Huyu spika wetu vipi?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
jamani mie sijaelewa kabisa ilikuwaje mheshimiwa spika akafanya utafiti huu.

hebu tliangalie na kulijadili

Spika afichua siri za wanaume wanaopewa kibano na wake zao

2008-04-10 15:46:28
Na Sharon Sauwa, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Samuel Sitta amewaacha hoi waheshimiwa wabunge alipotoa taarifa ya utafiti kuhusu wanaume wanaopigwa na wake zao.

Baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu, Spika alieleza kuwa ana ujumbe kutoka kwa mmoja wa wabunge ambaye amemuomba kurudia taarifa yake kuhusiana na utafiti huo.

``Nimepata ujumbe hapa tena kutoka kwa mheshimiwa mwanamke ambaye ananiomba nirudie kutamka kuhusiana na utafiti,``akasema.

Spika alisema utafiti unaonyesha asilimia 35 ya wanaume wanapigwa na wake zao ingawa hawasemi kutokana na kuona aibu.

Akasema hata kesi za namna hiyo haziripotiwi polisi kutokana na akinababa hao kuogopa kuchekwa.

Akasema asilimia hiyo inajumuisha pia waheshimiwa wabunge wanaume wanaokandamizwa makonde na wake zao.

SOURCE: Alasiri
 
duh mie siamini nnasikia ana vijumba kila kona halafu awe victim?

lkn chanzo cha kufanya utafiti huu ni nn?
 
duh mie siamini nnasikia ana vijumba kila kona halafu awe victim?

lkn chanzo cha kufanya utafiti huu ni nn?

may be Victim ndio maana anatafuta hivyo vijumba: any way haya ni ya kwake binafsi. Hivi suala la EPA, mikataba ya madini bado halijazungumzwa bungeni wiki hii
 
Jamani give him a break I think he was just having fun. Si unajua tena wakati mwingine jokes na story za hapa na pale zinafurahisha bunge.
 
Yale yale ya kufanyia mzaha kila kitu! Domestic violence si kitu cha kutania hata kama victim ni mwanaume.
 
Yale yale ya kufanyia mzaha kila kitu! Domestic violence si kitu cha kutania hata kama victim ni mwanaume.

Hebu fikiria, Fundi Mchundo, Spika wa nchi hajui hicho ulicho kisema hapo. Na yule mbunge wa kike pia aliyedhani ni poa tu, utani tu. Hebu fikiria. Halafu Wabunge woooote, sijui mia ngapi, hamna hata mmoja alisimama kumpinga Spika na mbunge wake. Halafu magazeti nayo yameichukulia kama hadithi ya kawaida tu.

Hebu ona, Spika mzima! Yani hao ndio watu wanaingoza nchi yetu. Kazi ipo!
 
jamani Spika,

Mie simwamini mtu sasa,Viongozi hawa nani kawachagua???

Au ndio kasi na viwango hivi??
 
labda spika alitaka kuwajuilisha watanzania mbali ya kuwa tunawatetea wanawake wapate haki zao lakini na wao ndio wavunjaji wakubwa wa haki

ila kwa vile wanaume wanaona aibu ndio wanaogopa kutamka waZi

huenda anataka uanzishwe mjadala wa kuwaadhibu kisheria kwa akina mama wanaowapiga waume zao the same as them
 
im sure JAKAYA ataunda tume kuinvestgate hii issue..tusubiri mieze sita...
 
jamani mie sijaelewa kabisa ilikuwaje mheshimiwa spika akafanya utafiti huu.

hebu tliangalie na kulijadili

Spika afichua siri za wanaume wanaopewa kibano na wake zao

2008-04-10 15:46:28
Na Sharon Sauwa, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Samuel Sitta amewaacha hoi waheshimiwa wabunge alipotoa taarifa ya utafiti kuhusu wanaume wanaopigwa na wake zao.

Baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu, Spika alieleza kuwa ana ujumbe kutoka kwa mmoja wa wabunge ambaye amemuomba kurudia taarifa yake kuhusiana na utafiti huo.

``Nimepata ujumbe hapa tena kutoka kwa mheshimiwa mwanamke ambaye ananiomba nirudie kutamka kuhusiana na utafiti,``akasema.

Spika alisema utafiti unaonyesha asilimia 35 ya wanaume wanapigwa na wake zao ingawa hawasemi kutokana na kuona aibu.

Akasema hata kesi za namna hiyo haziripotiwi polisi kutokana na akinababa hao kuogopa kuchekwa.

Akasema asilimia hiyo inajumuisha pia waheshimiwa wabunge wanaume wanaokandamizwa makonde na wake zao.

SOURCE: Alasiri

Kuna wakati wabunge wanakosa mambo muhimu ya kuzungumza. Ushauri wangu kwenu wabunge: Ikiwa mtakosa mada za kuzungumzia basi zungumzeni kuhusu "Mfumuko wa bei"Lakini si huo upuuzi mnaozungumza, kumbukeni mna siku chache sana kujadili mambo muhimu ya kitaifa.
 
labda spika alitaka kuwajuilisha watanzania mbali ya kuwa tunawatetea wanawake wapate haki zao lakini na wao ndio wavunjaji wakubwa wa haki ila kwa vile wanaume wanaona aibu ndio wanaogopa kutamka waZi huenda anataka uanzishwe mjadala wa kuwaadhibu kisheria kwa akina mama wanaowapiga waume zao the same as them

Anhaaaa, sawa. Kumbe kitu kidogo tu. Spika ameshindwa ku spiki.
 
Haki Sawa Walizopata Toka Beijing Wanazitumia.nimewahi Kusikia Wapo Wanaume Toka Mkoa Mmoja Wanadai Chama Cha Kuwatetea Kama Wabeijing.inaweza Kuwa Kweli Lakini Akamilishe Utafiti Wake....
 
According to the dataz, alishtengana na mama for the last ten years, huwa ana dogo dogo saizi ya mjukuu wake na huwa haishi na mama tena kwa hiyo ile sherehe majuzi ya ndoa miaka 40 na rais ndani ilikuwa geresha tu...., nasikia sasa anaunyemelea nyemelea urais 2010.....alishaanza kujiweka sawa el alikuwa mwiba wake sasa ameuondoa.....huenda hizi nyepesi nyepesi anazozitoa bungeni ndio kampeni yenyewe hiyo imeanza maana bongo huwezi jua.....!
 
Mimi nashangaa sense of humour yetu kama jamii! Tunachekelea kweli suala la domestic violence? Au tunaona inachekesha kwa sababu tunaona ni halali kwa mwanaume kumdunda mke wake na si vinginevyo? Hii kukubali hali kama hii ndiyo inayopelekea matendo kama haya niliyoyaainisha hapa chini. Je tungecheka ingekuwa mwanaume anatendewa hivyo? Na sasa kwa vile wale wanaostahili kufanyiwa hivi ndiyo yamewapata tunaona safi tu?

Huyu hapa amemkata mke wake mikono na vidole kwa kutoanua nguo mapema!

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/04/07/111884.html

Na huyu amemchinja mke wake baada ya kumfumania!

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/04/08/111993.html

Mimi naona kwa kulifanyia mzaha suala hili, Spika hakuitendea haki jamii. Vitendo hivi vimeshamiri mno katika jamii yetu.
 
According to the dataz, alishtengana na mama for the last ten years, huwa ana dogo dogo saizi ya mjukuu wake na huwa haishi na mama tena kwa hiyo ile sherehe majuzi ya ndoa miaka 40 na rais ndani ilikuwa geresha tu.....!

Kweli ukubwa kazi, yaani hairuhusiwi kuachana na mai waifu wako hata kama mmeshaboana vya kutosha. Mnagombana lakini mkiwa kwenye public mnachekeana kama hakuna baya lolote ......... Nilikua napita maoneo ya kimara nikaona bango la 40th anniverasary, baada ya siku moja ndipo niliposoma kwenye gazeti kua ilikua ni anniversary ya mzee 6..... Halafu Mkuu FMES unasema ilikua usanii? Teh...teh ... teh...

Heri mi nisiyefahamika nina tunyumba tudogo tuwili, kamoja magomeni mikumi na kengine kinondoni LOL.
 
hii geresha ya kuwa wanatimiza miaka 40 hali ya kuwa wameachana miaka 1o kali

sasa wanamgeresha nani?
 
CCM majuzi tumeambiwa wanaongoza na ndiyo sehemu ya kampeni yao na maadili hayana maana kwao.Humu humu tulitamkiwa kwamba ni madume ya mbegu sasa sitashangaa mzee na u comedian wake .
 
Back
Top Bottom