Huyu Prof Tibaujuka naye vipi

namuombea atekeleze anayokusudia asiwe kama yule jamaa aliyesema walioiba pesa za epa wajisalimishe, kisha akasema wanaokula rushwa bandari wajisalimishe.
 
Mi naamini huyu mama angeenda University kufundisha angetoa mchango mkubwa zaidi, kuliko kuchukua political position aliyochukua sasa.
 
Ichondi, acha kupayuka. Huyu mama amefanya vizuri sana kwa kutoa onyo kali kuanzia mwanzo kabisa. Waswahili husema' Kambare mkunje akiwa mbichi' Kwa kufanya hivyo mapema amejiwekea target ambayo ni wazi na inafikika. Hivyo kila mtu anafahamu target gani amejiwekea kwa hiyo hakutakuwa na ubabaishaji. Tena nakushangaa, yaani huyu mama mwenye ujuzi wote wa mambo ya ardhi unaona hajui ? Umeshasoma vitabu vyake?
Ushauri wako kuwa angetulia kwanza unaonesha wazi kuwa watu kama nyine mmezoea hawa mafisadi. Kwa sababu akikaa kimya tu atazongwa na mambo chungu nzima kiasi suala hili, ambalo kwa kweli ndiyo suala kubwa na nyeti, lingegubikwa na mambo mengine. Mi naona anatoa imani sana. Hasa kwa kugusia maeneo ya ufukweni ambayo hakuna aliyewahi kuyataja. Wajua katika sheria duniani at least kuwe na kilomita moja kutoka kwenye maji mtu asijenge? Na hii iwe kwa watu wote kuweza kujiburudisha? Huyu analeta matarajio.

hana lolote bana ..ndo wale wale wengine wanapayuka eti walijazwa mimba wakiwa chuoni ..sasa kuna mawaziri hapo au utumbo
 
Mama inabidi apate maombezi na ikibidi apepewe! Hatutaki hadithi tunataka vitendo.
 
...Tatizo langu kubwa hapa ni yale maeneo ya wazi yanayomilikiwa na CCM, lakini hapo siku za nyuma yalikuwa yanamilikiwa na halmashauri za jiji, manispaa, miji, wilaya etc
 
Time will tell,its too early to conclude otherwise.

Mlisema hivi hivi alipochaguliwa Kikwete first time, alipoteuliwa Pinda kuwa PM etc etc.

Kitu gani kinakupa matumaini kwamba kitu chochote kitafanywa kwa mabadiliko ya msingi ?
 
tunahitaji maeneo ya wazi yaliyoporwa na ccm yarudishwe ktk miliki ya umma vinginevyo asimpige mkwara yeyote, kwani huo nao ni uporaji sasa ajiandae kuchukua hatua, vinginevyo akae kimya kama mawaziri wengine aache kujishaua
 
Ichondi, acha kupayuka. Huyu mama amefanya vizuri sana kwa kutoa onyo kali kuanzia mwanzo kabisa. Waswahili husema' Kambare mkunje akiwa mbichi' Kwa kufanya hivyo mapema amejiwekea target ambayo ni wazi na inafikika. Hivyo kila mtu anafahamu target gani amejiwekea kwa hiyo hakutakuwa na ubabaishaji. Tena nakushangaa, yaani huyu mama mwenye ujuzi wote wa mambo ya ardhi unaona hajui ? Umeshasoma vitabu vyake?
Ushauri wako kuwa angetulia kwanza unaonesha wazi kuwa watu kama nyine mmezoea hawa mafisadi. Kwa sababu akikaa kimya tu atazongwa na mambo chungu nzima kiasi suala hili, ambalo kwa kweli ndiyo suala kubwa na nyeti, lingegubikwa na mambo mengine. Mi naona anatoa imani sana. Hasa kwa kugusia maeneo ya ufukweni ambayo hakuna aliyewahi kuyataja. Wajua katika sheria duniani at least kuwe na kilomita moja kutoka kwenye maji mtu asijenge? Na hii iwe kwa watu wote kuweza kujiburudisha? Huyu analeta matarajio.

Kama sirikali wana uwezo wa kuwalipa waliojitwalia hizo sehemu sawa, la sivyo watashitakiwa. Wengi itakua walijipatia hizo sehemu kwa kuungahisha na Wizara hiyo hiyo lakini kwa rushwa. Kama hawakukatazwa kujenga kwa wakati huo, watadai fidia mpaka mahakamani. Hana haja ya kutishatisha maana hiyo mbinu tumeizoea toka kwa viongozi wa CCM. Jambo li wazi na atende kama anaweza maana wala hamna kambare mbichi wa kumkunja baada ya miaka nenda rudi ya ufisadi.
 
With Kikwete administration I expect no wonders labda kwenye Wizara moja tu kati ya zote, kila Waziri akiingia anapayuka tokea lini ukamwambia mtu aliyejipatia viwanja isivyo halali kujisalimisha mara moja kabla mkondo wa sheria haujachukua nafasi yake this is a joke to me why don't you take action unasubiri mtu ajisalimishe mwenyewe
 
QUOTE=Sijali;yaani huyu mama mwenye ujuzi wote wa mambo ya ardhi unaona hajui ? Umeshasoma vitabu vyake?

Correction: huyu mama ni mtaalamu na mjuzi wa mambo ya UCHUMI na si ARDHI. Husichanganywe na yeye kutokea UN-HABITAT. Yeye alikua UDSM kwenye Economic Research Bureau (ERB) ambayo sasa imekufa na kumezwa na idara ya uchumi. Na vitabu vyake ni vya uchumi. Husichanganywe tena na ripoti za UN-HABITAT ukadhani ni vitabu vyake.
 
Baada ya kusikia hiyo nilichoka kabisa
 
Mbona title haiendani na maelezo? Alilokosea ni nini? Au unamiliki viwanja vya wazi Nini?
 
Wana JF tusimshambulie mama wa watu bure!!!! Anatekeleza sera za sisiemu zilizodumu takriban miaka 50 na kutufikisha hapa tulipo!!!!!!!!!!
Orodha anayo lakini anaogopa kuwataja hadharani, maana akifanya hivyo hapo ndiyo itakuwa mwisho wa kelele zake kabla hata hajathibitishwa na JK kwenye nafasi hiyo!!!!!!Kumbuka huyu yuko probation-ndiyo katoka UN HABITAT-bado wanamstudy kama anaweza kuwa groomed kuwa fisadi au vinginevyo????????????????????????????
VITISHO NI STYLE YA SISIEMU!!!!!! Wewe omba Mungu ufike 2015 kama lo lote litakuwa limefanyika????????????????Kwani wewe na mimi tuna uwezo gani kuparamia open spaces na ufukoni????????????
Hebu ngoja tumuone!!!! ya nini kuandikia mate na wino upo????????????????????????
 
hayo maneno tu atakaa kimya hata jah-kaya mwenyewe alivyoingia madarakani alianza ivyo ivyo mara wala rushwa nawajua,wauza madawa nawajua sijui wajisalimishe, kipo wapi saiv?kama anataka kwel kipigana iyo vita aanza na huyo katibu mkuu wake,fisadi mkubwa wa ardhi huyo na umeme akiwa wizara ya nishati na sakata la iptl
 
Back
Top Bottom