Hydom hali ya usalama ni tete!mfanya biashara atekwa,katoa milioni 80 nawakaondokanae

massai

JF-Expert Member
May 2, 2011
653
137
Mfanyabiashara wa mazao anaitwa HANDO na mkulima pia ametekwa na kuchukuliwa kiasi cha fedha milioni themanini, kwa habari zisizo rasmi kwani kwenye kupeana huko sisi hatukuwepo.

Alishikiliwa kwa siku mbili na kati ya waliohusika alikuwepo msoma ramani mmoja ambae baada ya kubanwa walikuta ashawekewa milioni kumi na saba kwenye akaunti yake na ndie alie fanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo.

Sasa siasa inaingia vipi hapa ni kua katika kampeni mbalimbali zinazoendelea kichinichini huyu jamaa ni mfuasi wa CHADEMA na CCM walishasema kua ukitaka kuendelea na kufanikiwa kwa mfanyabiashara lazima uwe CCM.

Kama sio juhudi za wananchi huyu jamaa alikua hatarini kupotea kabisa, polisi walishaelezwa lakini kama kawaida yao huwa wanakwambia uchunguzi unaendelea.

Ndipo wananchi wakajazana kwenye kituo cha polisi baada ya kupiga HAYODA ambayo ni yowe pindi ipigwapo hata kama ulikua haja kubwa inabidi ukatize na kwenda mstari wa mbele kupambana na kilichotokea.

Habari hizi ni za uhakika na ntawapa stori zaidi pindi ntakapo pata.

Nipo hapa Hydom kikazi! Hydom ipo wilaya ya MBULU mkoa wa MANYARA mbunge wa huku ni MUSTAFA AKONAAY kabla yake alikua MARMO ambae kwa sasa ni balozi anaetuwakilisha nchini CHINA.
 
Tumekusoma, pakua jamvini kadri zitakavyoendelea kudondoka.
Hata hivyo wananchi wanayo nafasi ya kudhihirisha wanachokifahamu na si kuridhia wanachokiambiwa.
 
kweli,kama sio juhudi za wananchi yule jamaa angewapa kidogodogo wale polisi namchezo ungeishia palepale.kweli umoja ni nguvu na huyo tajiri anatakiwa kujua uhai ni bora kuliko mali,na kama sio juhudi za wananchi wale angekua ashaimbiwa parapanda,heshima ni jambo la hekima na uheshimu kila mtu.
 
Back
Top Bottom