Huyu single mother nasitisha mara moja kumuoa

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,063
3,685
Hapo vip!!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi ni mtu ambaye nilikuwa siamini katika kumuoa single mother ila baadaye nikajikuta nimekutana na single mother nikaona nitengue msimamo wangu ila kwa hili msimamo wangu narudi kuiheshimu.

Mnamo mwaka huu mwezi wa January, nimekutana na mdada mmoja ambaye tulimaliza naye chuo, na kwa bahati nzuri nilikuwa nasoma naye course moja na pia tulikuwa group moja kwenye discussion. Hivyo na mfahamu kwa kiasi alikuwa ni binti mwenye msimamo kwenye mahusiano.

Kipindi hicho sikuweza kumtongoza kwasababu nilikuwa nipo kwenye stress kubwa wakati nasoma university.

Ila ilikuwa namkubali kubali kiasi, ila wakati tukiwa mwaka wa tatu akakutana na jamaa alikuwa ni graduate na anakazi. Jamaa akafanikiwa kumuweka kwenye himaya yake. Kwangu haikuniumiza sana kwa kwasababu sikuwahi kumtongoza akanitoe nje.

Siku zikaenda jamaa akaenda kujitambulisha kwa binti, ikapangwa mpaka siku ya harusi na vitu kwa hivyo.

Jamaa akawa anahairisha harusi mara kwa mara ila kafanikiwa kuzaa naye mtoto, ila baadaye wakaingia kwenye misuguano wakavunja uhusiano na sababu mwanamke anasema jamaa alikuwa na mwanamke mwingine na mpaka sasa eti jamaa anaishi naye na amezaa naye mtoto, anyway mwanamke akamchukua yule mtoto aliyezaa na jamaa akampeleka kwa wazazi wake.

Mpaka nakutanane naye ameachana na jamaa na kwa takribani miaka mitatu. Anyway baada ya kunieleza hayo kwa uchungu nikaanza naye mahusiano baadaye nikaona kwasababu ni mwanamke ambaye namfahamu kitabia tokea nikiwa chuo acha nifumbe macho nifanye haraku za kuweka ndani kwa heshima.

Anyway baada ya kuanza naye mahusiano akapata ujauzito nikaona ili nisimkweze na aone nipo sereous naye ngoja nikamtambulishe, nikampeleka home kwa utambulisho.

Nikawa nimebakiza kibarua ya kwenda kwao ambaye mpaka sasa sijaenda bado.

Sasa leo akanipigia simu akaniambia amepata msiba, nikamuuliza nani akasema baba mkwe wake wa zamani na waenda na dada yake. Anyway sikutaka kumcrash.

Ila nimeona nipate muda wakutafsiri hiyo picture na kujiuliza maswali mengi.

1. Binafsi najiuliza kama ametoka misri na ameamua kwenda Caana kwanini anarudi nyuma

2. Na kama wameachana na hawakufunga ndoa na ameshatambulishwa katika familia nyingine anaenda kule kama nani...?na kwasababu gani hasa...?

Binafsi nikaona huyu anacheza na akili yangu kwasababu kama yupo sereous akesahau kule pa zamani na kusonga mbele na njia mpya...

Mimi ni mtu ni kazi yangu na biashara zangu, sasa naona kwasababu hana kazi labda anaona apate mahali ambapo atapunguza makali fulani ya stress za mahusiono na maisha may be.

Binafsi naona niwe naye karibu amzee yule kiumbe then niangalie ustarabu mwingine ila asilani sintoweza kumoa tena...m
Unakaribishwa kwa ushauri

MREJESHO

Baadaya ya huyu mwanamke kurudi kwenye msiba,nimekaa nikitafakari sana kitendo hicho.

Alikaa siku siku tatu mpaka akamaliza matanga,sijajua alivyoonana na x wake wamezungumza kitu gani...()

Kiukweli,alipo rudi kutoka kwenye msiba nilimkwepa kama week tatu hivi kwasababu bado stress zilikuwa juu ila kwa simu tunawasiliana naye kama kawaida.

Baada ya week tatu nilimuomba tuonane,baada ya kukutana tulionger japo mongezi yetu hayakujikita kwenye mambo ya msiba.

Lengo kukutana naye nikutaka niwe naye karibu sana kwasababu kwanza nimjamzito lakini pili nipata nafasi ya kumsoma na kujua nguvu ya mahusiono yake ya nyuma.

Nilimuambia aje tukae naye kwasababu ni mjamzito ili niweke mikakati ya kwenda kwao kujitambulisha ila lengo ni kutaka kujua yale mahusiano x.wake yanapo nguvu kiasi gani..

Alikubali kuja tukaanza kuishi kama kawaida ,hiyo mimba ina miezi minne kipindi hicho.

Anyway,mimi ni mtu ambaye nipo busy sana kwasababu ya maswala yangu ya biashara na kazi za hapa na pale..hivyo nikitoka saa mbili asibuhi narudi saa nne usiku au tano..nikirudi ni kula na kulala nakula mzigo kimtindo.

Baadaya week tatu leo nikasema ngoja nishinde nyumbani na huyu mwanamke ..embwana saa tatu asubuhu nageuke hivi nakutana na miss call kama 8 na namba hazijasaviwa kabisa zimepigwa kwenye simu ya mwanamke huyu.

Nikamgeukia nikamgusa bega nikamuuliza baby huyu ni nani kakupigia simu nyingi hivi..
Mimi:Nani kakupigia misscall nyingi kiasi hichi?
Mwanmke:simjui
Mimi:huyu anaonekana ni mtu anayekufahamu kwasababu kakupigia mara nyingi sana..

Mwanamke:simjui
Mimi:basi mpigie alafu weka loud tusikie anasema nini?
Mwanake: aah!aah!sawa!

Simu inapigwa na mwanake

Mwanamke:Hello

Jamaa:mbona hupokei simu yangu?

Mwanamke;unasema

Jamaa:mbona haupokei simu yangu unakwanza nini?

Mwanamke:kimya

Jamaa:upo wap sasa?

Mwanamke:nipo kwangu
Nb..hajasema nipo kwa mume wangu hivyo acha kunisumbua......??????
Jamaa:naomba tuonane kesho akataja mkoa
Mwanamke:kimya

Baada ya hayo mazungumzo nikamuuliza mwanamke huyo nina anaongea na wewe na anaoneka anamamlaka na wewe.
Mwanamke:ni yule x wangu ananisumbua.

Baada ya hapo nilishuka kitandani kama upepo nikaenda kutafuta konyagi mahali ilipo.

Anyway,nilitafakari na kusema bora nimejirizisha juu ya hili ila kwasababu nimjamzito nitakaa naye,alafu siku anaenda kujifungua ndio bye,bye mazima
Naona mwanamke wa design hii atakuja kunisababishia pressure na kisukari mapema.

Na inaonekana siku tukikwaruzana naye kwenye mahusiano nirahisi sana kukimbilia misri

Nimekaa naye ila ameniona nimebadilika sana,na naonekana ni mtu ambaye hana tumaini tena kwenye hayo mahusino baada ya hapo.. akaendakujifungua na baada ya hapo nikamuambia safari yetu imeshindikana hivyo tuwe wazazi tu.na bahati nzuri kanizalia binti amefanana sana na mimi na anamiezi kumi sasa.

Sasa hivi natafuta fresh girl niweke ndani mazima,japo kama nimekata tamaa na hawa viumbe.
 
Mbona sioni tatizo hapo, kumbuka wawili hao wameunganishwa na mtoto/watoto, it's obvious kwamba kukiwa na tatizo upande wowote lazima wahusiane, like it or not.

Muunganiko wa wawili hao upo relevant as long as mtoto/watoto wapo kwenye equation, bear it in your SKULL...

The best solution ni wewe kutembea mbele maana sioni ukiweza kuhimili hizo purukushani.
 
Aiseee.

Kuna lingine liliwahi kujitokeza kabla ya msiba au!?

Single moms kuna mambo ya kuyaepuka baada ya kuingia kwenye mahusiano mapya as tayari kuachana na baby daddy wako tayari muhusika utayekuwa nae na jamii kwa ujumla wanakuangalia vibaya.

Lakini pia nyie step father's pia mjikague vizuri bora kumuacha single mom na hamsini zake kuliko kumuongezea hamsini nyingine halafu unamuacha vile vile.

Mwisho kabisa wanawake kama wanaume wenyewe ndio hawa wa kutusema sema kila kukicha, ifike sehemu mahusiano waachie wengine kuwa busy kulea mwanao. Maana inakuwa kama wanawake wenye watoto ndio Wana matatizo sana.

Wanasahau kunà wanawake hawana watoto ila wamezika watoto idadi kubwa kwa abortions
 
Nimesoma mwanzo mwisho nikahisi nitakutana na kosa kubwa la binti kukengeuka, kwa mtazamo wangu kwenda msibani tena msiba wa babu wa mtoto wake/wenu si jambo baya.....Kuachana si uadui wa kufikia kushindwa kufarijiana hata katika msiba. Kama ana busara atafanya kilichompeleka na kurudi kwako.

Na anatakiwa akuombe ruhusa, endapo mtoa ruhusa utagoma kutoa ruhusa basi bibie asilazimishe.
 
Yote hayo ni kwa ajiri ya kwenda msibani tu!?
Msibani wanamjua kama nani?

Tajiri Tanzanite kabla hujaamua mpe nafasi, muulize taarifa za msiba umepataje? Unaenda wewe kama nani? Huo msiba unakuhusuje? Mwisho kabisa kataa katu kata asiende, kama ataenda kwa kulazimisha basi iwe ndio mwisho wako na yeye full stop.

Mwanaume kuwa na maamuzi magumu lakini yenye demokrasia.
 
Hapo vip!!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza...mimi ni mtu ambaye ilikuwa siamini katika kumuoa single mother ila baadaye nikajikuta nimekutana na single mother nikaona nitengue msimamo wangu ila kwa hili msimamo wangu narudi kuiheshimu.

Mnamo mwaka huu mwezi wa january...nimekutana na mdada mmoja ambaye tulimaliza naye chuo..na kwa bahati nzuri nilikuwa nasoma naye course moja na pia tulikuwa group moja kwenye discussion...hivyo na mfahamu kwa kiasi alikuw ni binti mwenye msimamao kwenye mahusiona.

Kipindi hicho sikuweza kumtongoza kwasababu nilikuwa nipo kwenye stress kubwa wakati nasoma university.

Ila ilikuwa namkubali kubali kiasi...ila wakati tukiwa mwaka watu akakutana na jamaa alikuwa ni graduate na anakazi...jamaa akapapanda akafanikiw kumuweka kwenye himaya yake...kwangu haikuniumiza sana kwa kwasababu sikuwahi kumtongoza akanitoe nje.

Siku zikaenda jamaa akaenda kujitambulisha kwa binti...ikapangwa mpaka siku ya harusi na vitu kwa hivyo.

Jamaa akawa anahaerisha harusi mara kwa mara ila kafaniliwa kuzaa naye mtoto...ila baadaye wakaingia kwenye misuguona wakavunja uhusiano na sababu mwanamke anasema jamaa alikuwa na mwanamke mwingine....na mpaka sasa eti jamaa anaishi naye na amezaa naye mtoto...anyway mwanamke akamchukua yule mtoto aliyezaa na jamaa akampeleka kwa wazazi wake.

Mpaka nakutanane naye ameachana na jamaa na kwa takribani miaka mitatu...anyway baada ya kunieleza hayo kwa uchungu nikaanza naye mahusiano baadaye nikaona kwasababu ni mwanamke ambaye namfahamu kitabia tokea nikiwa chuo acha nifumbe macho nifanye haraku za kuweka ndani kwa heshima.

Anyway baada ya kuanza naye mahusiona akamata ujauzito nikaona ili nisimkweze na aone nipo sereous naye ngoja nikamtambulishe...nikampeleka home kwa utambulisho.

Nikawa nimebakiza kibarua ya kwenda kwao ambaye mpaka sasa sijaenda bado.

Sasa leo akanipigia simu akaniambia amepata msiba..nikamuuliza nani akasema baba mkwe wake wa zamani na waenda na dada yake..anyway sikutaka kumcrash.

Ila nimeona nipate muda wakutafsiri hiyo picture na kujiuliza maswali mengi.

Binafsi najiuliza kama ametoka misri na ameamua kwenda Caana kwanini anarudi nyum....
Na kama wameachana na hawakufunga ndoa na ameshatambul8sho katika familia nyingine anaenda kule kama nani...?na kwasababu gani hasa...?

Binafsi nikaona huyu anacheza na akili yangu kwasabsbu kama yupo sereous akesahau kule pa zamani na kusonga mbele na njia mpya...

Mimi nu mtu ni kazi yangu na biashara zangu..sasa naona kwasbabu hana kazi labda anaona apate mahali ambapo atapunguza makali fulani ya stress za mahusiono na maisha may be.

Binafsi naona niwe naye karibu amzee yule kiumbe then niangalie ustarabu mwingine ila asilani sintoweza kumoa tena...m
Unakaribishwa kwa ushauri
Acha wivu uliopitiliza. Ukipenda boga, penda na ua lake. Ukiwa na wivu, usi deal na single mom.
 
Back
Top Bottom