Huyu tumsaidieje?

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,465
11,166
Nanukuu-:

"Mimi ni mama wa watoto watatu, nimelewa na ndoa yangu ina miaka kumi sasa, sababu ya kuja kuomba ushauri nikuwa, mwanzoni mume wangu alikua ni mtu wa kunywa pombe, si sana lakini mara nyingi alikua ni mtu wa kuchelewa kurudi nyumbani, siku za kazi ilikua ni lazima kupitia baa na kurudi kwenye saa tatu na wakati mwingine mpaka saa nne usioku.

Hakua akinipiga wala kuninyanyasa, alikua anafanya kazi vizuri na familia anahudumia vizuri sana, hali ile ilikua inanikera sana kwani weekend ndiyo mambo yalikua mabaya kabisa, alikua akichelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine alikua akirudi mpaka saa nane usiku. Tulikua tunagombana kila siku kuhusu yeye kuacha pombe lakini alikua hasikii. Alikua akiniambia kuwa pombe ndiyo inampa madili na kumkutanisha na watu mablimbali wenye pesa.

Mimi sikukubali kwani niklijua kuwa huko ndiyo anakutana na wanawake, ingawa nilikua sijawahi kumfumania lakikini ile hali ya kunwa kila siku ilinikera. Nilianza kufunga, kusali na kumuombea lakini hakuacha na sanasana alikua akinishangaa akiniamia kuwa yeye si mgonjwa anakunywa kwa starehe. Sasa mwaka jana mwanzoni nilienda kanisa moja Lipo Mbezi, ni haya makanisa ya kuombea, nilionana na mchungaji na kumuambia tatizo langu.

Alikubali kunisaidia, nilimbembeleza mume wangu kwenda kanisani mpaka akakubali akawa anasali katika lile kanisa. Kweli haikupita miezi miwili mume wangua laicha kabisa kunywa pombe, akawa akitoka kazini sa akumi na moja tu yupo nyumbani na kama akitoka ni kanisani. Nilifurahia sana kwani nilikua namuona mume wangu nyumbani. Lakini kaka liliibuka tatizo jingine ambalo limenifanya hata kutamani mume wangu arudie pombe. Sasa hivi mume wangu amekua ni mtu wa kanisani tu.

Kitoka kazini ni kusali na kuka anyumbani, kila kitu kimekua ni mchungaji mchugaji, anafanya kazi lakini zaidi ya nusu ya mshaahra wake unaishia kutoa sadaka, watoto tumeshindwa kwapeleka shule kwakua pes aanapeleka kwenye kazi ya Mungu, kila kitu anamsikiliza mchungaji, mara uitasikia kuna kanisa linajengwa, mara kuna matoleo na mambo mengine mengi. Mbaya zaidi anauza vitu vya nyumbani ili kutoa sadaka, alishauza gari eti kwakua mchungaji alitakiwa kusafirio nnje, anachukua mpaka vitu vya ndani, yaani mchungaji akitaka pesa na yeye hana anachukua ndani na kumpelelekea.

Nimechoka kaka sijui nifanye nini ili mume wangu kuacha tabia hii, nikilalamika anakua mkali na atamuita mchungaji itakua ni maombi kutwa nzima, wananikemea kuwa nina mapepo napingana na kazi ya Mungu. Kaka sisi tulikua tunasali Katoliki lakini sasa hivi mume wangu hataki kusikia cha kanisa jingine, amegombana na wazazi wake kwakua hawahudumii tena kwani hana pesa zote zinaishia kanisani katika kupandambegu. Kaka naomba nisaidie nifenye nini, mume wangu alikua ni mtu wa madili kazini, lakini sasa hivi anaishi kwa kutegemea mshahara ambao hata hautoshi kwani asilimia kubwa inaenda kanisani, ficha jina langu ila naomba ushauri wako."

Mwisho wa kunukuu.

Hebu tusaidiane ni jinsi gani tumsaidie aweze kuepukana na haya yanayomsibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ulitaka aache pombe ili amjue Mungu.
Sasa kamjua Mungu na Mungu kampokea kwa mikono yote.

Yaani ukimtoa huko, utajuta mwenyewe.
Ongea naye pole pole na kwa ukarimu wa hali ya juu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii chai, story za kutunga

Kwa sisi watungaji Wa story za uongo na ukweli huwa tunajua tu lipi kweli na lipi la uongo

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna mambo mengi bado hujayajua ama kutokana na umri mdg ama kuishi ki maigizo.

hakuna mchungaji hapo, huyo kalishwa dawa ya kunyenyekea.namfahamu mzee mmoja aliye uza nyumba,gari kutokana na kudanganya na mpumbavu 1 (anaye jifanya mchungaji)
 
Ok waiter fungua hilo bapa then mimina kidogo kwenye glass. Halafu yule jamaa wa kitimoto mwambie asije ila nenda pale kwenye jiko jingine mwambie jamaa aandae roast ya figo na ugali moja na chips kavu plate moja coz Joanah anakuja kula lunch hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahahahh
Hapo umenishawishi sasa
 
Huyu jamaa aidha kachukuliwa na mchungaji kama wale wazungu
Ama ni brainwashed

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom