I am reading too much or JK has a serious character problems??

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,403
54,878
Jokingly the president said: ``I gazed at that small boat and said to myself, mhh, I am a Mkwere without swimming skills. Better for Membe because he has married in Mbambabay. He can swim.``

But the president was well represented in the Frelimo anniversary celebrations by a team of government and party officials which included Party Vice-Chairman Pius Msekwa, Foreign Affairs and International Co-operation Minister Bernard Membe who had crossed the river on boats.

..jamani kama JK aliona boti sio salama kwake, kwanini akawapandisha Membe na Msekwa?

..halafu baada ya hapo he is making fun and joking about it!! GRRRR...

..nadhani uamuzi aliochukua na kauli zake baada ya hapo ni very careless and un-presidential.
 
he is THE PRESIDENT ...he cant die in a boat accident.
wache membe na wananchi wengine wafe
 
Inasikitisha sana, inafedhehesha sana, inadhalilisha sana. Nadhani tatizo hapa ni priority katika mipango ya maendeleo. Kujenga sky scrapper bot, kununua magari yakifahari, kujenga barabara za jiji n.k wakati vivuko havipo. Anyway kwa mwenye akili hili ni wazi lakini kiutendaji inahitaji talent na sio siasa
 
he is THE PRESIDENT ...he cant die in a boat accident.
wache membe na wananchi wengine wafe

Nakubaliana na wewe katika hili. President akifa fikiria nchi inakuwa katika hali gani na gharama za msiba na uchaguzi mpya?!!!!!!!!!!!!
 
Kwanza ilitokea kwenye kivuko cha Pangani, akazuiwa kupanda kwa sababu kilikuwa katika hali mbaya. Lakini cha kustaajabisha ni kuwa licha ya ubovu wa kivuko hicho ambao unajulikana na kila mtu, wasaidizi wake na watu walioandaa ziara walimfikisha rais mpaka kwenye kivuko hicho kwa lengo la kuvuka.
Sasa imetokea kwenye daraja. Waliohusika walijua kuwa ujenzi wa daraja haujakamilika, yet, walimpeleka rais na wakamtaka avuke kwa mtumbwi.
je, wameshaanza kumuona rais mtu wa kumfanyia majaribio kiasi hicho? Kwa nini yeye mwenye hashtukii matukio haya? kama kashtuka, mbona hatusikii hatua zilizochukuliwa?
 
Nakubaliana na wewe katika hili. President akifa fikiria nchi inakuwa katika hali gani na gharama za msiba na uchaguzi mpya?!!!!!!!!!!!!

Sema unatania! Gharama ulizo taja unadhani zitafikia gharama Tanzania inayoingia kupitia uongozi wake butu na mbovu kabisa? Watu wanajiibia huko BOT, kontakti feki za madini nk nk na bado wataendelea mpaka atoke madarakani...
 
Kuna umuhimu wa Muungwana kujiangalia yeye na matendo yake kisha ajinyooshee kidole...

Ageuze mwendo.
 
Kwanza ilitokea kwenye kivuko cha Pangani, akazuiwa kupanda kwa sababu kilikuwa katika hali mbaya. Lakini cha kustaajabisha ni kuwa licha ya ubovu wa kivuko hicho ambao unajulikana na kila mtu, wasaidizi wake na watu walioandaa ziara walimfikisha rais mpaka kwenye kivuko hicho kwa lengo la kuvuka.
Sasa imetokea kwenye daraja. Waliohusika walijua kuwa ujenzi wa daraja haujakamilika, yet, walimpeleka rais na wakamtaka avuke kwa mtumbwi.
je, wameshaanza kumuona rais mtu wa kumfanyia majaribio kiasi hicho? Kwa nini yeye mwenye hashtukii matukio haya? kama kashtuka, mbona hatusikii hatua zilizochukuliwa?

Hili ndio tatizo la utanzania wetu wa kisasa.....Badala ya kushukuru kuwa anafikishwa hapa ama anajifikisha huko na kujionea mwenyewe ukweli wa mambo ninyi mnaona kuwa anakosea.....Inaelekea wengi mnamis sana style ya uongozi ya kina MKAPA na elites wenziwe.

Mimi ningependa kuona anaenda kubovu zaidi na kuona mambo yalivyo badala ya kujidanganya na mandhari ya IKULU, KEMPISKI, NEW YORK, LONDON na kwengineko mlipo ninyi wala heri na wanaojifanya wala heri wa nchi hii...

Hatua kutochukuliwa nakubaliana nanyi kuwa huo ni udahifu mkubwa ulikokuwepo hadi sasa na akiendelea nao ajue wazi kuwa watammaliza very soon....Kwani wahuni wa nchi hii hawajui kitu SONI bali wao hutafsiri kuwa anawaogopa na wao ni UNTOUCHABLES......

Tanzanianjema
 
Jokingly the president said: ``I gazed at that small boat and said to myself, mhh, I am a Mkwere without swimming skills. Better for Membe because he has married in Mbambabay. He can swim.``

Kwa hili raisi wetu amekuwa mkweli, kuwa yeye aliogopa lakini membe anajua kupiga mbizi hivyo ni bora aende.

Haya huwa yanatokea dunia nzima ndio maana hata raisi wa marekani huwa haendi kila mahali hasa kule ambapo security yake inakuwa na utata.
 
Mbona Bush huwa nakwenda Iraq na Afghanistan?
 
Alichokifanya na kwa masikhara makubwa ni kuonyesha udhafu mkubwa kama Kiongozi.

Kitendo chake cha kulitamkia Taifa kuwa anaogopa kupanda boti na kuwatuma Membe na Msekwa waende kufanya kazi kumwakilisha ni hitimisho la kutuonysha tabia na uwezo wake kama Kiongozi.

Angalieni mambo ya Ufisadi, yeye kama Rais, kakaa mguu pande akisubiri wengine wafanye kazi. Pitia mikataba ya Madini, Richmond, Rada, kakaa kimya akisubiri wengine wafanye kazi.

Njoo kwenye sakata kubwa Kitaifa, Muungano na vurugu mechi zilizopo ndani ya chama chake, kakaa kimya, kama hayupo pale anaogopa mawimbi na kuchukua uamuzi au kutoa tamko la Kiraisi na Uenyekiti wa CCM, kisa yeye Mkwere, hawezi kuwa na msimamo ambao utaudhi watu!

Yes he has a serious character issue and it is not right for us! He is not effective, always avoids to take a stern stance or address critical issues without fears of hurting or making someone angry!

Take a look at Richmond Saga with Mwakyembe's finding or Chenge with SFO, do you know what Kikwete did in both cases, he played the Mkwere card and allow the nature to take its own course!

Iko siku tutavamiwa au kuingiliwa na jambo la hatari na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Bwana Jakaya Kikwete ataingia uvunguni kujificha akisema "mimi Mkwere siyawezi haya"!
 
kama angejua kuwa hatoweza kupanda hivyo viboti asingeenda tokea mwanzo....na angelitafuta reason ya kueleweka.

reason ya kizembe kama hiyo haikupaswa kutolewa na rais wa nchi.....
yaani awaruhusu wengine waingia ......kisa yeye mkware! ...
 
Back
Top Bottom