I can't let my country go to the dogs, Nyerere - 1995

'I Can not let my country go to the dogs' Hii ni kauli ambayo haijawahi kutenguliwa, fafanuliwa wala kuhojiwa iliyowahi kutolewa na Mwl. Nyerere dhidi ya akina 'UKAWA' alipokuwa akimfanyia kampeni ya urais Mh. Benjamin William Mkapa mwaka 1995.

kauli hii ya Nyerere ilimaanisha nini? UKAWA mnaikumbuka kauli hii bado? Mbwa wa Nyerere ni akina nani? Wako wapi? Lini? Kwa namna gani? na kwa sababu gani?. Nchi yake ipi isiende kwa mbwa hao kwanini? Je, yanayotokea wakati wa chaguzi leo yana uhusiano na kauli hii ya Nyerere? Nani ajitokeze kuitengua kauli hii? UKAWA angalieni chanzo cha tatizo kwanza kabla ya matokeo yake. Nyerere mnayemheshimu alishawaita mbwa, na iliyosemwa imesemwa na aliyoandikwa imeandikwa pia.

Mkuu
Wakati Mwl akitoa tamko hilo sidhani kama UKAWA ilikuwepo.
2. Naheshimu mawazo yako lakini nafikiri mwl alifananisha walafi kama mbwa. Na hao si lazima wawe ukawa tu. Katika sakata la escrow sidhani kama kuna mbwa kutoka Ukawa?.
3. Nashauri tuache ushabiki wakijinga na tuweke masilahi ya taifa mbele.
 
I cannot go to sleep in Butiama and leave my country go to the dogs, he was talking with journalist at his residence Msasani, but now his country has gone not only to the dogs but it has gone to hell
 
Mbona povu inakutoka ndugu yangu...!!? Soma kwa utulivu ione nia ya andiko langu...sikuwa na sina lengo la kupingana katika hili...

Lengo langu lilikuwa ni kujaribu kuweka kumbukumbu sawa...

Kwenye suala la mawasiliano, muktadha unaweza kusababisha kilichokusudiwa na mzungumzaji kisieleweke kama alivyokusudia...

Basil P. Mramba aliwahi tuambia watz "Hata ikibidi kula nyasi" ndege ya rais lazima inunuliwe...Kauli safi kabisa, lakini "muktadha" ukamfanya alaaniwe na kila aliyesikia kauli hiyo...

Kwa mazingira ya kauli ya mwl, uko sahihi kwa unachoamini wewe, lakini jaribu kurudi nyuma kidogo kihistoria bila kuwa na mhemko wa kiitikadi upate kuelewa ujumbe uliotolewa na mwl...

Nikukumbushe kidogo: Wakati huo mwl pia alikuwa na ugomvi na Jakaya, Edward na Samweli, hakutaka mmoja wa hawa aongoze nchi hii hali iliyoleta mpasuko ndani ya ccm na nchi kwa ujumla (ikumbukwe kuwa Benjamini hakufahamika sana miongoni mwa watz)...Hivyo kauli ya mwalimu ilikuwa na maana pana sana, mbwa ni pamoja na "wanamtandao" wa wakati ule.

Kwa hayo maelezo mafupi nikiunganisha na mawazo yako, mwl alikuwa anawaunganisha watz waliopasuka vipande kuwatoa kwa wenyemtandao na kuwaweka pamoja ili wampigie kura chaguo lake Ben...

Kwani mpaka sasa hatuoni unabii wa mwl kutimia...!!?? Tumewapa nchi wale aliowaita mbwa wakati ule, leo tunalia: richmond, epa, meremeta, twiga kupelekwa Arabuni, biashara ya meno ya tembo, biashara ya dawa za kulevya (ma-dealer wanajulikana na rais) iptl, pap, escrow nk...

Nakushauri rudi kwenye historia ya nchi hii na mfumo wa vyama vingi...wengine humu ndani hatufungamani na mifumo ya kiitikadi bali hoja zenye maslahi kwa taifa...MBWA WANATAFUNA NCHI YETU HATA SASA...

Nchi ni kipande cha ardhi na Mbwa ni mnyama. Hivyo hakuna mtu anayeweza kutafsiri usemi ule wa Mwl. kwamba hawezi kuiacha nchi yake (kipande cha ardhi na vilivyomo) vichukuliwe na Mbwa (mnyama), bali anaposema nchi yake alimaanisha Tanzania na mbwa alimaanisha watu wasiokuwa na uhusiano na CCM. Ndiyo maana pia aliongeza kwa kusema "kiongozi safi hawezi kutoka nje ya CCM" hii inamaanisha kuwa Mwl. Nyerere hakupenda vyama vya upinzani viitawale nchi hii. Alitaka vyama vya upinzani viwepo nchi ila vifanye kazi kama ya matuta madogo barabarani (bumps) yasiyoweza kuizuia kabisa CCM kupita barabarani ila kuitahadhalisha tu na mwendo mbaya barabarani.

