HUZUNI: Watanzania kuwaaga Watoto, Waalimu na Dereva wa ajali ya Karatu, uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Screenshot from 2017-05-07 13-50-53.png


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Mrisho Gambo, kesho Jumatatu ya tarehe 08/05/2017, Makamu wa Rais wa JMT, Bi Samiah Suluhu ataongoza watanzania wote ktk maombolezo ya msiba wa wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya Lucky Vincent waliofariki kwa ajali ya basi wilayani Karatu hapo jana.



 
Kesho Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ataongoza waombolezaji,wakazi wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dreva waliofariki wilayani Karatu Jana ktk ajali mbaya ambayo imesababisha vifo vya Watoto wa shule ya Luck Vincent ya kwa Morombo Arusha

Kwa mujibu tangazo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwisho Gambo shughuli nzima itaanza saa mbili asubuhi.

MUNGU awe mlinzi mkuu ktk shughuli nzima ya kuuga miili ya wapendwa wetu.

Tunaungana na wazazi,ndugu, marafiki walikopoteza wapendwa wao ktk ajali hii ya mbaya.

Jamii Forum tunashukuru kwa kuonyesha ushirikiano wa maombolezo kwa kubadili rangi ya baadhi background ya website
 
Hivi kuna umuhimu wa mkuu wa mkoa kujionyesha kwa kubandika picha yake kwenye mambo ya msiba kama haya! Hawa wana siasa ni ovyo kweli kweli. Si wangeweka picha za marehemu au hata nembo ya shule? Kichefuchefu!
Anaongeza umaarufu.
 
Huwa nakaa nafikiria wale wanaume walijitoa kwa hali na Mali kuzitoa zile maiti zote kule bondeni au korongoni ndani ya gari bila kujali chochote kile!!

MUNGU ndiye mlipaji wa kila kitu hapa duniani,Nasema MUNGU na awalinde na kuwasahaulisha yote mliyopitia kwa wakati najua nia yenu ilikuwa ni moja tu kuzitoa maiti za wapendwa Watoto wetu.

Kuna wengine inaweza kuwa ndiyo mwanzo wa kupata tatizo lingine kisaikolojia vijana hao nao wanahitaji ukaribu pia wa kisaikolojia maana kuna picha ambayo haitafutika ktk maisha yao.
 
Back
Top Bottom