HNIC
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 1,898
- 2,195
Alikuja kipindi kile Saudi Arabia imevamia Yemen kwa mgongo wa kumrejesha rais aliyepinduliwa na wakati huohuo walikuwa wanasaidia Magaidi kuipindua serikali ya Syria.
Saudi Arabia wakawa na wakati mgumu sana Yemen na mwishowe wakaanza kuzihonga pesa nchi maskini za Afrika ziwaunge mkono kwenye vita yao huko Yemen. Baadhi ya nchi zilikubali na zingine zilikataa.
Huyu waziri wao wa mambo ya nje (pichani hapo juu) moja kayti ya nchi alizokwenda kuomba ni Tanzania.
Nyote mnajua sisi moja ya sera yetu kuu ya mambo ya nje ni KUTOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE. Nimetazama list ya nchi zilizopeleka wanajeshi Yemeni kuungana na saudi Arabia Tanzania haimo na hivyo ni wazi ombi lao lilikataliwa na Rais wetu ambaye sera yake kubwa ni Maslahi ya Tanzania kwanza.
Sasa hivi kuna ugomvi mkubwa kati ya Saudi Arabia na Qatar na saudi Arabia inatumia nguvu ya pesa kuziambia nchi maskini kusitisha mahusiano na nchi ya Qatar.
Natumai kuwa mwanadolomasia nambari 1 wetu waziri Augostino Mahiga atamshauri Mheshimiwa Rais kuwa hatutofungamana na upande wowote kwenye ugomvi wao huko kwenye nchi za GCC na pia Tanzania itakuwa iko Tayari kutumia wataalam wake kuwapatanisha Saudi Arabia na Qatar kwani hiyo ndio sifa yetu. Na hawa wote wanakaribishwa Arusha kuja kupatanishwa.