Msimamo huu wa Nyerere ni hatari sana kwa Taifa kwakuwa haujawahi kuhojiwa wala kuutolea ufafanuzi wakati wa uhai wake. Hueanda una mizizi mirefu sana.
 
Aliyekwambia Viongozi huko CHADEMA,NCCR,CUF na vyama vingine vya upinzani hawakutoka CCM nani?

Kwahiyo unakubaliana na Nyerere kuwa lazima wapinzani pia waanzie CCM kwanza kabla ya kwenda upinzani ili wawe safi? Think critically dugu yangu ww.
 
Mkuu
Wakati Mwl akitoa tamko hilo sidhani kama UKAWA ilikuwepo.
2. Naheshimu mawazo yako lakini nafikiri mwl alifananisha walafi kama mbwa. Na hao si lazima wawe ukawa tu. Katika sakata la escrow sidhani kama kuna mbwa kutoka Ukawa?.
3. Nashauri tuache ushabiki wakijinga na tuweke masilahi ya taifa mbele.

Toa hoja, Nyerere aliongea hayo wakati akimnadi Mkapa dhidi ya Lyatonga Mrema (mpinzani wa mgombea wa CCM kutoka NCCR). NCCR leo iko ndani ya ukawa. Kwa vigezo vya Nyerere wakati ule mbwa ni mtu au kundi lolote nje ya CCM. Yeye alikuwa anamaanisha kuwa CCM ina katiba, sera na watu makini wanaoweza kuchuja watu waovu (mbwa) ndani ya chama wasiponyoke na kupewa madaraka ya kuiongoza nchi kuliko vyama vya upinzani ambavyo alikuwa anaviona kama dodoki linaloweza kufyonza na kuruhusu kila kitu kupita kwa urahisi. Yeye alikuwa haamini kama Mrema na NCCR walikuwa na uwezo na mtandao wa kuingoza nchi hii. Je, yale yalikuwa mawazo yake binafsi au ni mawazo ya CCM, serikali na vyombo vya dola? Je, mawazo yake yalikuwa kwa Mrema na NCCR tu kwa wakati ule au ni maoni yake ya jumla kuhusu vyama vyote vya upinzani kwa nyakati zote za uhai wa taifa hili? Je, mawazo yake yale yalikuwa na usahihi kiasi gani? Nani atufafanulie? Maana Nyerere alijipambanua kuwa nchi hii ni yake (my country), hivyo alikuwa na misimamo mikali kuhusu Muungano, Azimio la Arusha, na bila shaka CCM kuendelea kutawala nchi hii milele kwa njia yoyote ile iwayo. Yeye alikuwa akiamini ni CCM pekee inayoweza kudumisha muungano kama ulivyo, ni CCM pekee yenye uwezo wa kupambana na ukabila na udini ndani ya nchi hii, kwa kuwa kwa wakati ule alikuwa akinusa ukabila NCCR na Chadema na udini CUF na NRA.
 
Hili jambo ni la kuchambua kwa umakini.
Kwanza Nyerere alidanganyika na mbwa mwitu waliokuwa wamejivika ngozi za kondoo. Nyerere aliamini katika sera ya ujamaa na kujitegemea. Wale waliojivika ujamaa feki akwaaamini, akawatetea huku akiwabeza waliokuwa wamesimamia kwenye ubepari wa kizalendo. Walipoonja tamu ya madaraka, wakammaliza mzee wa watu na sera zake, wakakihamishia chama kwenye sera za kuuza rasilimali za nchi kwa njia zilizojaa ufisadi makubwa, na kupora fedha za umma.
Hawa mbwa walioaminiwa na mwl, sasa wanakataa hata maadili ya utumishi wa umma kuwekwa kwenye katiba. Wanataka ufisadi utamalaki, na zaidi waweze kupora na kuiba bila kuulizwa ulizwa.
Kwa mazingira ya sasa, nchi ipo mikononi mwa mbwa mwitu, imeshapata majeraha ya kutosha.
Itoshe kwa watanzania kuachana na fikra mfu, tuseme imetosha.
Mungu ibariki Tanzania.
 
UKAWA/CHADEMA, acheni kumnukuu Mw. Nyerere na Mungu katika maneno yale yanaowapendeza na yale msioyapenda mnayaweka pembeni. Je mnakumbuka maneno haya " I cannot let my country go to the doggs", Mw. Nyerere aliyatamka wakati gani?

Kwa kuwakumbusha tu ilikuwa ni wakati wa uchaguzi na Mrema Augustino alishika kasi ya ajabu. Mw. Nyerere hakuwa na tatizo na utendaji kazi wa Mrema bali waliokuwa wakimzunguka,aliwaita "wahuni tu hawa na Mrema akishawatengenezea mambo wanamtimua" . Kundi lilelile na watu walewale wamebadilisha gia angani na kutua kwa staili mpya. Na hata wewe Lowassa waliotoka jasho na hicho chama wako wapi leo we kaa sawa tu,mwisho wa siku utamjua Mbowe na Mbatia ni watu wa aina gani.

Something hidden there. Slaa pia tulimwambia take care. Sasa gia imebadilishwa angani he is no more,ilitafutwa njia tu ya kumuondoa,hao jamaa wana malengo yao
 
Waambie ccm waludishe azimio LA arusha na mnahangaika maana wahindi wamegoma kudhamini kampeni zenu Kazi IPO na ccm mbona amsemi kuhusu chama kuwapa wafanyabiashara
 
CCM ni chama cha wanafiki,wanapenda kujidanganya pia ukiwa mhalifu unalindwa.....ndio maana wahalifu wanaweka bendera ya ccm katika eneo lao la kusubiri.....target
 
Ukawa@chadema acheni kumnukuu Mw. Nyerere na Mungu katika maneno yale yanaowapendeza na yale msioyapenda mnayaweka pembeni. Je mnakumbuka maneno haya Mw. Nyerere aliyatamka wakati gani? Kwa kuwakumbusha tu ilikuwa ni wakati wa uchaguzi na Mrema Augustino alishika kasi ya ajabu. Mw. Nyerere hakuwa na tatizo na utendaji kazi wa Mrema bali waliokuwa wakimzunguka,aliwaita "wahuni tu hawa na Mrema akishawatengenezea mambo wanamtimua" . Kundi lilelile na watu walewale wamebadilisha gia angani na kutua kwa staili mpya. Na hata wewe Lowassa waliotoka jasho na hicho chama wako wapi leo we kaa sawa tu,mwisho wa siku utamjua Mbowe na Mbatia ni watu wa aina gani. Something hidden there. Slaa pia tulimwambia take care. Sasa gia imebadilishwa angani he is no more,ilitafutwa njia tu ya kumuondoa,hao jamaa wana malengo yao

Hata CCM wanapenda kufanya hivyo ungekuwa fair kama karipio hilo lingewafikia wazee wa Lumumba.Nasikia mmemtimua Mzee wa Benchi la Ufundi?
 
Ukawa@chadema acheni kumnukuu Mw. Nyerere na Mungu katika maneno yale yanaowapendeza na yale msioyapenda mnayaweka pembeni. Je mnakumbuka maneno haya Mw. Nyerere aliyatamka wakati gani? Kwa kuwakumbusha tu ilikuwa ni wakati wa uchaguzi na Mrema Augustino alishika kasi ya ajabu. Mw. Nyerere hakuwa na tatizo na utendaji kazi wa Mrema bali waliokuwa wakimzunguka,aliwaita "wahuni tu hawa na Mrema akishawatengenezea mambo wanamtimua" . Kundi lilelile na watu walewale wamebadilisha gia angani na kutua kwa staili mpya. Na hata wewe Lowassa waliotoka jasho na hicho chama wako wapi leo we kaa sawa tu,mwisho wa siku utamjua Mbowe na Mbatia ni watu wa aina gani. Something hidden there. Slaa pia tulimwambia take care. Sasa gia imebadilishwa angani he is no more,ilitafutwa njia tu ya kumuondoa,hao jamaa wana malengo yao

Nyerere alisema @ I cannot let my country go to the doggs" Maana yake sintakubali kuiona nchi yangu inaangukia kwenye mikono mibaya...
 
Nyerere alisema @ I cannot let my country go to the doggs" Maana yake sintakubali kuiona nchi yangu inaangukia kwenye mikono mibaya...

Lakini bado imekuwa kwenye mikono si mibaya tu bali MIOVU kwa takriban miaka 30!!!!!!!!!!!!!!!Na leo wanatuichagulia RAIS ambaye hana hata dhamira ya kuwa Mzalendo.Magufuli hana usafi wowote ni bora huyu anayejulikana MCHAFU maana ameona umuhimu wa kuwa MSAFI
 
Back
Top Bottom