huyu waziri anawaonya vijana au anawahamasisha kujirusha na mafataki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

huyu waziri anawaonya vijana au anawahamasisha kujirusha na mafataki?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Kichwani, Dec 1, 2010.

 1. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  wadau......

  hapo kwenye hiyo link kuna habari inayomhusu waziri mpta terezya hovisa akisimulia maisha yake chuoni............. eti ali[okuwa cho kikuu alipewa mimba na "fataki" na kisha huyo "fataki" alimsomesha hadi leo ni dr............ hajasema kama huyo "fataki" ndiye aliyemuoa........... fuatilia mwenyewe uone zaidi.............

  Waziri atoa ushuhuda alivyorubuniwa na fatak

  sasa naona maana ya fataki imechukua mkondo mwingine............. natarajia mwanafunzi wa cho kikuu ni mtu mzima na kila anachofanya anakielewa vizuri na madhara yake............ sioni haja ya kutumia fataki hapo ............ pia anasema baada ya kumpa mimba aliendelea kumsomesha hadi leo amefikia u-dr na sasa uwaziri......... sasa nauliza....

  1. hivi huyu fataki ni mbaya kweli?...........
  2. hapo anawaonya au anawahamasisha kujitafutia mafataki wazuri watakaowasaidia kufikia malengo yao ya elimu?............
  3. mwanafunzi wa chuo kikuu amabaye anatarajiwa kuwa mwerevu kuhusu mapenzi na hata masuala ya uzazi wa mpango, anapojiingiza kwenye mapenzi na hata baadaye kupata mimba naye asingizie fataki?..............

  naona mawaziri kama hawa hawajaanza kazi bado............ bado wamelewa na uteuzi................
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  waziri kiherehere
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kwa timu ya mawaziri kama hawa!!.............JK kazi anayo..........
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,420
  Likes Received: 414,718
  Trophy Points: 280
  Waziri atoa ushuhuda alivyorubuniwa na fatak Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 21:23 0diggsdigg

  i Mwandishi Wetu

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Luoga Hovisa jana alitoas ushuhuda wa kusikitisha wa maisha yake katika kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), alipoeleza kuwa alipewa uja uzito na 'Fataki' wakati akisoma Chuo Kikuu.

  Waziri Luoga alilazimika kushirikisha vijana hao kuhusu maisha yake kutaka kuwaonyesha alivyomudu kuvumilia na kupambana na maisha hadi kufikia mafanikio aliyoyapata sasa, akisema badala yake sasa anaweza "kuchakachua" hadi wanaume watano lakini "haoni sababu" na kuwataka wanafunzi kuepuka watu wenye tabia za kifataki kwa kuwa wanaweza kuwaharibia mwelekeo wa maisha.

  Fataki ni jina maarufu waliopachikwa wanaume ambao wana tabia ya kufuata mabinti wadogo na kuwatelekeza baada ya kuwaharibia maisha kwa kuwapa mimba. Waziri Luoga alieleza jinsi alivyokutana na mwanamume huyo ambaye alimpa uja uzito, lakini akaongeza kuwa baadaye mtu huyo alimsomesha na hivyo kumaliza vizuri masomo. "Sio kwamba muige mfano nilioutoa," alisema Waziri Luoga akiwaambia wanafunzi hao. "Si kwamba na nyie kama wanafunzi mkayafanye haya, la asha! Badala yake ninawapa changamoto kwamba katika maisha silaha mnayopaswa kuing'angania ni elimu peke yake na si vibaka wa mitaani," alisema Dk Luoga. "Acheni kudanganywa na mafataki ambao ni matapeli na ambao huweza kuwapotezea dira ya maisha, badala yake msome kwa bidii, kwa ajili ya mafanikio ya maisha yenu." Dk Luoga alisema kuwa vijana wengi, hasa wanafunzi wamekuwa wakirubuniwa kutokana na kushindwa kustahimili tamaa za maisha na kuamua kujiingiza kwa vijana wa mitaani ambao aliwaelezea kuwa hawana sera.

  Waziri huyo, ambaye ni sura mpya katika baraza lililoundwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, alikumbushia taaluma yake ya ualimu kwa kutumia kalamu na kuwafundisha washiriki wa kongamano hilo masuala ya maisha na athari za ukimwi kwa vijana, huku akijitangza kuwa naye ni mtoto wa mkulima. "Ni bora kuacha kabisa na kuamua kusubiri kwani kwa kuwa mahusiano katika masomo ni hatari... badala yake mzidi kumuomba Mungu na kuwa waadilifu," alisisitiza "Leo hii, ninamshukulu Mungu kwa Elimu aliyonipa kwa sababu alinijua mimi ni mtoto wa mkulima, hivyo niliamua kutochezea maisha yangu kiholela. "Hapa unavyoniona, kama waziri nina fedha za kutosha; gari la kifahari ninalo ehe! Unadhani nikitaka kuwa na mafataki hata watano, nitashindwa?" "Nikiamua kuchakachua wanaume hata watano, naweza kwa sababu uwezo ninao na fedha ninayo.

  Lakini sioni faida yeyote badala yake ni kujitumbikiza mahali ambapo ni hatari zaidi," alisema. "Cha msingi hapa ni kuhakikisha mnajenga maadili mema mnapokuwa shuleni na nyumbani ili kuepuka kurubuniwa na kupoteza mwelekeo wa elimu mliopata." Naye mtaalamu wa ushauri wa afya katika kamati ya vijana, Dk Telesphoy Kyaruzi alisema tatizo kubwa linalowapelekea vijana wengi kujiingiza katika ngono zembe na kupata maambukizi ni uchumi mbovu. Dk Kyaruzi alisema kwa kuliona hilo, wanaiomba serikali kuhakikisha inatoa mikopo kwa vijana ili kuwasaidia waweze kujiendesha na kuepuka vishawishi.
   
 5. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kiherehere???
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  KWELI KABISA MKUU.... kazi anayo na ukizingatia jamaa mwenyewe ndio aliwaita viherehere... LOL
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Rais wangu mpendwa aliwahi kusema wanaopata mimba mashuleni ni kiherehere chao... Si mimi bali nime-quote tu kutoka kwenye literature
   
 8. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mcharuko......! Huenda na uwaziri kaupata kwa njia hiyo.....!
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,420
  Likes Received: 414,718
  Trophy Points: 280
  Una uhakika ulimchagua?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  as long as ni rais wa jamhuri... na mimi ni raia basi ni rais wangu; alivyoupata hiyo ni topik nyingine
   
 11. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  dah, mkuu umenikumbusha kauli muafaka sana ya mkuu wa kaya............. kumbe ndio hao waliopata mimba kwa viherehere vyao na sasa anawaambia dada zetu kuwa sometimes viherehere vinalipa.................. aisee!!!...................
   
 12. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  omg!!!
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mbona hii ni obvious...we mtazmae tu anavorembua macho huyo waziri ndo utajua kaupataje huo uwaziri
   
 14. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  huyu mh. waziri ni mbunge wa wapi, au ni wa viti maalum??.......................
   
 15. F

  Ferds JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ushuhuda mzuri coz unatoa picha halisi ya maisha yetu ,na yeye kama mtanzania mwanamke alipitia yanayofanywa na wengi vyuoni, sasa tatizo lake nini hapo hebu someni kwa makini mmpate ujumbe mi naona ni ushauri mzuri tu, au kwa sababu ni waziri, angeutoa mtu wa kawaida kwa lengo lilelile la kuisa jamii ungechukuliwa hivyo mlivyouchukulia, acheni hayo mambo wandugu
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  umesoma tu hujatafakari ndugu yangu.................any way............. ukitafakari zaidi utagundua kuwa anawahamasisha badala ya kuwaonya................
   
 17. F

  Ferds JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Waziri Luoga alilazimika kushirikisha vijana hao kuhusu maisha yake kutaka kuwaonyesha alivyomudu kuvumilia na kupambana na maisha hadi kufikia mafanikio aliyoyapata sasa, akisema badala yake sasa anaweza "kuchakachua" hadi wanaume watano lakini "haoni sababu" na kuwataka wanafunzi kuepuka watu wenye tabia za kifataki kwa kuwa wanaweza kuwaharibia mwelekeo wa maisha.

  nitafakarie hiyo paragrah na unieleze umehamasishwa kudo au otherwise.........................,eti bwana akili kichwani,hebu twende paragraph kwa paragraph, stress iwe ktk mstari uliokoza tafadhali
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani mtu wa chuo kikuu unarubuniwa na fatati ..hapana
   
 19. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  tupeni CV, isje akawa ndo suga mama huyu mama!
   
 20. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  angalia hapo penye colou na bold............. kwa anayejua maana ya kushawishi hawezi kuletaswali zaidi........... anyway, kwa kukusaidia.... sasa anaweza lakini haoni sababu kwa kuwa ni waziri........... alivokuwa chuoi aliweza na aliona sababu na "alichakachua" akafanikiwa kusoma............ ndiyo lugha iliyo nyuma ya maneno hayo na utaipata "ukitafsir"i, sio"ukisoma".............
   
Loading...