Huyu Waziri anamhujumu Rais Magufuli kama kulipa kisasi?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Kwa kauli zake nadhani anamtafutia janga Rais na Watanzania wote kwa ujumla.

Kama kauli hiyo haijatokana na msimamo wa pamoja wa Serikali, ambao nilitarajia utoke baada ya Kikao cha Baraza la Mawaziri, basi inahitaji kuchunguzwa kama kweli ina lengo zuri.

Tunahitani waziri anayeweza kumpunguzia Rais pressure kwa kujikita katika kauli za kidiplomasia.

Kuonesha wazi wazi tena kwa njia ya matusi kuwa hukufurahishwa na maoni ya Wabunge wa Bunge la EU, ni udhaifu.

Hata hivyo nina wasi wasi huenda hii ikawa hujuma iliyofanywa kisomi sana.
 
Hatujawahi kushindwa Vita yoyote, so kama wanajiandaa iwe kwa vita ya Vikwazo, vita ya kigaidi itakayopelekea majeshi yetu yawe sungusungu kwenye mpaka wetu na Msumbiji poa tu, sisi tupo tayari. Hata hao Magaidi wa Msumbiji wakitaka kuvuka mpaka kuja kuteka Westgates zetu wajue tupo tayari.

Hatujawahi kushindwa.
 
Aloo naungana na wewe mtoa mada Kabudi alichofanya ni kwenda kuchokoza mambwa alafu yeye kawahi kupanda juu ya mti then yale mambwa yataanza kumkimbiza Jpm kwa sababu hajajiandaa.Alafu Kabudi kule juu ya mti anabaki anacheka the way jpm anavyosumbuka na yale mambwa chini.
 
Kiburi si uungwana! Kabudi anapaswa kujifunza kutokana na msemo huu.
 
Ikiwa bosi wake ndo amekaimu mamlaka yote na kuziendesha idara na taasisi zote kama anavyo weza yeye. Ni dhahili kuwa alilishwa maneno na bosi wake, hatuitaji kujiuliza mara mbili.
 
Hatujawahi kushindwa Vita yoyote, so kama wanajiandaa iwe kwa vita ya Vikwazo, vita ya kugaidi itakayopelekea majeshi yetu yawe sungusungu kwenye mpaka wetu na za Msumbiji poa tu, sisi tupo tayari. Hata hao Magaidi wa Msumbiji wakitaka kuvuka mpaka kuja kuteka Westgates zetu wajue tupo tayari.

Hatujawahi kushindwa
Kama tulishindwa vita rahisi kabisa ya bei ya sukari, unadhani hiii ya Ulaya tutaiweza kaka? Kikubwa tukae tuweke mikakati namna ya kujenga jina na diplomasia yetu kimataifa. Hakuna aliyweza kubishana na mabeberu akabaki salama
 
Back
Top Bottom