSN TZ

Member
Feb 13, 2019
10
45
tume huru sio kipaumbele chetu kwa sasa huu ni muda wa kujenga nchi
Huwezi kuongoza nchi bila kufuata katiba! Nchi yeyote ni lazima iendeshwe kwa katiba inayokidhi matakwa ya nchi (raia). Unapozungumzia nchi, unazungumzia wananchi na wala sio Rais au waziri Mkuu.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,532
2,000
Huwezi kuongoza nchi bila kufuata katiba! Nchi yeyote ni lazima iendeshwe kwa katiba inayokidhi matakwa ya nchi (raia). Unapozungumzia nchi, unazungumzia wananchi na wala sio Rais au waziri Mkuu.
Mbona mnaleta ukakasi humu? Atiii!! Huwezi kuendesha nchi bila katiba. Kwani hukumsikia huyu kiongozi wetu akiapa kuilinda katiba yetu?? Leteni hoja zenu zenye mashiko sio vishikizo.
Katiba sio kipaumbele kwa sasa bali kuinyoosha nchi kwanza. First things first. Katiba tulioiapia kuilinda maana yake ni kuwa; Hatuibadilishi kwanza.
 

MSN TZ

Member
Feb 13, 2019
10
45
Mbona mnaleta ukakasi humu? Atiii!! Huwezi kuendesha nchi bila katiba. Kwani hukumsikia huyu kiongozi wetu akiapa kuilinda katiba yetu?? Leteni hoja zenu zenye mashiko sio vishikizo.
Katiba sio kipaumbele kwa sasa bali kuinyoosha nchi kwanza. First things first. Katiba tulioiapia kuilinda maana yake ni kuwa; Hatuibadilishi kwanza.
Kuinyosha nchi kwani uliambiwa nchi imepinda? Unajua ni vema ukajitambua hata kama ni mfia chama. Ninachokiona wengi mnamsapoti mzee baba pasipo kujua kwamba mnaburuzwa na mtu ambae hapaswi kuwaburuza.

Kwa hiyo ukiweza kujitambua hutoweza kusema katiba sio kipaumbele. Umeona Kenya katiba mpya inavyotoa nafasi ya ku-challenge matokeo ya Urais mahakamani? je Tanzania kitu hicho kipo?

umeona kenya Rais anavunja katiba hovyo na wananchi wanamvumilia? Katiba Mpya ni muhimu sana wakati huu kuliko nyakati zingine zote kwa tanzania.

3. kipaumbele changu cha tatu ni kutoa ajira kwa watanzania na hasa vijana waliomaliza vyuo vikuu na vyuo vya kati, na pia kuhakikisha kilimo kinatoa ajira kwa vijana na hasa kuhakikisha masoko ya mazao yao yatafutiwa masoko ndani na nje ya nchi. Hii pia itasaidia kukuza uchumi wa nchi.

Pia nategemea kuongeza mapato ya nchi hadi kufikia kiasi cha Trilion 2 kwa mwezi au zaidi. Najua utauliza na kushangaa kivipi ila hilo lipo ndani ya mikakati yangu. ukitembea utajifunza mengi pia.

ukishindwa kunielewa halafu ni mwana CCM mwenzangu basi naomba pita uende ukalale.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom