Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
jamani mie sijaelewa kabisa ilikuwaje mheshimiwa spika akafanya utafiti huu.
hebu tliangalie na kulijadili
Spika afichua siri za wanaume wanaopewa kibano na wake zao
2008-04-10 15:46:28
Na Sharon Sauwa, Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Samuel Sitta amewaacha hoi waheshimiwa wabunge alipotoa taarifa ya utafiti kuhusu wanaume wanaopigwa na wake zao.
Baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu, Spika alieleza kuwa ana ujumbe kutoka kwa mmoja wa wabunge ambaye amemuomba kurudia taarifa yake kuhusiana na utafiti huo.
``Nimepata ujumbe hapa tena kutoka kwa mheshimiwa mwanamke ambaye ananiomba nirudie kutamka kuhusiana na utafiti,``akasema.
Spika alisema utafiti unaonyesha asilimia 35 ya wanaume wanapigwa na wake zao ingawa hawasemi kutokana na kuona aibu.
Akasema hata kesi za namna hiyo haziripotiwi polisi kutokana na akinababa hao kuogopa kuchekwa.
Akasema asilimia hiyo inajumuisha pia waheshimiwa wabunge wanaume wanaokandamizwa makonde na wake zao.
SOURCE: Alasiri