Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Pamoja na ushauri wa tuition ya ana kwa ana humu JF, nashauri watu waingie kwenye YOU TUBE andika chochote kama 'growing soilless wheatgrass' au 'fodders growing', yatakuja mengi.Ukijifunza hayo pamoja na haya humu mwetu JF, nina hakika utapata kitu. Kwa kweli ni process rahisi sana, haina gharama sana LAKINI faida zake kwa mifugo yetu ni KUBWA SANA. Changamkia mwana JF!
 
Sure brother.
 
By the way hizi ni HYDROPONIC FODDERS na siyo FOODERS! Hii nikuweka record sawasawa in case unataka kuingia kwenye mtandao ingawa utasahihishwa tu ukiingiza wrong thing! Tuko pamoja.
 
Mkuu, mimi nimeanza kufuga wa kienyeji wapo 100.Ila nataka nifuge kwa kiasi kikubwa hawa ambao ni crossed breed. Je,ni aina gani nzuri hasa kwa kuhimili magonjwa, uzito na ukuaji wa haraka,nimepitia maada mbalimbali karibu aina ninazozifahamu zote zina changamoto ya magonjwa hasa hao weusi, sasso ila kroiller ndo sijaona ikizungumziwa.Je,vipi soko lao lipo kama la wa kienyeji au nalo linasumbua na pia wanaweza kupewa pumba ya kawaida tu wakakua kwa hatua za mwanzo kabla sijahamia kwenye hydroponic fodder.
Twende sambamba majibu ya maswali yako yatapatikana! Ila binafsi sijafuatilia sana aina za kuku.
 
Nawashukuru sana wakuu kwa taaluma hii adhimu.
Ila naomba niulize swali moja lililonifanya nikapekua comments zote kulitafutia majibu...
Je, ukitaka kufuga kuku mathalani wa kienyeji, kwa kutumia teknolojia maridhawa ya haidroponiki, inatosha kuwapa hiyo fodder peke yake bila vyakula vingine?
Au fodder ni nyongeza tu kama zilivyo nyasi nyingine anazokula kuku mfugwa?
Kiungwan nitangulize shukrani...
Si vyema kumlisha fodder peke yake ila kwa kipindi ambacho vyakula vingine ni changamoto unaweza kuwapatia fodder tu!
Ratio iko hivi Fodder kwa layer mash - 2:1 Kilo mbili za fodder changanya na kilo moja ya mchanganyiko huo uliozoeleka.
 
Nadhani mtoa mada alishalijibu hili.
Kwa siku kuku(alie karibu na kutaga au anaetaga) anahitaji gramu 125.
Kasema kuwa kwa siku kuku huyu atahitaji hii fooder kiasi cha gram 80.
Hivyo basi ni wazi kuwa kuku huyu atahitaji gram 45 pia za chakula cha kawaida.
Ahsante sana mkuu, naona wengine wanataka tuendelee kujibu yale yale!
 
19ec3b12f612d000269510a6376a1dc2.jpg
 
Asante. Ni kwa vipi Naweza kapata barley nikiwa naishi Dar?
Mi mwenyewe nimeitafuta nimekosa ... nimeshangaa ukiingia sokoni kuulizia shayili unapewa ngano .. hata wafanyabiashara wa nafaka hawaijui hiyo kitu....
Nasikia Arusha inapatikana ila sijapata mtu wa kunihakikishia ...
 
Shayiri kuipata ni shughuli kwa sababu inalimwa na wakulima baadhi kwa ubia na makampuni ya bia (tbl na sbl).. Kisha wanawauzia wao mzigo wote... Tutumie ngano na mtama tu.
 
Shayiri kuipata ni shughuli kwa sababu inalimwa na wakulima baadhi kwa ubia na makampuni ya bia (tbl na sbl).. Kisha wanawauzia wao mzigo wote... Tutumie ngano na mtama tu.
Ahsante kwa ushauri .... ulezi je? na kwa wafuatiliaji ...
Fuatilieni mbegu hizi zinatofautianaje kwenye fodder
Mtama mwekundu,
mtama mweupe
Uwele
Ngano.
 
Wakuu kunasiku nilipost humu kuhusu Hydroponic techinology, Ila kama ilivyo kawaida yetu thread kama hizi huwa watu wanapotezea, Ila ukweli ni kwamba hii tekinolojia ni nzuri sana na inaweza kuwa ndo suluhisho pekee mpaka sasa la chakula cha mifugo.

Inaweza kukupunguzia gharama za chakula kwa 50% na kama tunavyo jua kwenye ufugaji hasa Kuku chakula kinabeba hadi asilimia 85 ya gharama zote za uendeshaji wa kuku.

110846c.jpg

Kanga wakiwa wanakula Hydroponic fodder.
DIY-Fodder4.jpg

Kuku wakila hydroponic fedder.

HYDROPONIC FODDER inaweza tumika kulishia aina zote za mifugo na hii ni njia rahisi sana na isiyo kuwa na gharama sana.
Mkuu naomba Msada. Hydroponic yangu nilipanda ngano, baada ya siku 8 niliwapa kuku wa nyama wa wiki 2 ajabu waligoma kabisa kula. Inaweza kuwa sababu gani?
 
Mkuu naomba Msada. Hydroponic yangu nilipanda ngano, baada ya siku 8 niliwapa kuku wa nyama wa wiki 2 ajabu waligoma kabisa kula. Inaweza kuwa sababu gani?
Siku 8 kwa ngano inakuwa imeishakuwa ngumu sana ...
Kuku wapatiwe kuanzia siku nne hadi 6 mwisho ...
Nguruwe wapatiwe kuanzia siku 6 hadi 9.
Wanyama wengine ambao ni watumiaji wa nyasi .. hao hata wakipatia iliyokomaa wanakula tu!
Kuna swali jingine mkuu?
 
Mkuu, ngano ya siku 6 inakuwa fupi au kwa sababu situmii nutrition?
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom