Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Mkuu, mimi nimeanza kufuga wa kienyeji wapo 100.Ila nataka nifuge kwa kiasi kikubwa hawa ambao ni crossed breed. Je,ni aina gani nzuri hasa kwa kuhimili magonjwa, uzito na ukuaji wa haraka,nimepitia maada mbalimbali karibu aina ninazozifahamu zote zina changamoto ya magonjwa hasa hao weusi, sasso ila kroiller ndo sijaona ikizungumziwa.Je,vipi soko lao lipo kama la wa kienyeji au nalo linasumbua na pia wanaweza kupewa pumba ya kawaida tu wakakua kwa hatua za mwanzo kabla sijahamia kwenye hydroponic fodder.
 
Wakuu nahitaji mjuzi wa kutengeneza system ya hydroponics. Kwa malipo.
Ni contact private box
 
Wakuu nahitaji mjuzi wa kutengeneza system ya hydroponics. Kwa malipo.
Ni contact private box
Hiyo Hydroponics ndiyo madude gani.?!!!
Fafanua kidogo maana nna broo wangu ni fundi seremala mzuri tu
Anachonga mpaka yale makabati ya Ikulu,
Hivyo sidhani kama atashindwa kukuchongea hiyo "Hydroponics"
Maana mbao zipo za kutosha stoo.
 
Mkuu ni namna ya kupanda mboga. Bila kutumia mchanga. Inatumia pvs kupitisha maji yenye virutubisho vyote.
 
Wakuu nahitaji mjuzi wa kutengeneza system ya hydroponics. Kwa malipo.
Ni contact private box
usiwe na hofu wataalamu tupo wa hyrdoponics
Wakuu nahitaji mjuzi wa kutengeneza system ya hydroponics. Kwa malipo.
Ni contact private box
naam mkuu watalamu tupo wa hii kitu,hydoponics kwa taafsiri ya kiingereza " ability to control all necessary plant variables kama vile mwanga,nutrient na vinginevyo ,swala ni mtaji,ila sio mkubwa sana inategemea sana na zao unalotaka kulikuza.mfano chainizi ukiotesha mbegu zake ndani ya hydoponics system huchua siku tatu kufika urefu wa cm 4 na nyanya zinakubali vizuri sana na mengineo jamii ya haya.yafuatayo ni mahitaji rahisi na muhimu
1;eneo unalotaka kuotesha liendana na mahitaji yako,ikumbukwe kuwa eneo lazima liwe closed kama vile nyumba au banda maalum
2;pvc pipe (ukubwa unategemea na staili unayotaka kulima minimum ni nchi mbili),growing pot(ukubwa kulingana na zao unalotaka kuotesha ila sio muhimu sana),tube light au LED system(kulingana na ukubwa wa eneo), automatics water taps,mipira ya maji.automatics system control,ph meter,water pump(solar or electic water pump ni muhimu).tank la maji au karo la maji
 
Hiyo Hydroponics ndiyo madude gani.?!!!
Fafanua kidogo maana nna broo wangu ni fundi seremala mzuri tu
Anachonga mpaka yale makabati ya Ikulu,
Hivyo sidhani kama atashindwa kukuchongea hiyo "Hydroponics"
Maana mbao zipo za kutosha stoo.
Upo serious mkuu? Mimi naona umekusudia kufanya mzaha kidogo, na umenifurahisha kwelikweli!
 
Hivi hii kitu bado haijaanza tumika sana Tanzania au ndo mpaka SUA wa hii introduce kwa wakulima, kama kuna mtaalamu alobobea kwenye hii Technology ya Hydroponic ebu atuchambulie hapa kwa undani inafanyaje kazi na mengineyo.
 
Nawashukuru sana wakuu kwa taaluma hii adhimu.
Ila naomba niulize swali moja lililonifanya nikapekua comments zote kulitafutia majibu...
Je, ukitaka kufuga kuku mathalani wa kienyeji, kwa kutumia teknolojia maridhawa ya haidroponiki, inatosha kuwapa hiyo fodder peke yake bila vyakula vingine?
Au fodder ni nyongeza tu kama zilivyo nyasi nyingine anazokula kuku mfugwa?
Kiungwan nitangulize shukrani...
 
swali zuri ngoja tusubirie majibu
 
Nadhani mtoa mada alishalijibu hili.
Kwa siku kuku(alie karibu na kutaga au anaetaga) anahitaji gramu 125.
Kasema kuwa kwa siku kuku huyu atahitaji hii fooder kiasi cha gram 80.
Hivyo basi ni wazi kuwa kuku huyu atahitaji gram 45 pia za chakula cha kawaida.
 
Wa mkoani, hii kitu yale maji unayomwagilia yanatuamishwa kwenye hyo trei au yanachuuzika na kupotea?
sijui kama nimeeleweka!!
Nimekuelewa.... Tray ya kuoteshea hiyo fodder huwa inakua na matundu kadhaa kwa ajili ya kutolea maji kiasi.... Kwa hiyo maji kiasi yananyonywa na hiyo fodder na mengine yanatoka kupitia hayo matundu.
 
Ok, asante.
Haya yanayotoka hayapotezi sehemu fulani ya nutrients pamoja na booster?
 
Utengenezaji wa fodder kwa ajili ya mifugo, unaweza kutumia vifaa ulivyo navyo, siyo lazima uwe na hizo special trays, hizi zaidi ziko kibiashara zaidi. Unachohitaji ni kifaa chochote kinachoweza kubeba hizo mbegu kwa usalama na zenye matundu chini yanayotoa maji kwa chini. Maji yakikaa kwenye "trays" zako - ziwe nyungo au makasha ya mabao au ya plastic, ili mradi yawe na matundu yanayotiririsha maji kwa chini! Mimi nataka kutumia "trays" nitakazotengeneza kutokana na MADUMU ya maji kwa kuyakata na kuyatoboa! Hydroponic fodders unaweza kutengeneza kwa kutumia nafaka zozote kama ngano, mtama, ulezi nk. Nutrients pia ni kibiashara zaidi! Unaweka nutrients gani kwenye LISHE ya kitoto chako kama siyo ulezi/mtama/mahindi na karanga tu? Jaribuni mtupe feedback.
 
Nyongeza kidogo, unaweza kutengeneza hizo fodders hata kwa kutumia udongo. Unaweka udongo kiasi kwenye tray na unanyunyuzia maji na kisha unaweka mbegu zako kwa kuzisambaz vizuri juu ya huo udongo; kisha unaendelea na utaratibu wa kawaida wa kumwagilia maji. Udongo unaharakisha ukuaji wa hiyo fodder yako. Pitieni kwenye utube muone kwa wataalamu namna ya kutengeneza hizi fodder hata kwa matumizi ya binadamu. Fuatilieni muone namnaya kutengeneza 'wheatgrass fodder" ambayo hata binadamu unaweza kutumia!
 
Hebu wataalam tujuzeni kuhusu hatua ya "fermentation" ya hizo mbegu. Mbona haielezewi humu? Ni hatua muhimu sana kwenye utengenezaji wa hizi fodders kwani inaharakisha (it speeds) ukuaji wa hizi mbegu kuwa majani (fodders).
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom