I got to say it..."Tumeuziwa Mbuzi kwenye gunia"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
yes the whole hype about "Sullivan Summit"; whatever crap "A summit of a lifetime" that was.. and whatever the picture and photo ops.. the bottom line ni kuwa mkutano huu umechemsha na kwa upande wa mafanikio.. I bet you Wakenya ndio watakuwa wamenufaika sana..

Next time.. leteni wawekezaji wa kweli, watu wenye hela za kuwekeza!!! And I won't mind some Wajerumani, Waingereza.. Wajapani.. n.k.. hawa waswahili wenzetu hata Kilimanjaro hawaendi kupanda..

Halafu kuna tetesi kuwa kuna watu wamelipa dola milioni 3... (stay tuned).. And then read my signature... It'll do u good.
 
Huoni kwa mbali kuwa hao ni mafisadi waliokubuhu kiasi wamefanikiwa kuunda mtandao wa kimataifa ,miradi na mikataba mingi huanzia kwenye vikao ya aina hii.
Wanaotakiwa kuwa macho ni wananchi ,wajue ni nani na nani walihudhuria hapo na hata muhula wa Muungwana haujamalizika unaona watu wanakuja na biashara za uwekezaji na mikataba iliyokwisha farijiwa na viongozi wetu eti wanaotutakia maisha bor kila mmoja wetu.Vikao kama hivyo ni mwiba kwa Taifa changa.
 
yes the whole hype about "Sullivan Summit"; whatever crap "A summit of a lifetime" that was.. and whatever the picture and photo ops.. the bottom line ni kuwa mkutano huu umechemsha na kwa upande wa mafanikio.. I bet you Wakenya ndio watakuwa wamenufaika sana..
Next time.. leteni wawekezaji wa kweli, watu wenye hela za kuwekeza!!! And I won't mind some Wajerumani, Waingereza.. Wajapani.. n.k.. hawa waswahili wenzetu hata Kilimanjaro hawaendi kupanda..

Halafu kuna tetesi kuwa kuna watu wamelipa dola milioni 3... (stay tuned).. And then read my signature... It'll do u good.

Kama wakenya wamenufaika basi inamaana sisi ndio tumeshindwa kuchangamka na sio kosa la hao " waswahili" wenzetu.
 
yes the whole hype about "Sullivan Summit"; whatever crap "A summit of a lifetime" that was.. and whatever the picture and photo ops.. the bottom line ni kuwa mkutano huu umechemsha na kwa upande wa mafanikio.. I bet you Wakenya ndio watakuwa wamenufaika sana..

Next time.. leteni wawekezaji wa kweli, watu wenye hela za kuwekeza!!! And I won't mind some Wajerumani, Waingereza.. Wajapani.. n.k.. hawa waswahili wenzetu hata Kilimanjaro hawaendi kupanda..

Halafu kuna tetesi kuwa kuna watu wamelipa dola milioni 3... (stay tuned).. And then read my signature... It'll do u good.

MKJ,

Hapo sijakupata kidogo,hiyo $ 3,000,000 imelipwa na (a)wtz (kwa maana ya serikali or whatever govt authority) kwa ajili ya maandalizi ya hii Sullivan,au (b)wafanyi biashara ndo wamelipa (mf. ITV waliolipa $ 700,000 kwa ajili ya exclusive right ya matangazo)?

Kama unachomaanisha ni option (a) ndo kusema sisi watz ndo tumeliwa na "wajanja" wachache serikalini ambao wametumia nafasi hii kuwekeza mifukoni mwao?
 
Mimi nadhani cha msingi kufanyika baada ya Sullivan ni kutathmini udhaifu wote ulioonyeshwa na wafanyabiashara wetu na kubuni njia za kuuondoa udhaifu huo. Tukitumia muda mwingi kutafuta "mchawi" wafanyabiashara wetu wataendelea kuwa na udhaifu walioudhihirisha katika Sullivan.

Tuendelee:
1. Ilibainika kuwa wafanyabiashara wengi pamoja na waziri wao wa biashara hawakuwa hata na ratiba ya mkutano na shughuli za maonyesho! Kuinvest pesa katika shughuli bila kuwa na taarifa muhimu kama ratiba ya shughuli hiyo ni kosa kwa mfanyabiashara anayejali faida.

Mapendekezo: Wafanyabiashara wapewe elimu ya biashara, vyombo vya habari Tanzania wekeni columns za elimu ya biashara kwa lugha rahisi ili ieleweke.Serikali isimamie elimu ya biashara kwa wafanyabiashara sio tu kwenye shule za biashara.Vyombo vya kufanya hivi vipo vitumieni ipasavyo.
Wafanyabiasha wawe na hamu ya kujifunza.
Kwa wale wenye access na internet nashauri kipindi cha elevator pitch cha MSNBC http://www.msnbc.msn.com/id/21134540/vp/24990860#24918070

Mteja siku zoe kwenye biashara hana kosa, mfanyabiashara ndio mwenye wajibu wa kumfanya mteja aingie kwenye soko lake. Kwa hiyo katika Sullivan iwapo hatujanufaika basi tumeshindwa sisi sio "waswahili" na kitendo cha kusema tuachane nao tufuate wateja wengine toka Ujerumani etc kinafanya sisi tupunguze ukubwa wa soko letu. Tujielize, je wakati sisi tumeamua kuwaacha hawa "waswahili" nani atawachukua wawe wateja wake? Kama yeye ameweza kuwafanya wawe wateja wake sisi tumeshindwa nini???
 
yes the whole hype about "Sullivan Summit"; whatever crap "A summit of a lifetime" that was.. and whatever the picture and photo ops.. the bottom line ni kuwa mkutano huu umechemsha na kwa upande wa mafanikio.. I bet you Wakenya ndio watakuwa wamenufaika sana..

Next time.. leteni wawekezaji wa kweli, watu wenye hela za kuwekeza!!! And I won't mind some Wajerumani, Waingereza.. Wajapani.. n.k.. hawa waswahili wenzetu hata Kilimanjaro hawaendi kupanda..

Halafu kuna tetesi kuwa kuna watu wamelipa dola milioni 3... (stay tuned).. And then read my signature... It'll do u good.

Hapa naona kuna tatizo kwani Mzee Mkjj, sijaona hata jema moja ulionalo afanyalo JK. Kunani? agenda za siri?
 
ningefurahi kama ningepewa bajeti nzima ya mkutano huu pamoja na pesa imetoka wapi.
 
Tatizo la sisi wa TZ ni misifa tunapenda sana kuliko kuchapa kazi.Mimi nilisha sema wakenya lazima wata tupiga bao kwenye huu mkutano nyie subirini mtaona wenyewe jamaa watakavyo anza kung'aa.
 
yes the whole hype about "Sullivan Summit"; whatever crap "A summit of a lifetime" that was.. and whatever the picture and photo ops.. the bottom line ni kuwa mkutano huu umechemsha na kwa upande wa mafanikio.. I bet you Wakenya ndio watakuwa wamenufaika sana
..
Lawama kwa nani hapo mkuu? kama walinufaika wakenya sisi wabongo tulikuwa wapi?

Hakuna lawama hapo fanyeni kazi!
Next time.. leteni wawekezaji wa kweli, watu wenye hela za kuwekeza!!! And I won't mind some Wajerumani, Waingereza.. Wajapani.. n.k.. hawa waswahili wenzetu hata Kilimanjaro hawaendi kupanda
..
Kwako wazungu ndio wawekezaji sh**
 
Kabla hajaning'nizwa mtu, wakati serikali ikijipanga kueleza jinsi nchi ilivyofaidika na mkutano huu, ninatakla CTI na TCCIA nao waje kutueleza, si kwa maneno ya blah blah, bali kwa data za uhakika, ni jinsi gani wafanyabiashara wa ndani wamenufaika na mkutano huo. Business deals anmd partnership agreements which have been established. Wakianza kuleta siasa, sitawaelewa.
 
