Huyu pia nimemshindwa,anapigiwa simu na wanaume sana

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Habari zenu wapendwa,

Mimi mwenzenu sijui nina balaa au gundu au mkosi yani hata sijui niseme nini kitu gani, maana kila mwanamke ninayempata ana visa vyake pia, huyo wa juzi nimemuacha kwasababu ya kuomba hela sana, hadi nikaanza mbele kimyakimya.

Nimempata huyu dada mwingine ambaye tulitongozana Facebook huyu sasa raha yake ni moja tu ni kwamba haombi hela wala nini, ila ukiwa nae inabidi ujiandae kisaikolojia, yaani demu anapokea simu kila wakati, mbaya zaidi anapokea simu za wanaune tu na muda mwingi yupo bize na kujibu msg za watsap na za kawaida.

Yaani hana raha ukiwa nae kinachonikera ni kwamba akipigiwa na hao wanaume wengi wao wanamuuliza "upo wapi" utakuta yupo kwangu ila anawambia nipo Ubungo,au nipo kwa ma mdogo Gongo la mboto ila narudi.

Sasa hii kwangu imenishinda kwa kweli,maana ananipa jaka moyo sana kwa kweli hadi karaha,wadada kwanini mpo hivyo siku hizi? Kuwa na wanaume wengi ni raha au sio?
 
Umeona ee...

Yaani huyo wala hajali kabisa, uko na mwanaume wako hapo halafu bze na cm?!

Siku hizi kuna wanaume wachache sana...wavulana ndiyo wengi! Mtu unakuta analalama hapa kivulana wakati hata yeye alimpata kwa namna hiyo hiyo asiyopenda wenzake wampate...ikiwa jamaa ni real gentleman basi amuweke ndani aone kama tabia hii ya ktafuta wasaidizi itaendelea!
 
Siku hizi kuna wanaume wachache sana...wavulana ndiyo wengi! Mtu unakuta analalama hapa kivulana wakati hata yeye alimpata kwa namna hiyo hiyo asiyopenda wenzake wampate...ikiwa jamaa ni real gentleman basi amuweke ndani aone kama tabia hii ya ktafuta wasaidizi itaendelea!
haya mapya sasa,,ntaoa wangapi
 
Subiri iko siku atasema nipo hapa kwa mama mdogo wangu..Ebu ongea na mtoto wake hapa nyumbani..Utapewa simu na sijui utasema kweli wewe mtoto wa mama mdogo wake ama la...Cheza na wanawake hawakawii kukuita hata house boy wao..Wewe unatambulishwa huyu anaitwa Manuu ni house boy wetu naenda nae supermarket akani bebee mizigo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom