I hate Siku ya Wapendanao

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Siku ya Wapendanao Maarufu kama Valentines Day,ni siku pekee ambayo siipendi katika kalenda ya maisha yangu,mwanzoni nilikuwa naipenda sana siku ii kuliko hata siku yangu ya kuzaliwa (My birthday).Ninaichukia siku hii kwasababu moja kubwa ifuatayo; Nilikuwa na mpenzi wangu tuliyependana sana,alikuwa ndio mpenzi wangu wa kwanza katika maisha ya mapenzi.Tulikutana na huyu mpenzi wangu tukiwa Chuo Kikuu pale Morogoro jina la chuo kapuni..Mahusiano yetu yalikuwa mazuri sana,kiasi kwamba niliamini kwamba huyu mpenzi wangu ndio angekuwa mwenzangu wa ndoa. Bila kutarajia siku ya wapendanao ya mwaka 2005,ndipo mambo yalipoenda kombo.Nakumbuka ilikuwa ni siku ya kazi ambapo tulikuwa tunaratiba ya vipindi darasani kama kawaida. Kwa kweli nilijiandaa kama ilivyo kawaida yetu kwaajili ya kuwa pamoja jioni ya siku hiyo baada ya vipindi.Kama kawaida nilikuwa nimenunua kadi na maua mzuri pamoja na zawadi kwaajili ya mpenzi wangu. Wakati tuko kwenye kipindi cha jioni kwa kweli nilipoteza kabisa network ya kusikiliza lecture jioni ile kwani nilikuwa nafikiria my outing with my love..Baada ya kipindi nikarudi zangu hostel nakuanza kujiandaa kwaajili ya mtoko. Nikiwa najiandaa nikapata ujumbe mfupi toka kwa mpenzi wangu,sikuamini nilichokisoma.Ujumbe ulikuwa mfupi sana kuliko jumbe nyinine zote nilizowahi kuzipata toka kwake.Ujmbe ulisema ametafakari kwa kina na kuona ni bora tuachane,nakuomba nisimuulize zaidi ila niwe best friend wake..At first nilidhani it was just a joke,nami nikamtext akadai yuko serious,ikabidi nipimgie majibu yakawa ni yale yale.,then ikabidi niende nikamuone,tulikuwa tunakaa hostel tofauti,we had a serious talk lakini ukweli ukabaki kuachana..Sikuwa nimegombana naye kiasi cha kuachana..Niliumia sana kwakuwa nilimpenda na kumwamini sana mpenzi wangu huyu,mkumbuke ni mpenzi wangu wa kwanza, ni yeye aliyenifundisha what love is,ni yeye aliyenifundisha jinsi ya kupenda na kupendwa ,ni yeye aliyenionjesha ladha ya mapenzi,ni yeye aliyenifundisha siku ya wapendanao ni kitu gani,ni yeye aliyenifundisha mambo mengi yahusuyo mapenzi na vitu vingi vinavyofanana na hivyo. Iliniuma sana sana but I had to face the reality,nilikuwa sina jinsi. Tangu siku hiyo nikaichukua siku ya wapendanao mpaka hii leo,sina muda kabisa na siku hii..
 
pole sana..
wenzio sisi huwa hatuuichukulii very serious hiyo siku ya
wapendanao,
sana sana tunaichukulia kuwa ni siku ya ngono
kwa watoto wa shule na malimbukeni wa mapenzi.
 
pole sana..
wenzio sisi huwa hatuuichukulii very serious hiyo siku ya
wapendanao,
sana sana tunaichukulia kuwa ni siku ya ngono
kwa watoto wa shule na malimbukeni wa mapenzi.

Duu mkuu hiyo siku siitamani kabisa wala siipendi kabisa,Siku ya jana simu zote zilizimwa na kuja kuwashwa morning,Leo tunapewa sorry nyingi sio mchezo!!

ila kama ulivyosema hapo!!
 
The advantae of realizing fantasy from reality is the realistic disposition and spared disappointment.
 
.....but there are so many people all over the World who enjoy this day in one way or another with their loved ones.
 
Njoo kwangu nitakurejeshea heshima ya siku hii.

Mkuu GS, Kwanza pole sana yaliyokukuta hapo Feb 14th, 2005. Sijui labda mimi nina mtazamo tofauti na hili. Ni kweli unapoachwa na mtu ambaye ulitegemea awe wako wa maisha na ulimpenda kwa moyo wako wa dhati unaumia sana na kama ulikuwa shule inaweza hata kuathiri masomo yako. Ni miaka mitano tangu tukio hilo baya litokee kwako, lakini kwa maoni yangu huna haja ya kuichukia siku hii kutokana na tukio hilo la kusikitisha sana bali kama sasa hivi una mwenzio usherehekee ipasavyo na huyo uliye naye sasa hivi na kuyasahau yale yaliyopita.

Imagine kama ungeachwa siku yako ya kuzaliwa je nayo ungeichukia siku hiyo ya umuhimu mkubwa sana kwako na kuacha kusherehekea Birthday yako kwa kuwa tu uliyempenda kwa moyo wako wote alikuacha siku hiyo yenye umuhimu mkubwa kwako? Nafahamu wakati mwingine inakuwa vigumu sana kuyasahau machungu lakini pamoja na hayo hustahili kuichukia siku hii especially kama una mwenzio ambaye anapenda kusherehekea siku hii kwa namna moja au nyingine maana kila unapokataa kusherehekea siku hii labda atakuona bado unamkumbuka huyo mpenzi wako mliyekuwa naye chuoni.
 
Ni siku nzuri pia kwa kurepea mahusiano yaliyoanza kuzua vizaazaa au wenzetu wanaita drama.Unaweza kutuma au chocolate au kipande tunda kama vile apple au embe dodo. unaweza kutuma kadi kuondoa ukimya au unaweza kumpigia simu na kumtakia siku njema ya wapendanao. Ni siku nzuri ya biashara kw wale wenye kuuza zawadi au vitu vinavyohusiana na desturi na mila za wapendanao hasa kwa wale wanaohusudu tamaduni za magharibi .unaweza kuwa na valentine day kila siku au kila mwezi.ila la kheri na wengine wsipopata chochote ndio huanza visa baada ya valentine day. engine ni siku ya kubreak up na wegine ni siku ya kujenga au kurepea nyufa.valetine day unaweza kusherekea na wazazi au watoto au rafiki au hata watoto wasio na wazazi au msaada. ni mpenzi ya mtu kuamua kuichukulia vipi hiyo siku ya wapenda nao duniani.
 
Kuacha au kuachwa ni ajali ya mapenzi still life goes on, na mpenzi/wapenzi watapatikana. Katika zama hizi za utandawazi kuacha/kuachwa ni kitu cha kawaida siyo zile enzi zetu bado tupo vijana. Muhimu jiandae kisaikolojia na kusahau penzi lililovunjika
 
my dia pole sana kwa yaliyokukuta,binasfi naiona siku hii kama kawaida na hata kama nina matatizo yangu siwezi kuichukia maana ni siku iliyoumba na Mungu na wala si binadamu.For me jana was a very special , because I have a man who loves me deeply,he neva let me down,he respect me,he alwaz put me first,he neva cheat on me,he sapport n comfort me alwaz,n for valentines we gonna mit the same place wea we met for the first tyme!You wanna knw him!its JESUS MY SAVIOUR!HAPPY VALENTINE PPLE IF U WANT WE CN SHARE MY MAN,JESUS!and am not jerous sharing him with u dia.
 
kuachwa ni shughuli peevu
Pole sana JS nakumbuka mtu mmoa alisema naapa sitarudia kupenda " wewe je?
 
Imekaa kibiashara zaidi kuliko upendo. Ni biashara biashara tu! Upendo ni kwanini uwe wa siku hiyo moja tu?
 
Asante sana wote mlionipa pole,nimefarijika.Ni kweli kama webgi mlivyosema humu kwamba natakiwa kusonga mbele...na kusahau yaliyopita but I tried it and i failed.Lakini najua ipo siku nitakampompata wa kweli nitasahau yote kabisa.Nimeuruhusu moyo wangu kupenda tena,hivyo najua nitapenda tena.Ni kweli wapo wanoenjoy siku hii kwa sana na hata jana niliwaona nilipokuwa katika shughuli zangu nyingine..Kuna rafiki yangu mmoja aliniletea kadi juzi jioni,it was a nice card lakini ikanikumbusha 2005..Ipo nimeiweka sitting room..Jamani usiombe kuachwa kwenye siku hii njema.
 
So u dnt want to share my man with me?
asante sana wote mlionipa pole,nimefarijika.ni kweli kama webgi mlivyosema humu kwamba natakiwa kusonga mbele...na kusahau yaliyopita but i tried it and i failed.lakini najua ipo siku nitakampompata wa kweli nitasahau yote kabisa.nimeuruhusu moyo wangu kupenda tena,hivyo najua nitapenda tena.ni kweli wapo wanoenjoy siku hii kwa sana na hata jana niliwaona nilipokuwa katika shughuli zangu nyingine..kuna rafiki yangu mmoja aliniletea kadi juzi jioni,it was a nice card lakini ikanikumbusha 2005..ipo nimeiweka sitting room..jamani usiombe kuachwa kwenye siku hii njema.
 
Hapana Pearl,the thing is JESUS ni wa kiroho zaidi,nahitaji mtu wa mwilini?siunajua YESU huyu huyu pamoja na uwepo wake ndiye aliyeweka kitu mapenzi/ndoa?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom