Ufisadi Ardhi wamtisha Waziri Anna Tibaijuka
RIDHIWAN, SOFIA, MWANRI, DK. KIMEI WAFIKISHWA TAKUKURU
na Ratifa Baranyikwa
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameanza kazi kwa kuwataka watu ama vigogo waliochukua maeneo ya wazi na waliojipatia viwanja isivyo halali kujisalimisha mara moja kabla mkondo wa sheria haujachukua nafasi yake.
Tibaijuka alitoa agizo hilo jana wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ambaye alikuwa ameongozana na Naibu wake, Goodluck ole Madeye, Katibu Mkuu, Patrick Rutabanzibwa, pia alisema kama kuna watu wamevunja sheria kwa kujipatia maeneo isivyo halali aidha kwa kushirikiana na maafisa wa wizara hiyo, hawatabaki salama.
Tibaijuka alisema wanaotumia jeuri ya fedha kwa kuvunja sheria nao hawatabaki na kuongeza kuwa kama sheria ina upungufu katika eneo linalosababisha migogoro itafanyiwa marekebisho.
Kama kuna watu wamevunja sheria hawatabaki .nasema bora wajisalimishe, waliochukua maeneo ya wazi wayarudishe, kama kuna mtu kapewa kiwanja ajisalimishe, alisema Prof. Tibaijuka.
Kadhalika waliojitwalia maeneo ya fukwe za bahari, aidha kwa kujenga nyumba zao au chochote kile, Tibaijuka alisema watu hao wako kwa muda tu kwa kuwa sheria haikubali kujenga katika maeneo hayo.
Walioko kwenye Beach wako kwa muda tu zile ni Public Utilities, zipo kwa ajili ya watu kwenda kufurahi si kwa ajili ya kujimilikisha wao, wataalamu wetu wanajipanga tutafika huko, alisema Tibaijuka.
Akizungumzia kero na migogoro ya ardhi, na watu kujenga kiholela, alisema watarudisha walinzi wa ardhi katika manispaa ambao walikuwepo katika siku za nyuma kwa kazi ya kulinda ardhi.
Tutarudisha walinzi wa ardhi, ili kupunguza migogoro ya ardhi, hili limetugharimu sana, alisema Tibaijuka.
Huyu kazi imeshamshinda!!! Hajakaa hata wiki moja ndani ya wizara, anaanza na matisho na mkwala usiokuwa na maana. Nadhani huyu ameshashindwa kabla hajaanza. Eti wajisalimishe, kina nani? Wajisalimishe kwa nani na kwa ajili ya nini. Kwa nini asingekuja na orodha ya hao vigogo na wenye fedha akaitoa hadharani mbele ya hao waandishi wa habari badala ya kuja na nothing zaidi ya upupu wa ccm wa kutisha halafu unaishia.
Huu utendaji wa kazi wa namna hii ni wa magazeti zaidi na umeshapitwa na wakati jamani, she just wanted press coverage. Prof umeanza vibaya, ungekaa kwanza, ukajua wizara ya ardhi manake yake nini, na kwa nini kuna ufisadi. Wizara ya ardhi sio viwanja, it is more than that, and I am so dissapointed. Nilivyosikia JK kamteua huyu mama nikajiuliza, ebo, what is he thinking, and I was darm right-- huyu hakuna kitu. I am sorry!!