Kati ya Wizara, Bodi na utawala wa Tanesco nani anafanya maamuzi?

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
762
Jamani mimi napata shida na ninaona kuna conflict of interest katika utekelezaji. Nikichukulia mfano structure ya shirika la umma kama Tanesco na mengine. Leo ngoja tujadili Tanesco.

TANESCO

1. Kuna Management ya Tanesco
2. Kuna Board ya Wakurugenzi
3. Kamati ya Nishati na Madini
4. Wizara ya Nishati na Madini.

Ok, who is the decision maker? nani anafanya nini?

I am serious
 
Jamani mimi napata shida na ninaona kuna conflict of interest katika utekelezaji. Nikichukulia mfano structure ya shirika la uma kama Tanesco na mengine. Leo ngoja tujadili Tanesco.

TANESCO

1. Kuna Management ya Tanesco
2. Kuna Board ya Wakurugenzi
3. Kamati ya Nishati na Madini
4. Wizara ya Nishati na Madini.

Ok, who is the decision maker? nani anafanya nini?

I am serious

Bad Politics <<<<< Ulaji tunajitengenezea mkuu.
 
Kwa maoni yangu binafsi, management ndiyo wale watekelezaji wa kila siku (wabeba boxi) kuanzia mkurugenzi mkuu mpaka kufikia wafanyakazi wa kawaida. Board ndiyo wenye maamuzi kuhusu vipi mambo yaende kwenye shirika. Lakini wenyeviti (kama mfano huo wa TANESCO) hawatakiwi waende kuhamia ofisini ili kufuatilia utendaji wa kazi, hapo kutakuwa na muingiliano wa shughuli.

Wizara ni kwamba inafanya monitoring na hasa inatakiwa kufocus kwenye decisions za kisiasa.

Kamati ya bunge hiyo ni issue nyengine inafuatilia shughuli yote ya uendeshaji wa shirika au taasisi
 
Well TANESCO kwavile ni administratively and financially autonomous body,yenyewe kupitia bodi ya wakurugenzi ndo inapaswa iwe decision maker.

Ila kwavile bodi yenyewe na wakuu wake wanaserve political and private interests,ndo mana tunashuhudia UPUPU tu ukitendwa na shirika hilo!
 
Kama kuna kazi siitamani kwenye maisha yangu... ni kuwa CEO wa kampuni kama hiyo!!!
 
Wizara yenyewe jukumu lake ni la kisera zaidi. Yenyewe inatengeneza sera,mipango na mikakati mbalimbali ihusuyo umeme. Ingawa TANESCO nao wana uhuru wa kuandaa mipango na mikakati yao.
 
Tanzania ni nchi ya mipango...ukiwa na business plan ya kufanya jambo la hovyo hovyo kwenye maeneo yaliyo hot kibiashara waone wakubwa tu wakumegee eneo lako la kujikusanyia kipato...yes!
 
1) Tanesco ni kampuni ya kufuwa na kugawa umeme kwa hayo lazima iwe na management.

2) Same as above, kampuni la lazima iwe na board ya directors. Kwa hiyo swali lako la kwanza na la pili halina mantiki bali ulitaka kujaza namba tu.

3)Kamati ya Nishati na Madini ni kamati ya Bunge ambao ni mhimili wa tatu wa uongozi na ni wawakilishi wa wananchi katika masuala yao ya kila siku yanayoendeshwa na serikali. Hii ni kamati muhimu sana kwa kutuwakilisha sisi wananchi na nnaona hii ya bunge hili imeanza kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Natumai itazidisha bidii.

4) Wizara ni wizara, kama hujui maana ya wizara na au waziri, na kazi zake naomba soma katiba ya Tanzania.

Upo hapo ulipo?
 
Binti Mkongwe/Nyandaigobeko asante, in Dowans scenario which body should rule out wether we use their plant or not
 
Jamani mimi napata shida na ninaona kuna conflict of interest katika utekelezaji. Nikichukulia mfano structure ya shirika la uma kama Tanesco na mengine. Leo ngoja tujadili Tanesco.TANESCO
1. Kuna Management ya Tanesco
2. Kuna Board ya Wakurugenzi
3. Kamati ya Nishati na Madini
4. Wizara ya Nishati na Madini.

Ok, who is the decision maker? nani anafanya nini?

I am serious
Blue Balaa, hakuna conflict of interest yoyote.
Conflict of interest ni muingiliano wa ki maslahi binafsi kati ya vyombo hivyo.
Wizara ndio mmiliki kwa niaba ya Watanzania, yeye hutunga sera tuu na kutoa miongozo.
Bodi hutoa maamuzi yaani decision maker.
Menejimenti ni mtekelezaji wa maamuzi ya bodi. Kamati ya Bunge ni oversight kuangalia kwa jicho la tatu for checks and balance na inaplay only advisory role kwa bodi na menejimenti na inawajibika kwa Bunge. Ewura ni regulatory authority na Fair Competition ni kusimamia ushindani wa haki huku Fair Competition Tribunal ndio mamlaka za rufaa za regulators wote (TCRA, SUMATRA, EWURA, TIRA, TCAA, etc) na bado hakuna conflict of interest.
 
1) Tanesco ni kampuni ya kufuwa na kugawa umeme kwa hayo lazima iwe na management.

2) Same as above, kampuni la lazima iwe na board ya directors. Kwa hiyo swali lako la kwanza na la pili halina mantiki bali ulitaka kujaza namba tu.

3)Kamati ya Nishati na Madini ni kamati ya Bunge ambao ni mhimili wa tatu wa uongozi na ni wawakilishi wa wananchi katika masuala yao ya kila siku yanayoendeshwa na serikali. Hii ni kamati muhimu sana kwa kutuwakilisha sisi wananchi na nnaona hii ya bunge hili imeanza kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Natumai itazidisha bidii.

4) Wizara ni wizara, kama hujui maana ya wizara na au waziri, na kazi zake naomba soma katiba ya Tanzania.

Upo hapo ulipo?

Naona umejitahidi sana kufanya justification na bila shaka wewe ni mtumishi wa huma, we hate you for your poor performance. Ok tell me the overall performance ya hiyo TANESCO under the umberlla of Board, Wizara, Kamati na sijui Ewura.
 
Blue Balaa, hakuna conflict of interest yoyote.
Conflict of interest ni muingiliano wa ki maslahi binafsi kati ya vyombo hivyo.
Wizara ndio mmiliki kwa niaba ya Watanzania, yeye hutunga sera tuu na kutoa miongozo.
Bodi hutoa maamuzi yaani decision maker.
Menejimenti ni mtekelezaji wa maamuzi ya bodi. Kamati ya Bunge ni oversight kuangalia kwa jicho la tatu for checks and balance na inaplay only advisory role kwa bodi na menejimenti na inawajibika kwa Bunge. Ewura ni regulatory authority na Fair Competition ni kusimamia ushindani wa haki huku Fair Competition Tribunal ndio mamlaka za rufaa za regulators wote (TCRA, SUMATRA, EWURA, TIRA, TCAA, etc) na bado hakuna conflict of interest.

Asante Pasco, kwangu hizo umbrella zote ni nothing if the performance is poor. Are you satisfied with their performance?
 
Tafadhali uwe wazi zaidi. Decision Maker on what matters?

Kila Mtumishi, kila Kiongozi, kila Kitengo, kila Idara, kila Kamati, kila Bodi, kila Tume, kila Wizara n.k wana FANYA MAAMUZI FULANI kwa mujibu wa ama maelezo na mipaka yao ya kazi (job descriptions), Hadidu za rejea (terms of references) au Kanuni / Sheria (Regulations / Acts) ziongozazo. Na wanapofanya maamuzi yaliyo katika mipaka yao, haiwezi kuitwa 'conflicts of interests' isipokuwa kama miongozo inayowaruhusu ndiyo iliwekwa au kutungwa kwa makosa na hivyo inatakiwa kubadilishwa / kurekebishwa.

Siko hapa kuitetea TANESCO au Uendeshwaji wake. Kama tunataka kurekebisha pabovu, basi:

Nashauri utuwekewe hapa Muundo wa Uongozi wa Shirika (TANESCO - Organogram) na Wajumbe wa hizo Kamati / Bodi / Tume kisha ututonye juu ya migongano ya maamuzi au marudio (duplicates) au hata mianya kama ipo katika utoaji wa maamuzi.

Mfano kama Bodi ya Wakurugenzi inaweza kupanga makundi na viwango vya gharama za malipo (tariffs & amounts) wakati huo huo Management Committee au Eura nayo inaweza kupanga hayo hayo na kuyatangaza bila kuwa na mawasiliano au kikao kimoja kuwajibika kwa kikao kingine. Hali hii inaitwa muingiliano wa Mamlaka. Mfano mwingine ni pale kama tunaona wajumbe wa tuseme EURA pia ni Wajumbe (wenye nguvu za kufanya maamuzi) wa Kamati Tendaji au Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO n.k. Hapa ndio tunaweza kuzungumzia Conflict of Interests (COI) maana huwezi kusimamia vyema bila upendeleo matakwa ya wazalishaji (mtoa huduma) na pia wakati huo huo ulinde ya Watumiaji hiyo huduma.

Hivyo, sielewi kama kweli ulitaka kuelezea Mgongano wa kimaslai (conflict of interests) au mwingiliano wa madaraka / mamlaka maana hayo mawili yana utofauti sana.
 
Tanesco, kama mashirika mengi ya umma halina tija wala halifai kuwepo. Kama ni mfuatiliaji mzuri, utaona kuwa hili ni moja katika mashirika makubwa sana na linabebwa na serikali kwa gharama zetu walipa kodi kila kukicha.

Nadhani ni hivi karibuni, serikali itapo polish mchakato wake wa kuivunja monopoly ya Tanesco tutaona natural death ya Tanesco kama ilivyokuwa kwa mashirika mengine ya uma.

Misingi mibovu ya uchumi aliyoiwacha Nyerere ni hii ya umma ku-monopoly viwanda, mashirika makubwa na kadhalika. Tumeona yalivyokufa toka wakati Nyerere yupo hai, kayabeba wee, mpaka yakatutia kwenye umasikini mkubwa wa Tanzania.

Tumeona yaliyo wachwa kubebwa au yaliyokumbana na ushindani (baada ya kuruhusu ushindani) yalivyokufa au kukaribia kufa.

Siku ushindani wa kufuwa na kugawa nishati ya umeme itapo-ruhusiwa rasmi na mashirika mapya kupewa proper concession na Serikali. Tutaona kifo cha Tanesco.

Na hapo ndio tutapoona mabadiliko ya huduma za umeme. Bila hivyo, hatuna la zaidi ila kuendelea kuteseka na sababu ni Tanesco.

Kumbuka, hata inunuliwe mitambo mipya leo ya kufuwa umeme, na ikiwa Tanesco ndio wataiendesha, tatizo litabaki pale pale.

Na pia kumbuka hata kuwekwe mtambo wa kuzalisha mw kubwa, kuna njia gani za kusambaza huo umeme mkubwa? Nyaya zetu si unaziona zilivyochoka?

Tanesco should die.
 
Binti Mkongwe/Nyandaigobeko asante, in Dowans scenario which body should rule out wether we use their plant or not

Kama hakuna mgongano wa maslahi ya kisiasa TANESCO wenyewe ndiyo walitakiwa wapeleke justification kwa nini wanataka kutumia Dowans, pros and cons (labda technically and business wise). Bodi inatakiwe iangalie hiyo proposal yao bila ya kuwa na bias halafu ndiyo itoe decision kwamba waendelee au siyo.

Si unakumbuka kadhia ya Idris na mwenyekiti wa board? Kwanza alianza kwa kumuondoa pale ofisini (ambayo naamini ni sahihi) halafu kwa kesi ya Richmond walikataa kabisa lakini wakalazimishwa kisiasa. Business proposals hazikuangaliwa na zikatupwa kwa nje huko.
 
Kwa maoni yangu binafsi, management ndiyo wale watekelezaji wa kila siku (wabeba boxi) kuanzia mkurugenzi mkuu mpaka kufikia wafanyakazi wa kawaida. Board ndiyo wenye maamuzi kuhusu vipi mambo yaende kwenye shirika. Lakini wenyeviti (kama mfano huo wa TANESCO) hawatakiwi waende kuhamia ofisini ili kufuatilia utendaji wa kazi, hapo kutakuwa na muingiliano wa shughuli.

Wizara ni kwamba inafanya monitoring na hasa inatakiwa kufocus kwenye decisions za kisiasa.

Kamati ya bunge hiyo ni issue nyengine inafuatilia shughuli yote ya uendeshaji wa shirika au taasisi

hizo kamati ni nyingi mno ndio maana mamabo mengi hayafanyiki maana kila kamati ni usanii tu
maaamuzi mengi yanahitaji kupitia sehemu nyingi sana hayo yote yanachangia kiala kitu kuwa na urasimu hata ktk huduma zake
hili sio tatizo la tanesco tu nadhani kutakuwa na matatizo karibu wizara zote
kumbuka hao viongozi wote wanalipwa mamilioni ya pesa kila mwezi
halafu eti mnasema tz haina pesa, mmh ni wewe na mimi ndio hatuna
 
Naona umejitahidi sana kufanya justification na bila shaka wewe ni mtumishi wa huma, we hate you for your poor performance. Ok tell me the overall performance ya hiyo TANESCO under the umberlla of Board, Wizara, Kamati na sijui Ewura.
yes i support u for ur assumptions and auguments
lazima ifikie mahali tuwaeleze hawa jamaa kuwa WE HATE YOU,labda watajua umhimu wa kufanya wajibu wao
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom