Huyu sheha(M/kiti) nataka kuja kumshitaki kwa Mkuu wa Wilaya hili limekaaje wakuu?

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,159
1,309
Tuna Sheha kwa upande wa Bara mnamwita Mwenyekiti anatuuzi sana wananchi kwa kulazimisha michango ambayo haistahili kwakweli. Zanzibar tuna masheha wengi lakini sijawahi kuona vituko anavovinya huyu wa mtaani kwangu.

Habari kamili....
Ni sheha ambae aliamua kupitisha michango kwa wananchi kwa kisingizio cha kwamba anatengeneza ulinzi shirikishi kitu ambacho wanamtaa wote hawakuafiki. Na kitu kilichofanya wasikubali kuchanga ni kwamba huyu sheha wanajua vyema anapenda pesa kuliko kuwahudumia watu wake.

Pia hawezi kukuhudumia huduma yoyote hata kama ni ya bure bila kukudai rushwa. Na pia ulinzi huo hauleti faida kwa maana hakuna hata mmoja anaepiga doria sana sana pesa zinatakiwa kuliwa tu.
Na ndomaana wananchi wa shehia yake walikataa kutoa michango hiyo.

Na kibaya zaidi tangia juzi anamtuma mtoto wake apitie michango baada ya kumjibu sina pesa nimejibiwa sitakuja kupewa huduma yoyote pindi nitakapokuja kuwa na shida ya ofisi yake na ndo maana nikasema nasubiri nije niende aninyime huduma nimpeleke kwa Mkuu wa Wilaya akajibie hili.

Mwisho.. Naomba kufahamishwa au kupewa mawazo nimefanya kosa kutochangia? Ilihali mwenyewe naweza kulinda nyumbani kwangu?
 
Toa mchango wako wa mawazo naona sijakuelewa
Njoo bara uone wanavyofanywa wanaokataa, ndio maana nikaishia kusema Zanzibariiii bwana daaah! Si kwamba sikuwa na cha kuchangia shekhe
 
Njoo bara uone wanavyofanywa wanaokataa, ndio maana nikaishia kusema Zanzibariiii bwana daaah! Si kwamba sikuwa na cha kuchangia shekhe
Nifahamishe basi na huku tupate njia ya kufanya maana huku undugu na ujamaa umekuwa mbele kuliko kazi.
 
Nifahamishe basi na huku tupate njia ya kufanya maana huku undugu na ujamaa umekuwa mbele kuliko kazi.
Wacha majungu!
Huko kwenu hakuna udugu na ujamaa why mwapenda kubagua manyago ya Watanganyika ni makubwa zaidi viongoz waserikali wanafanya watakavyo ktk kuwadhulumu wananchi mpk kuwaeka ndani kuwanyanganya mali mpk kuuwa ww umeambiwa utowe mchango kwa usalama wako mwenyewe unaende kulia JF hebu ndenda huko Tanganyika ukaone viongoz walivyogeuka kuwa WATAWALA
 
Masheha wengi wako hivyo, yaan hata ukihama sehemu moja kwenda nyingine inabidi upate barua kutoka kwa sheha ila ukienda anasema hakujui, sijui kiongozi gani anayewajua watu wake wote
 
Wengine hatujui huyo shehe sijui sheha ndio nani umesema tu mwenyekiti ni mwenyekit wa chama au mtaa hebu dadavua huku bara n cheo kipya kabisa hicho na mamalaka yake yakiutawala yapoje mkuu
 
Wengine hatujui huyo shehe sijui sheha ndio nani umesema tu mwenyekiti ni mwenyekit wa chama au mtaa hebu dadavua huku bara n cheo kipya kabisa hicho na mamalaka yake yakiutawala yapoje mkuu
Huku kwetu sheha anachaguliwa na mkuu wa mkoa, anaongoza shehia/kata yaani sijui hata nieleze vipi lakini ni kama mwenyekiti wa kijiji.
 
Wacha majungu!
Huko kwenu hakuna udugu na ujamaa why mwapenda kubagua manyago ya Watanganyika ni makubwa zaidi viongoz waserikali wanafanya watakavyo ktk kuwadhulumu wananchi mpk kuwaeka ndani kuwanyanganya mali mpk kuuwa ww umeambiwa utowe mchango kwa usalama wako mwenyewe unaende kulia JF hebu ndenda huko Tanganyika ukaone viongoz walivyogeuka kuwa WATAWALA
Sijui hata unaongea nini maana umechanganya madawa.
 
Back
Top Bottom