Hyundai kutengeneza Magari ya Umeme

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
c2037c4137e1ab86c4a6359cb6391114~2.jpg
Spidi ya dunia kuhamia kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme badala ya mafuta imekolea na sasa kampuni ya magari ya Hyundai ya Korea Kusini imeonesha mfano wa magari yake ya umeme ambapo gari lao halitokuwa na usukani bali fimbo ya usukani ambayo itakua ikijikunja ili Mtu aweze kuendesha gari kwa uhuru.

Viti vyake vya nyuma vimepangwa kama sofa kwenye umbo la L kuzunguka kona ya nyuma ya gari hilo ambapo kwenye dari kuna TV kubwa ambayo Abiria wa nyumba wanaweza kuegemea nyuma na kutazama.

Hyundai wanatarajia kuanza kuuza magari yao madogo ya umeme mapema mwaka ujao wa 2022 lakini aina hii mpya iliyooneshwa wiki hii ya magari makubwa bado hawajasema yataingia lini sokoni.
 
Naiona misoto na njaa kali uarabuni katika miaka ijayo ya usoni

Vile visima vikikosa soko utakua ni muda wa kuliona rangi ya jasho la kiarabu linafananeje
 
Naiona misoto na njaa kali uarabuni katika ijayo ya usoni

Vile visima vikikosa soko utakua ni muda wa kuliona rangi ya jasho la kiarabu linafananeje
Kunako endelea ajira ndio kitakuwa kisanga.
Hapo vipaji ndio pekee vitakuwa na dili.
 
Naiona misoto na njaa kali uarabuni katika ijayo ya usoni

Vile visima vikikosa soko utakua ni muda wa kuliona rangi ya jasho la kiarabu linafananeje
Hili limezungumzwa sana hata magari yote yatumie umeme soko la mafuta halitaathirika, inakisiwa litaongezeka, Kuna demand kubwa sana ya Mafuta

Soma hii article ya forbes

 
Kwa umeme huu huu wa mgao ama?
Bila umeme wa mgao, Gari likiisha charge inabidi usubiri tu, kwa sasa kama sijakosea ni around saa 1 kuchaji gari. Pengine kwa baadae muda ukashuka zaidi.

Sema tutapigwa sana, Imagine mitumba toka Japan ya magari inakuja na battery mbovu mbovu gari inakuwa haikai na chaji kama simu kwa siku unachaji mara 4
 
Back
Top Bottom