Huyu Prof Tibaujuka naye vipi

ICHONDI

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
600
134
Ufisadi Ardhi wamtisha Waziri Anna Tibaijuka

• RIDHIWAN, SOFIA, MWANRI, DK. KIMEI WAFIKISHWA TAKUKURU

na Ratifa Baranyikwa

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameanza kazi kwa kuwataka watu ama vigogo waliochukua maeneo ya wazi na waliojipatia viwanja isivyo halali kujisalimisha mara moja kabla mkondo wa sheria haujachukua nafasi yake.
Tibaijuka alitoa agizo hilo jana wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo ambaye alikuwa ameongozana na Naibu wake, Goodluck ole Madeye, Katibu Mkuu, Patrick Rutabanzibwa, pia alisema kama kuna watu wamevunja sheria kwa kujipatia maeneo isivyo halali aidha kwa kushirikiana na maafisa wa wizara hiyo, hawatabaki salama.

Tibaijuka alisema wanaotumia jeuri ya fedha kwa kuvunja sheria nao hawatabaki na kuongeza kuwa kama sheria ina upungufu katika eneo linalosababisha migogoro itafanyiwa marekebisho.

“Kama kuna watu wamevunja sheria hawatabaki….nasema bora wajisalimishe, waliochukua maeneo ya wazi wayarudishe, kama kuna mtu kapewa kiwanja ajisalimishe,” alisema Prof. Tibaijuka.

Kadhalika waliojitwalia maeneo ya fukwe za bahari, aidha kwa kujenga nyumba zao au chochote kile, Tibaijuka alisema watu hao wako kwa muda tu kwa kuwa sheria haikubali kujenga katika maeneo hayo.

“Walioko kwenye Beach wako kwa muda tu zile ni Public Utilities, zipo kwa ajili ya watu kwenda kufurahi si kwa ajili ya kujimilikisha wao, wataalamu wetu wanajipanga tutafika huko,” alisema Tibaijuka.

Akizungumzia kero na migogoro ya ardhi, na watu kujenga kiholela, alisema watarudisha walinzi wa ardhi katika manispaa ambao walikuwepo katika siku za nyuma kwa kazi ya kulinda ardhi.

“Tutarudisha walinzi wa ardhi, ili kupunguza migogoro ya ardhi, hili limetugharimu sana,” alisema Tibaijuka.

Huyu kazi imeshamshinda!!! Hajakaa hata wiki moja ndani ya wizara, anaanza na matisho na mkwala usiokuwa na maana. Nadhani huyu ameshashindwa kabla hajaanza. Eti wajisalimishe, kina nani? Wajisalimishe kwa nani na kwa ajili ya nini. Kwa nini asingekuja na orodha ya hao vigogo na wenye fedha akaitoa hadharani mbele ya hao waandishi wa habari badala ya kuja na nothing zaidi ya upupu wa ccm wa kutisha halafu unaishia.

Huu utendaji wa kazi wa namna hii ni wa magazeti zaidi na umeshapitwa na wakati jamani, she just wanted press coverage. Prof umeanza vibaya, ungekaa kwanza, ukajua wizara ya ardhi manake yake nini, na kwa nini kuna ufisadi. Wizara ya ardhi sio viwanja, it is more than that, and I am so dissapointed. Nilivyosikia JK kamteua huyu mama nikajiuliza, ebo, what is he thinking, and I was darm right-- huyu hakuna kitu. I am sorry!!
 
Ichondi, acha kupayuka. Huyu mama amefanya vizuri sana kwa kutoa onyo kali kuanzia mwanzo kabisa. Waswahili husema' Kambare mkunje akiwa mbichi' Kwa kufanya hivyo mapema amejiwekea target ambayo ni wazi na inafikika. Hivyo kila mtu anafahamu target gani amejiwekea kwa hiyo hakutakuwa na ubabaishaji. Tena nakushangaa, yaani huyu mama mwenye ujuzi wote wa mambo ya ardhi unaona hajui ? Umeshasoma vitabu vyake?
Ushauri wako kuwa angetulia kwanza unaonesha wazi kuwa watu kama nyine mmezoea hawa mafisadi. Kwa sababu akikaa kimya tu atazongwa na mambo chungu nzima kiasi suala hili, ambalo kwa kweli ndiyo suala kubwa na nyeti, lingegubikwa na mambo mengine. Mi naona anatoa imani sana. Hasa kwa kugusia maeneo ya ufukweni ambayo hakuna aliyewahi kuyataja. Wajua katika sheria duniani at least kuwe na kilomita moja kutoka kwenye maji mtu asijenge? Na hii iwe kwa watu wote kuweza kujiburudisha? Huyu analeta matarajio.
 
Sasa hapo amekosea nini???
Kama umejenga sehemu ya wazi umekwisha. Acha kupayuka ovyo bwana. Tulaumu kwa sababu za msingi:angry:

Ichondi Kukaa siku moja sio hoja
matatizo ya Ardhi ya Tanzania kila mtu anayajua, hata wewe ukipewa leo hiyo nafasi hautapata shida kujua matatizo yako wapi
 
Strategies zinatofautiana tusianze kusifia au kulaumu sasa, tusubiri tuone.
 
Ichondi, acha kupayuka. Huyu mama amefanya vizuri sana kwa kutoa onyo kali kuanzia mwanzo kabisa. Waswahili husema' Kambare mkunje akiwa mbichi' Kwa kufanya hivyo mapema amejiwekea target ambayo ni wazi na inafikika. Hivyo kila mtu anafahamu target gani amejiwekea kwa hiyo hakutakuwa na ubabaishaji. Tena nakushangaa, yaani huyu mama mwenye ujuzi wote wa mambo ya ardhi unaona hajui ? Umeshasoma vitabu vyake?
Ushauri wako kuwa angetulia kwanza unaonesha wazi kuwa watu kama nyine mmezoea hawa mafisadi. Kwa sababu akikaa kimya tu atazongwa na mambo chungu nzima kiasi suala hili, ambalo kwa kweli ndiyo suala kubwa na nyeti, lingegubikwa na mambo mengine. Mi naona anatoa imani sana. Hasa kwa kugusia maeneo ya ufukweni ambayo hakuna aliyewahi kuyataja. Wajua katika sheria duniani at least kuwe na kilomita moja kutoka kwenye maji mtu asijenge? Na hii iwe kwa watu wote kuweza kujiburudisha? Huyu analeta matarajio.

Maonyo kama hayo hayasaidii chochote, kila mtu anyeingia hapo anaanza kutoa onyo mwisho wa siku hakuna anchofanya. Tumesikia na kushuhudia maonyo mengi sana, ila hakuna linalofanyika baada ya hapo. Kinachotakiwa fanya utafiti, then toa maamuzi. Si umeona Magufuli kamwambia Mrema live huku anamwangalia usoni!
Hii ni kutafuata cheap popularity mapema na asubuhi! TUNATAKA HATUA HATUTAKI MAONYO!
 
SUALA LA EKARI MIA MOJA, SINA SHIDA KAMA ALIPATA KIHALALI...

naamini kabisa kwamba alichosema ni kutekeleza maagizo ya mkuu wake wa kazi ili ajaribu kurudisha imani ya wananchi, unfortunately Mama Tiba asingeweza kuwa waziri leo kama yeye asingekua mmoja wao wa hao walaji

she was chosen because she fits into their frame
 
Nguvu ya soda tu, hii yote ni kwa kuwa yeye bado hajapata kiwanja ufukweni, atanyamaza tu.
 
This country bwana too many Makambaz, what I meant politicians, if she have guts to do it let her do it and stoping making empty threats
 
Kweli huyu mama anaanza kuchemsha na statement zake tata

Wazo lake ni zuri ila approach anayotumia ni kama ile ya EPA. Kwa hiyo tunaweza ku conlude wahusika. ni watanzania Class A.

Otherwise anasema hata wizara ya ardhi haina document ya kumbukumbu

  • yapi yalitaliwa kuwa maeneo wazi.
  • Wahusika( Mawaziri,Madiwani Mameya kamishna) walihuika kuvigawa.
 
Longolongo tu na nguvu za soda. Mtakuja kuniambia. Wanaoweza kufanya kweli hawachaguliwi na Kikwete, wanaochaguliwa hawawezi kufanya kweli.
 
It is not proper to judge her now let see what she is going to deliver out of her statements
 
Laiti angejua hayo maeneo yako wapi na yanamilikiwa na nani asingeongea hivyo. Tumesha m record na tunasubiria utekelezaji. Nachojua akipambana sana atahamishwa wizara nyingine kupinguza kelele.
 
Ufisadi Ardhi wamtisha Waziri Anna Tibaijuka

Huyu kazi imeshamshinda!!! Hajakaa hata wiki moja ndani ya wizara, anaanza na matisho na mkwala usiokuwa na maana. Nadhani huyu ameshashindwa kabla hajaanza. Eti wajisalimishe, kina nani? Wajisalimishe kwa nani na kwa ajili ya nini. Kwa nini asingekuja na orodha ya hao vigogo na wenye fedha akaitoa hadharani mbele ya hao waandishi wa habari badala ya kuja na nothing zaidi ya upupu wa ccm wa kutisha halafu unaishia.

Huu utendaji wa kazi wa namna hii ni wa magazeti zaidi na umeshapitwa na wakati jamani, she just wanted press coverage. Prof umeanza vibaya, ungekaa kwanza, ukajua wizara ya ardhi manake yake nini, na kwa nini kuna ufisadi. Wizara ya ardhi sio viwanja, it is more than that, and I am so dissapointed. Nilivyosikia JK kamteua huyu mama nikajiuliza, ebo, what is he thinking, and I was darm right-- huyu hakuna kitu. I am sorry!!

Tatizo lako na huyu mama hasa ni nini?
  • kuitisha press conference mapema?
  • Kutokukaa kwanza akaijua wizara kabla ya kufanya press conference?
  • utendaji wa magazeti?
  • kuongelea viwanja?
  • JK kumteua kuwa waziri wa ardhi?
  • Alichokuwa anafikiria JK wakati akimteua Prof. Tibaijuka kuwa waziri?
Kwa ufupi hoja unazojenga hazina mantiki.
 
Nilimwangalia Jana kwenye TV maongezi yake me sikuyaelewa kwa sana zaidi ya kusikia kila mara anasema au vip
 
Aaaaa watanzania bana! ni kama waonjaji wa mboga na chumvi! Chumvi ikizidi kelele, ikipungua kelele! sasa lipi litakuwa jema kwenu, muacheni mama na strategy zake subirini mje muhukumu baada ya kuona utekelezaji wa malengo yake
 
Binafsi sikufurahishwa toka mwanzo alivyoamua kugombea ubunge..
Angebaki kuwa mwanaharakati Kuliko mwanasiasa..
Namuonea huruma manake sifa alizozijenga kwa miaka mingi zitapotea ndani ya miaka hii mitano...
 
It is not proper to judge her now let see what she is going to deliver out of her statements
This is not about her, rather it is about the Kikwete administration's power structure, what can be done within it and what cannot.

Sasa wewe unataka kuniambia huyu Mama akikutana na kingmakers na big donors wa Kikwete huko atafanya nini ?
 
It is not proper to judge her now let see what she is going to deliver out of her statements

Mtu makini angetumia say, miezi miwili kuangaliz matatizo ya ardhi kama alivyosema; halafu atakapoibuka ankuja na strategies zake ni kuangamiza adui tu!!

Ukiangalia kwa makini anakuja na kama zile za JK 2005 wakati anahutubia bunge kwa mara ya kwanza!! Longolongo tu...
 
[
Huyo mama huwezi kushindana naye yeye anauzoefu katika eneo hilo kushinda unavyodhania kama huna hoja sio vibaya ukasoma za wengine. smahani lakini!!!!
 
Back
Top Bottom