NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,032
- 4,028
Chasha poultry farm hii technology naitafuta sana nilikuwa nataka kujua pa kuanzia mimi shida yangu ni ajili ya mifugo tu ng'ombe. na kuku baadae.Hebu nipe mawasiliano na wewe na pia je kwa hapa Tanzania ni wapi wanatoa mafunzo na angalau hata kuona kwa macho?,Najua wenzetu Kenya wako mbele sana kwa masuala hayaWakuu kunasiku nilipost humu kuhusu Hydroponic techinology, Ila kama ilivyo kawaida yetu thread kama hizi huwa watu wanapotezea, Ila ukweli ni kwamba hii tekinolojia ni nzuri sana na inaweza kuwa ndo suluhisho pekee mpaka sasa la chakula cha mifugo.
Inaweza kukupunguzia gharama za chakula kwa 50% na kama tunavyo jua kwenye ufugaji hasa Kuku chakula kinabeba hadi asilimia 85 ya gharama zote za uendeshaji wa kuku.
Kanga wakiwa wanakula Hydroponic fodder.
Kuku wakila hydroponic fedder.
HYDROPONIC FODDER inaweza tumika kulishia aina zote za mifugo na hii ni njia rahisi sana na isiyo kuwa na gharama sana.