Huyu ofisa wa udahili TCU, Fabian Mahundu anapotosha umma kwa maslahi ya nani?

Sasa hivi Rushwa ndio itatawala,TCU walikua hawapokei rushwa nina kuhakikishia 100%.
Sasa hivi vyuo ndio watapokea rushwa na nina mfano tayari wa mtu anaetafutiwa nafasi chuo fulani.
Mpaka Rais anajua walikua wanahongwa na wenye vyuo vya ajabu wapate wanafunzi
 
Mtoa mada ningekuona wa maana sana kama ungesisitiza vyuo vyetu viwe na online application ambayo gharama zake ni nafuu na haina usumbufu kama kujaza hayo ma-form ya application na kuyatuma kwa njia ya posta. Yaani mambo ya kizamani sana. Open University wanayo online application na wameondoa kabisa matatizo haya ya kutumia hard copy.
 
Kama alikosa nafasi MUHAS ni juu yake,labda alichelewa kuapply kwasababu jinsi unavyowai kuapply ndio jinsi chance ya kupata nafasi kwenye chuo husika inavyokua kubwa.
Mfano MUHAS wana idadi yao ya wanafunzi wanaowahitaji na kutokana na wanafunzi wengi kuhitaji kusoma hiko chuo wana wai kuapply.
Kuna dogo mwaka juzi alichelewa kuapply UDSM akakosa nafasi wakati alikua ana div 2,sasa hivi anasoma Chuo kikuu cha Iringa lakini malengo yake yalikua ni kusoma UDSM.
Kama mtu unataka chuo fulani na una vigezo wahi kuapply utapata bila shida ila ukichelewa lazima ukose.
Hicho unachokizungumza hakijawahi kuzungumzwa kama kigezo cha kupata nafasi chuo fulani kupitia CAS. There is always an explanation for ill deeds.
Unafikiri MUHAS wanapenda wachukue mtu wa div 2 eti kisa amewahi kuomba na kumuacha mtu mwenye 1.3 kwakuwa kachelewa???
Hakuna kitu kama hicho.
 
Hicho unachokizungumza hakijawahi kuzungumzwa kama kigezo cha kupata nafasi chuo fulani kupitia CAS. There is always an explanation for ill deeds.
Unafikiri MUHAS wanapenda wachukue mtu wa div 2 eti kisa amewahi kuomba na kumuacha mtu mwenye 1.3 kwakuwa kachelewa???
Hakuna kitu kama hicho.

Hakuna huo upendeleo unaotaka kutuaminisha,wanachukua wanafunzi wenye vigezo wanavyoviitaji.
 
nashukuru Mungu nilisoma enzi za vyuo vikuu vitatu tu (UDSM-MLIMANI, UCLAS, MUHIMBILI), MZUMBE na SUA....... Tena nikaapa nikimaliza BSc sitasoma tena Bongomovie....... na kweli a dream came true...
Offliner User please niweke sawa hapa ukimaliza Bsc hautasoma tena Bongomovie, naona kama kuna cha kujifunza hapa!
 
Mkuu,tatizo halikuwahi kuwa mfumo. Tatizo ni ufaulu wa mwanafunzi binafsi. Tuliofaulu vyema tulichagulika chuo kikuu chochote. Ufaulu mzuri ndiyo kila kitu.

Hili ndilo muhimu zaidi kwa mwanafunzi kuzingatia.

Ukifaulu vizuri huna hata haja ya kuapply vyuo viwili, chuo kimoja tu kingetosha. Tatizo ni huu ufaulu hafifu.
 
Jana nilimsikiliza ofisa mwingine wa TCU akiongea ITV, na leo yupo huyu anaitwa Fabian Mahundu. Ukiwasikiliza hawa maofisa maongezi yao yanaonesha kuwa, tunahama kwenye mfumo wa udahili uliokuwa bora, wenye ufanisi mkubwa na madhubuti, na tunahamia kwenye mfumo ambao ni crude, inefficient na utakaokuwa na changamoto nyingi.

