Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 863
Siku ya Wapendanao Maarufu kama Valentines Day,ni siku pekee ambayo siipendi katika kalenda ya maisha yangu,mwanzoni nilikuwa naipenda sana siku ii kuliko hata siku yangu ya kuzaliwa (My birthday).Ninaichukia siku hii kwasababu moja kubwa ifuatayo; Nilikuwa na mpenzi wangu tuliyependana sana,alikuwa ndio mpenzi wangu wa kwanza katika maisha ya mapenzi.Tulikutana na huyu mpenzi wangu tukiwa Chuo Kikuu pale Morogoro jina la chuo kapuni..Mahusiano yetu yalikuwa mazuri sana,kiasi kwamba niliamini kwamba huyu mpenzi wangu ndio angekuwa mwenzangu wa ndoa. Bila kutarajia siku ya wapendanao ya mwaka 2005,ndipo mambo yalipoenda kombo.Nakumbuka ilikuwa ni siku ya kazi ambapo tulikuwa tunaratiba ya vipindi darasani kama kawaida. Kwa kweli nilijiandaa kama ilivyo kawaida yetu kwaajili ya kuwa pamoja jioni ya siku hiyo baada ya vipindi.Kama kawaida nilikuwa nimenunua kadi na maua mzuri pamoja na zawadi kwaajili ya mpenzi wangu. Wakati tuko kwenye kipindi cha jioni kwa kweli nilipoteza kabisa network ya kusikiliza lecture jioni ile kwani nilikuwa nafikiria my outing with my love..Baada ya kipindi nikarudi zangu hostel nakuanza kujiandaa kwaajili ya mtoko. Nikiwa najiandaa nikapata ujumbe mfupi toka kwa mpenzi wangu,sikuamini nilichokisoma.Ujumbe ulikuwa mfupi sana kuliko jumbe nyinine zote nilizowahi kuzipata toka kwake.Ujmbe ulisema ametafakari kwa kina na kuona ni bora tuachane,nakuomba nisimuulize zaidi ila niwe best friend wake..At first nilidhani it was just a joke,nami nikamtext akadai yuko serious,ikabidi nipimgie majibu yakawa ni yale yale.,then ikabidi niende nikamuone,tulikuwa tunakaa hostel tofauti,we had a serious talk lakini ukweli ukabaki kuachana..Sikuwa nimegombana naye kiasi cha kuachana..Niliumia sana kwakuwa nilimpenda na kumwamini sana mpenzi wangu huyu,mkumbuke ni mpenzi wangu wa kwanza, ni yeye aliyenifundisha what love is,ni yeye aliyenifundisha jinsi ya kupenda na kupendwa ,ni yeye aliyenionjesha ladha ya mapenzi,ni yeye aliyenifundisha siku ya wapendanao ni kitu gani,ni yeye aliyenifundisha mambo mengi yahusuyo mapenzi na vitu vingi vinavyofanana na hivyo. Iliniuma sana sana but I had to face the reality,nilikuwa sina jinsi. Tangu siku hiyo nikaichukua siku ya wapendanao mpaka hii leo,sina muda kabisa na siku hii..