mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,193
- 6,381
- Thread starter
- #81
Ahsante kwa elimu MkuuKwanza tuelewe mizunguko (guarding circles) inayomlinda Mh Rais. Tukiachana na mzunguko huo ambao umo ndani ambao hatuuoni, kuna mizunguko mitatu iliyo dhahiri katika video.
Mzunguko wa tatu upo huo wa polisi pamoja na wanausalama waliovalia kaunda suti. Unaona kabisa Trafki anaupita na kujitokeza kuukabili mzunguko unaofuata. Hao walijisahau kabisa.
Mzunguko wa pili ni huo wa Wanajeshi walioshikilia mitutu mikubwa mikubwa.
Ukiangalia kwa umakini, kuna mwanajeshi mmoja anamnong'oneza afisa (katika mzunguko wa tatu) kitu. Kumnong'oneza huko kukamfanya kupoteza focus ya kuangalia kwa umakini
Isingelikuwa huyo mwenzake kumuwahi huyo Trafiki na kumuamuru asipite huko bila shaka angelipita karibu kabisa na circle ya kwanza.
Mzunguko wa tatu, unahusisha wanausalama wengine pamoja na huyo mnayemwita Mpambe. Baada ya kuamuriwa kwa kusukumwa trafiki analazimika kupita katikati ya mzunguko wa pili na wa tatu.
Trafiki alifikaje?
Kwanza ametumia advantage ya yeye kuwa sehemu ya usalama. Amevalia kitrafiki.
Akapata upenyo kusogea ndani zaidi.
Lakini tukubali kuwa kuna uzembe ulifanyika wa kumpuuzia.
Hata baada ya kusukumwa anaondoka kwenda kumuagamia mwanausalama kiunoni. Sijui ni makusidi ama kukosa balance.
Huenda ni makusudi kwa kuwa hakusukumwa kwa nguvu sana. Ni kidogo tu. Lakini pia, askari anatakiwa awe mkakamavu, force kidogo kama ile si ya kukuyumbisha kutaka kuanguka.
Huenda si makusidi kwa sababu:
Uoga ulichangia kukosa balance. Nafasi baina ya aliyesukuma na aliyetaka kumuangukia haikuwa ya kutosha.
Je, ni threat?
Hapana, kwa sababu hakusababisha usumbufu wa aina yeyote. Alishindwa kuelewa mipaka yake, mahali anapotakiwa kuishia.
Ila uzembe umefanyika kwa kikosi kushindwa kumzuia kutofika huko