Hata Ingekuwaje Matunda Sio Ya Siku Moja Tume Kaa Kinjaa Mno. Na Mipango Ya Leo Wala Sio Ya Muda Mfupi Wala Mda Mrefu. Mission Startment Ndio Sifuri Kabisa
 
Lengo la mkutano huu ni kuisaidia Afrika kujikwamua kiuchumi. Kama tumeshindwa kunufaika na huu mkutano lengo hilo litafikiwa? Jibu ni hapana, tulitakiwa tunufaike na huo mkutano. Je ni kwa nini hatukunufaika? Ni kukosa ubunifu wa watanzania ambao unaitaji elimu na upeo wa kufikiri. Je hii elimu ya ubunifu tutaipata wapi? Je tathmini ya wenyemkutano wanasemaje? lengo limefikiwa au siyo? Kama hawa jamaa wanania ya kweli tuendelee wanahitajika basi kutufundisha namna ya kubuni biashara na siyo kutuambia tukauze bidhaa zetu marekani kwa mpango wa AGOA hali wakijua kabisa hatuwezi.
 
Hivi wakoloni wakati wakija Afrika walikuwa na lengo la kuiendeleza Afrika? Jibu ni hapana. Je tunauhakika gani hawa wawekezaji wanalengo la kuiendeleza Afrika? Hapa jamani ni lazima tukubali kusuka au kunyoa hawa jamaa lengo si kuiendeleza Afrika bali leongo lao ni kuja kufanya biashara full stop. wanatumia maneno mazuri kuwa wakiwekeza tutanufaika lakini wapi. Leo hii Holiday Inn hatuko nayo tuna jitu lingine tu sijue muda wa kulipa kodi ulikuwa umekaribia? tulikuwa na sheraton-royal palm-move n pick. Je huu ndiyo uwekezaji wa kutunufaisha? They came to do business so when we are talking with them say they are business people and not wawekezaji wakutunufaisha moja kwa moja.
 
Ukoloni ni bora kuliko wawekezaji. walijenga shule ili wapate watu wa kufanyanao kazi, walijenga barabara, reli, nyumba nk wawekezaji kila kitu wanatumia vyetu, barabara, nyumba za wafanyakazi wao, reli, shule, wasomi wetu, wao wanachota tu.
 
yes the whole hype about "Sullivan Summit"; whatever crap "A summit of a lifetime" that was.. and whatever the picture and photo ops.. the bottom line ni kuwa mkutano huu umechemsha na kwa upande wa mafanikio.. I bet you Wakenya ndio watakuwa wamenufaika sana..

Next time.. leteni wawekezaji wa kweli, watu wenye hela za kuwekeza!!! And I won't mind some Wajerumani, Waingereza.. Wajapani.. n.k.. hawa waswahili wenzetu hata Kilimanjaro hawaendi kupanda..

Halafu kuna tetesi kuwa kuna watu wamelipa dola milioni 3... (stay tuned).. And then read my signature... It'll do u good.

Mwanakijiji kwa hii umechemsha, tena sana, for the first Summit this is a milestone, usiwalaumu waandaaji au wageni waliofika, bali pia watu kama wewe ambao hamna knowledge summit kama hizi huwa sinakuwaje. Kwanza kabisa kwa hii summit I may suggest kuwa media coverage imekuwa ndogo kidogo. Pili usilaumu serikali kuwa watanzania hawakufaidi, ila ulaumu kuwa waTanzania ni ma-mbumbu; ndivyo tulivyo! Hakuna summit, symposium au conference kama hizi wenye hela wanakwenda, only brokers, agents, financial instutions na makampuni yanayowakilisha wenye pesa. Hawa wakirudi kwao waTawaambia wenye pesa nao wata-assess situation na in a next summit or an event wanaweza wakaja. Watanzania wenzangu we expect too much from putting nothing, it is impossible; we must put our efforts to realise the best output!
 
