Huyu Rais wa Msumbiji ni Mmakonde mwenzetu au aliishi Bongo?

Mtagwa lindi

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
311
96
Wakuu, nimeona Rais wa Mozambique Filipe Nyussi anaongea Kiswahili fasaha kabisa je kuna anayefahamu vizuri historia ya huyu mwamba ni mwenzetu au alisoma hapa Bongo?

download.jpg
 
Ni mmakonde ambaye amesomea primary tanzania kabla ya kurudi msumbiji. Vilevile asilimia kubwa ya wamakonde waliopo msumbiji hata wale ambao hawajawahi fika tanzania wanajua kuongea na kusoma kiswahili. Wamakonde wanahesabika Kama ni wakimbizi wa kutoka tanzania
 
Wakuu, nimeona Rais wa Mozambique Filipe Nyussi anaongea Kiswahili fasaha kabisa je kuna anayefahamu vizuri historia ya huyu mwamba ni mwenzetu au alisoma hapa Bongo?

unaposikia TANZANIA NA MSUMBIJI NI NDG , hivi ndio viashiiria vyake. UHURU WA NCHI YA MSUMBIJI. ulipatikana kutokana na juhudi za chama cha FRELIMO kupiga kambi yake TANZANIA KAMA KITUO KIKUU CHA HARAKATI ZAKE , WALIKUWA NA KAMBI KUUBWA P[ALE MOROGORO ENEO LA Mazimbu, na kwa Dsm pale kilipo chuo cha Deplomesia ndipo ilipokuwa kambi yao. wamekaa muda mreefu saana tangu harakati hadi kupatikana uhuru , wameoa na kuolewa hapa. na hata baada ya kupata uhuru waliambiwa wanaotaka warudi, na kwao wasiotayari wabaki tu Tanzania. haya ndio majibu kwa mujibu wa ufahamu wangu juu ya swali lako.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom