Matanzia kizebazeba
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 654
- 630
Booster unachanganya na maji unayomwagilia.Mkuu hii booster ya majani unachanganya na chakula cha kuku au?
Shukran
Booster unachanganya na maji unayomwagilia.Mkuu hii booster ya majani unachanganya na chakula cha kuku au?
Shukran
ina tija sana tena sana - we hujajua tu. faida ya kufuga inapungua kutokana na gharama za kulisha kuwa kubwa.Haya ma Hydroponic fodder ni sawana sungura,Kenyawafugaji wotewakubwa wa Kuku, Ng'ombe hakuna anaye tumia hii kitu, wanao itumia niwale wana uza, yaani anakuwa na kukuwake 6 wa kuzugia kuwalisha fodder au Ng'ombe wake mmoja, ila kiuhalisia hikitu haina tija
Katibu kwa mail tuwasiliane.Mkuu unapatikana wapi na unaweza kunisaidiaje step by step?
Ikiwezekana nije kwajili ya shamba darasa
Chakula hicho ni kwa ajili ya kuku, ndani yake hakuna majani .. na hiyo ni shida sana kwa kuku wetu.
Mm nlipewa hii formula
Kama jina lako!Kilimo cha hyroponic fodder katika picha, inaelekea watu wengi hawajaelewa hii aina mpya ya kilimo cha kuotesha majani kwa ajili ya kulishia mifugo.
Ni kilimo cha kuotesha majani kwa kutumia nafaka zenye virutubisho vingi hasa shairi, ngano, mtama, mahindi
Angalia huyu mkulima katika picha hapo juu. Ametayarisha mbegu zake kwenye try, angalia try za juu zipo tayari kulishia wanyama, inachukua siku sita au saba tangu mbengu zinapomwagwa kwenye try
Chakula cha mifugo kipo tayari mkulima anakiondoa kwenye try tayari kulishia wanyama.
Mkulima analisha ng'ombe
Kuku nao wanafurahia chakula chao.
Nikusaidie kuhusu lipi? niko tayari ...Mkuu naomba unisaidie na mimi
Safi sana mkuu wape maujuzi ... bravo!Kwa wale mliopo sumbawanga mni_pm niwafundishe.... Naijua vizuri.. Karibuni.
Huu utaalamu mzuri sana.Waungwana naamini hamjambo!
Nitangulize shukrani za dhati kwenu wote mnaoutumia mda wenu vyema katika kuhakikisha yale mnayoyaelewa mnawaelekeza wengine.
Leo nataka niwajuze kile nilichokiona baada ya kupata maelezo mazuri kuhusu Hydroponic Fooder.
Kuna mjasiriamali mmoja alitoa maelekezo mazuri kuhusu namna ya kutengeneza chakula bora na kingi kwa mifugo kwa njia ya kisasa. Kweli nilinunua mahitaji na nikajaribu kutengeneza karibia mara mbili, nikawa nakwama.
Baadaye akajitokeza mjasiriamali mwingine akaelezea kwa kina na nashukuru sana kwa sababu alinilenga mimi binafsi kwa kunitumia PM. Nilipojaribu mara hii nilifanikiwa ila changamoto ikaja kwenye nutrients.
Nilifanikiwa kutafuta nutrients na bahati nzuri nikakutana na mtaalam ambaye kweli yeye aliwahi kutengeneza na ana uzoefu; tatizo kwake ni kwamba hana muda wa kufanya kazi hizo kwa sababu ametingwa na ajira. Alinipatia nutrients aina ya ID-Grow Green.
Bwana huyo pamoja na kwamba sikufahamiana naye kabla, alionesha nia ya kutaka kunifundisha na namshukuru Mungu yale aliyonifundisha niliyaelewa vyema.
Leo ni siku ya tatu tangu nimestawisha na naona maendeleo ni mazuri sana. Kwa kila hatua nitakayopitia nitawajuza ili wale wenye nia ya kuyafanyia kazi waweze kufanya huko waliko.
Angalizo: Kuna nutrients ambazo ukizitumia zinaweza zikasababisha madhara makubwa kwa mifugo yako na walaji pia.
Baada ya siku 9 nitakuja na full habari kuhusiana na kile nitakachokuwa nimekizalisha. Wenye nia msikose kuniuliza ili twende wote sambamba kwenye zoezi hili.
Kiukweli ukikutana na mtaalam wala hautatumia muda mwingi kuelewa kinachoendelea. Mimi atakayehitaji maelezo namkaribisha - tena hatua kwa hatua. Kikubwa ni kuandaa muda wa kupeana maelekezo. Ukifanikiwa wewe unakuwa umesaidia jamii.
1. KIlo moja ya mtama / ngano ni Tshs 2,000/= kwa hapa Mwanza, na hiyo ni bei ya rejareja. Ina maana ukinunua kwa jumla utakuwa chini.
2. Kuhusu kiasi cha kulisha ng'ombe mmoja binafsi sijafatilia - mi nafuga kuku, kumu mia wanatumia kilo nne za H.Fooder
Hydroponics Fooder ni nini?
Ni utaratibu wa kuotesha mazao aina ya mtama, ngano, shayiri, ulezi n.k bila kutumia udongo. Ina maana utakachokiotesha kinatumika chote kama chakula kuanzia mizizi hadi majani. Unaotesha kwenye trai na unatumia virutubisho vyenye wingi wa NPK, kwa sasa mimi natumia DI Grow green pamoja na EM na mbegu zinaota vizuri.
Kama wewe ni mfugaji na una shida na uzalishaji wa chakula tuwasiliane ili nikuelekeze.
Trei zipo
Mbegu ziko sokoni
Maji yapo hapo ulipo
Nutrients unaagiza popote
SOP's ndo muhimu na utaelekezwa ...
Uliza jingine
Booster unachanganya na maji unayomwagilia.
Kwa wale mliopo sumbawanga mni_pm niwafundishe.... Naijua vizuri.. Karibuni.
uko wapinauza shayiri gunia mbili kwa anayehitaji
Mkuu, "SOP" ndio nini. ?Naomba msaada hapo..Hydroponics Fooder ni nini?
Ni utaratibu wa kuotesha mazao aina ya mtama, ngano, shayiri, ulezi n.k bila kutumia udongo. Ina maana utakachokiotesha kinatumika chote kama chakula kuanzia mizizi hadi majani. Unaotesha kwenye trai na unatumia virutubisho vyenye wingi wa NPK, kwa sasa mimi natumia DI Grow green pamoja na EM na mbegu zinaota vizuri.
Kama wewe ni mfugaji na una shida na uzalishaji wa chakula tuwasiliane ili nikuelekeze.
Trei zipo
Mbegu ziko sokoni
Maji yapo hapo ulipo
Nutrients unaagiza popote
SOP's ndo muhimu na utaelekezwa ...
Uliza jingine
Standard of Procedures ....Mkuu, "SOP" ndio nini. ?Naomba msaada hapo..
Gram 80 tu, kwani msosi wake kamili ni gm 125 tu kwa siku.hongera mtoa uzi, naona mapinduzi yanaendelea! hv ndege mmoja hasa kuku anastahili kula kiasi gani cha hiyo fodder kwa siku nzima? nahitaji makadirio tafadhali...
ok, thanks!Gram 80 tu, kwani msosi wake kamili ni gm 125 tu kwa siku.
Ok thanksStandard of Procedures ....