Huyu Tajiri wa Mabasi ya Mbulu Trading Co. Ltd(au Sunvic Express Ltd) Ameiweka Serikali Mfukoni km yule Mgiriki wa Mwl. Nyerere?

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,131
6,131
Kuna Kampuni ya mabasi inayofanya safari zake kati ya Arusha na Haydom kupitia Karatu na Mbulu km ilivyotajwa hapo juu. Ktk kibali chake cha biashara ilitakiwa kila siku iwe inasafirisha mabasi manne, mawili kutoka Arusha kwenda Haydom(basi la kwanza inatakiwa iondoke saa 12 asubuhi na la pili saa 2 asubuhi) na mawili kutoka Haydom kwenda Arusha(basi la kwanza inatakiwa iondoke saa 12 asubuhi na la pili saa 2 asubuhi), Jumla mabasi manne. . Kiuhalisia sahivi kampuni hii inatoa huduma kutumia basi moja tu badala ya mabasi manne. Yaani leo km inaenda Haydom kwenda Arushahakuna basi la kutoka Haydom kwenda Arusha. Na hiyo safari moja basi linajaza abiria na mizigo kupindukia hakuna pakupitisha mguu wakati huo hakuna polisi anayehangaika kulisimamisha wao wanachukua tu pesa zao wala hawachungulii ndani ya basi. Ikifika Makuyuni wanawapakia baadhi ya abiria kwenye Hiace kukwepa mizani ya Makuyuni.

Hatulalamikii kupeleka basi moja, tatizo tunaambiwa LATRA imekataa kusajili mabasi mengine ktk route tajwa kisa tajiri wa Sunvic Express analipia time table zake zote kwa maana haruhusiwe mtu mwingine yeyote kuitumia hiyo route ni mali yake ana hati miliki nayo. Huyu mkalasinga(Mhindi) hakuna mamlaka inamgusa, hagusiki. Hata km hatatoa basi hata moja hakuna anayeweza kutumia hii njia. Kwa mfano leo Jumapili hakuna hata basi moja lakini hakuna wa kusafirisha abiria, itabidi uunganishe kutumia magari matatu mpaka ufike Haydom. Upande mpaka Karatu(Sh. 8000), then Mbulu(Sh. 6000) na mwishowe Haydom(Sh. 6000). Jumla ya gharama Sh. 20,000 badala ya sh. 14,000/= ya LATRA(Serikali).

Kimsingi LATRA na Polisi mikoa ya Arusha na Manyara wamenunuliwa na huyu tajiri. Tunaomba LATRA kitaifa na wizara husika itusaidie wananchi wake aidha kwa kumnyanganya huyu tajiri mwenye kiburi na kudharau serikali hii njia wapewe watu wengine watakaoheshimu sheria za nchi yetu na kutujali watanzania ktk nchi yetu. Wapewe Kibali matajiri wengine. Hawa watu wa mizani Makuyuni na polisi kitengo cha Tarfiki wamulikwe kuna rushwa ya wazi hapa.

Idara ya kazi na vyombo vingine vya serikali vimulike kampuni hii, wafanyakazi wananyanyanswa sana, hawana mikataba ya kazi, hawana NSSF, mfanyakazi anafukuzwa wakati wowote. Tajiri anatukana wafanyakazi kwa lugha ya udhalilishaji uliopitiliza, hakuna utu wa kibinadamu. Huyu mhindi km anaona watanzania siyo watu arudi kwao pengine ataheshimu wahindi wenzie. Karne hii tunanyanyaswa na mtu moja wakati matajiri wenye mabasi ni wengi na wanatafuta njia. Katika ukanda huu yapo makampuni kama Jesus Love, Ally Shoko, Mtei Express, Lakrome, Makara na wengineo aachie Njia na LATRA iache kuumiza wananchi kwa kuchukua rushwa wanatuumiza wananchi.

Ruti ya saa 12 asubuhi alishaiua miaka mingi iliyopita na hakuna basi lingine linaruhusiwa kisa Mkalasinga(Sunvic) anailipia, lengo la serikali ni kulipia huduma hewa au kinacholipiwa ni kitu gani. Mtu analipia huduma ambayo haipo, hiki ni kitu gani? Wananchi tunataka huduma.
 
Mbunge wako hapo ametokea chama gani?,why kama tatizo hilo linawagusa wengi msigomee services hizo?why hamfanyi service protest?,na why ukimbilie huku wakati huku hakuna solution yeyote au ndio yale yale kukimbilia kwenye key boards, huyu mtu aliyetugeuza mazuzu alipatia mno (mimi sio zuzu)
 
Mbunge wako hapo ametokea chama gani?,why kama tatizo hilo linawagusa wengi msigomee services hizo?why hamfanyi service protest?,na why ukimbilie huku wakati huku hakuna solution yeyote au ndio yale yale kukimbilia kwenye key boards, huyu mtu aliyetugeuza mazuzu alipatia mno (mimi sio zuzu)
Halafu huko anapopataja Unadhani kuna kitu cha maana basi
 
mleta uzi unazingua... nina uhakika hakuna mtu mwenye basi lake la maana atataka kulipitisha kwenye hiyo ruti hasa kuanzia Karatu hadi Haydom kwasababu sio lami. Jiulize kwanini kutoka Karatu - Mbulu zinazotamba ni Land Cruiser? jibu ni barabara mbovu. Isitoshe watu wa Mbulu wana option ya kupitia njia nyingine ya Mbulu - Magara - Arusha badala ya huo mzunguko wa Karatu. Hiyo barabara ikishatiwa lami patachangamka. Tutumie muda huu kumshukuru Sunvic kwa kutoa huduma kwa zaidi ya miaka 40 kwenye hiyo njia. Sema Sunvic ni basi ambalo ukipanda inatakiwa usiwe na haraka.
 
Back
Top Bottom