Poorest Countries in the World
Rank Country GDP - per capita
1 Malawi $ 600
2 Somalia $ 600
3 Comoros $ 600
4 Solomon Islands $ 600
5 Congo, Democratic Republic of the $ 700
6 Burundi $ 700
7 East Timor $ 800
8 Tanzania $ 800
9 Afghanistan $ 800
10 Yemen $ 900

Source: CIA World Factbook

Ktk hii list nchi ya Tanzania haikupashwa kuwapo kabisa kwani kila kitu tunacho. Kinachotuweka ktk hii list ni "u ndiyo mzee" kila mtu akiingia TZ akijitambulisha kuwa ni muwekezaji tunamchekea na kumpatia kiti kirefu. Sullivani pia imetu cost kwa vicheko hivyo hivyo. Kukimbilia misaada imekuwa ni tatizo kubwa kwetu pia. kila siku rais ni njia na mkuu kuomba wakati vitu vyote tunavyo. Yaani inatia kinyaa mno basi tu.
 
Wajasiriamali wadai kutapeliwa
Wamtupia lawama Luhanjo

na Mwandishi Wetu

WAJASIRIAMALI waliokuwa wamehamasishwa na serikali kuja kufanya maonyesho ya shughuli zao wakati wa Mkutano wa Nane wa Leon Sullivan, wameitupia lawama serikali wakidai kuwa imewatapeli.

Wajasiriamali hao, kutoka mikoa kadhaa hapa nchini na nchi jirani, walidai kutozwa fedha nyingi kwa ajili ya kupatiwa mabanda ya maonyesho, lakini wakatelekezwa.

Wakiongea na waandishi wa habari jana katika viwanja vya maonyesho ya Nane Nane eneo la Njiro, wajasiriamali hao walisema kuwa serikali kupitia kwa viongozi wa Chama cha Maonyesho ya Kilimo na Mifugo Tanzania (TASO), wamewasababishia hasara kubwa na wanajiandaa kutafuta wanasheria, ili wafungue kesi.

Akiongea kwa niaba ya wenzake, Thomas Mollel, alisema kuwa kuna kina mama wametoka Mkoa wa Iringa na wamekodi gari aina ya Fuso kwa gharama kubwa, lakini hadi jana walikuwa hawajauza kitu hata kimoja na wala hakuna mtu aliyetembelea mabanda hayo.

Aidha, alisema kuwa kuna wajasiriamali wengine wametoka nchi jirani ya Kenya na wengine Zanzibar na wote hivi sasa hawajui watarejeaje makwao baada ya kupoteza gharama kubwa wakiwa mkoani Arusha, bila hata kupata chochote.

Alisema katika mabanda hayo, kuna wajasiriamali waliolipa kiasi cha dola za Marekani 4,000 ambao wametoka Kenya na Watanzania kulazimika kulipa sh 75,000 kwa siku tangu Mei 28 hadi jana bila mafanikio yoyote.

Wajasiriamali hao wametaka serikali kulipa gharama zote walizoigia kusafiri kutoka makwao hadi Arusha na hasara waliyoipata kutokana na maonyesho hayo.

Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa TASO, Peter Ngasa, ambao ndio wasimamizi wa maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alikiri kutokea kwa hasara hiyo na kutupa lawama zote kwa wizara ya Mambo ya Nje.

Ngasa alisema utaratibu mzima wa maandalizi ulihusisha kuwepo kwa maonyesho katika viwanja hivyo vya TASO, lakini wanashangazwa na wizara hiyo kutoweka ratiba ya wageni hao kutembelea maonyesho hayo.

Aidha, akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa maofisa itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa utaratibu mzima wa mandalizi ya mkutano huo umeharibiwa na wajumbe wa kamati waliokuwepo mkoani Arusha kwa kipindi cha miezi sita kabla ya mkutano.

Alisema walichofanya wajumbe wa kamati hiyo ni kuandaa malazi ya wageni na si kushughulikia masuala mengine.

I think its too much ndio mana watu wamechokaaaa
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom