Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Sisemi kwa maana ya kuwatukana lakini kutokana na uzoefu wangu katika mambo ya afya ya akili (mental health) naweza kusema pasipo shaka kabisa kuwa kuna watu wanahitaji kupimwa na kupatiwa matibabu ya haraka kwani wana matatizo katika uwezo wao wa kutumia chembechembe za ubongo kufikiri na kujenga hoja.
Soma sehemu hii ya habari iliyoko kwenye gazeti la mwananchi kuhusu mambo ya Muro:
wengi wamekuwa wakihoji mtu kukutwa na pingu ati ni raia; na sasa duka linasema wanashangaa inakuwaje raia kuuziwa pingu! Sikutaka kusema lakini sina budi kusema.
HIVI NI KIPI KIGUMU ENYI watawala WETU?! Kumuuzia raia bunduki na risasi za moto au kumuuzia pingu? Kama mmepitisha sheria inayokubali raia kununua bunduki na risasi kwenye duka la serikali inakuwaje jambo la kushangaza kununua pingu KWENYE duka hilo hilo?
Yaani mnachofanya ni sawasawa mnashangaa imekuwaje mtu kanunua baskeli wakati yeye ni raia ilhali duka lenu linauza magari!? Kama raia anaweza kununua gari kusafiria na akakuta mnauza, piki piki na baskeli, akiamua kununua gari na baskeli ni kipi kinaweza kudhuru zaidi barabarani!?

"Sisi wenyewe tumeshangazaa baada ya kuona taarifa ile kwenye vyombo vya habari, lakini tunachojiuliza ni kwamba inakuwaje raia anauziwa pingu wakati hana matumizi nayo,†alisema Kanali Mgawe.