Mimi ni mdau wa elimu, nafahamu wanachojaribu kukiaminisha kwa uma hawa jamaa ni upotoshwaji uliokithiri. Wametumwa hapo kutetea interests za vyuo vya kibabaishaji vilivyoanzishwa vichochoroni huku wakijineemesha kwa rushwa kubwa kuanzia uanzishwaji wake hadi kuwahakikishia rundo la wanafunzi.

Kwa jinsi wanavyoongea hawa jamaa, ipo dhahiri kuwa wapo tayari kuhujumu mfumo huu mpya, ili uonekane haufai na ikiwezekana turejee mfumo wa zamani. Naomba, nitoe wito kwa waziri Ndalichako, awabadilishe vitengo hawa jamaa, wasijihusishe kabisa na process za udahili.

Lakini pia, maongezi yao ni insurbodination kwa Rais ambae aliongea publicly kuwa huo mfumo ulikuwa misused.
Juzi nilileta uzi kupinga na kuonesha mapungufu ya mfumo ambao umepigiwa upatu na rais bila kufanya research....nina uhakika 90% tunarudi nyuma... Kwa mfumo huu mwanafunzi kukosa chuo ni rahisi sana.
 
Tatizo la Watanzania wengi hasa vijana wa sasa wakiona tu mtu anatofautiana na kauli ya rais wao kwa akili zao mgando hufikiri kuwa ametumwa.
Rais ni binadamu kama wewe, na hakuna binadamu mwenye efficiency ya 1, wote ni vichaa japo tunatofautiana aina na ukubwa wa kichaa.
Suala kama hilo la TCU siyo la kukimbilia kufungua thread, fanya utafiti wa kile unachokiamini na kile kilichongelewa na hao watu then njoo na maelezo toshelezi pasipo toa hukumu ili uone maoni ya wenzako maana kila mmoja ana mawazo yake
 
kwi kwi kwi...wanalilia application fees walizokuwa wanalipwa na watuma maombi Thru TCU...
Sijawasikia...ila kama wamepinga basi wamekosa nidhamu kupinga maamuzi halali ya Rais...
 
Siyo kweli,,
Nina mdogo wangu, alipata div 1 point tano alitaka kusoma udaktari,wakampeleka kairuki university. Ada pale ni zaidinya milioni sita ilhali bodi ya mikopo inatoa 3.6 m hivyo mpaka leo tunalazimika kuongezea kiasi kinachopungua. Kuna watoto wengi wa masikini wanaamua kuacha masomo kwa kushindwa ku top-up.

Halafu pia, moja ya motivation ya mwanafunzi kusoma vizuri kidato cha sita, ni ili apate points nzuri aweze kusoma chuo kizuri. Si sawa, mtu anapata div 1 point saba unampeleka sijui stefano moshi, sijui sekuko, sijui st joseph. Vyuo, hata waalimu hakuna, mwanafunzi anasoma degree anafundishwa na tutorial assistant. Vidarasa havina hadhi ya chuo kikuu, wanafunzi wanaishi mitaani huku mabinti wakiishia kuishi kinyumba na wanaume. Ktk kipindi hiki kilichopita, ndipo tu eshuhudia mabinti wengi sana wakimaliza vyuo na kurudi nyumbani na watoto.
Mkuu vyuo vya serikali vina uwezo wa kuwacompdate wanafunzi wote wanaopata div 1.. Idadi ya wanafunzi inaongezeka kila mwaka wakati vyuo hivi vya serikali haviongezewi uwezo wa kuongeza udahili..
 
Jamani TCU si ni regulator...?
Si waelekeze vyuo husika nini cha kufanya ili wawe na mfumo mzuri wa application?
Uliona wapi regulator akawa mtendaji...nani atamwajibisha mwenzie sasa????

Wao wajikite na kazi yao ya ukaguzi...na ushauri kwa vyuo vyote...

Walichokuwa wanafanya ni kituko...huwezi kufanya udaili wakati wewe ndie msimamizi wa ubora wa vyuo...
 
Back
Top Bottom