Huyu ni sumaye mpya au wa zamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ni sumaye mpya au wa zamani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bbukhu, Oct 5, 2012.

 1. b

  bbukhu Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HUYU NI SUMAYE MPYA AU WA ZAMANI?​
  Na Barnaba bukhu.

  Waziri mkuu mstaafu ndugu Fredrick Sumaye amejidhihirisha kuwa mtu mwenye msimamo usioeleweka katika nyanja ya siasa. Amekuwa akibadilikabadilika kama kinyonga.

  Hivi karibuni mwanzoni mwa mwezi Septemba akiwa katika maadhimisho ya miaka 20 ya chuo kikuu huria Cha Tanzania yaliyofanyika Dar es salaam, Sumaye alisema serikali ina wajibu wa kudhibiti mianya ya rushwa ambayo inawanufaisha watu wachache kwa maslahi binafsi. Alisisitiza pia kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo hivyo serikali inapaswa kuweka mkakati wa kuitokomeza na kwamba taifa lolote duniani lisipodhibiti rushwa haliwezi kupiga hatua ya maendeleo kutokana na watu wachache kutumia rasilimali za nchi kujinufaisha. Hiyo ni kweli kama ilivyo Tanzania sasa haipigi hatua yoyote ya maendeleo kwa sababu rasilimali za nchi pamoja na kodi za wananchi vinatumika kwa maslahi na manufaa ya wachache.
  Hiyo kauli ya Sumaye ni nzuri sana kama ingetolewa na kiongozi makini na mwenye uwezo wa kuitekeleza kwa vitendo. Lakini kauli hiyo inapotolewa na kiongozi ambaye alipokuwa madarakani hakufanya lolote au hakuchukua hatua yoyote katika kukabiliana na kuitokomeza rushwa, inatupa mshangao mkubwa sana mpaka tunajiuliza maswali mengi. Pia kauli kama hiyo inatufundisha kuwa viongozi wetu wana sura mbili katika jukwaa la siasa. Wakiwa madarakani, wanakuwa na sura ya udikteta, kulinda chama chao, kukumbatia mianya ya rushwa lakini wakiondoka madarakani wanavaa sura nyingine ya kupinga rushwa na kutaka kuonekana kuwa viongozi bora!
  Ndugu Sumaye tangu alipotoka madarakani ameendelea kuwa kada wa kukitetea na kulinda chama chake cha mapinduzi ccm na kuvichafua vyama vya upinzani kuwa havina uwezo wa kuongoza nchi na kuwa ni vichanga! Mwaka 2005 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na madiwani Sumaye alitumiwa kukipigia debe chama cha mapinduzi na kuwapigia debe wagombea wa nafasi za uongozi kupitia chama chake.
  Kwa mfano katika moja ya mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kata mpya ya Endasiwold mkoani manyara mwaka 2010, Sumaye aliwahi kuwaambia wananchi wa kata hiyo ya Endasiwold kuwa chadema haina umbo la kuongoza nchi, Dr. Slaa ameningÂ’inia kwenye mti usio na mizizi na kwamba hata akishinda urais hawezi kuwapata viongozi watakaomsaidia!
  Naam, huyu ndiye Fredrick Sumaye Mbunge wa zamani wa jimbo langu la HanangÂ’. Ni mbunge wangu ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu hivyo hakupata nafasi ya kuwa sauti ya wapigakura kwani mbunge akiwa waziri anaitetea serikali; anakuwa sauti ya serikali badala ya kuwa sauti ya wapiga kura wake. Ni kiongozi ambaye alikuwa katika nafasi kubwa kabisa serikalini na mwenye uwezo wa kudhibiti mianya ya rushwa ambayo anaizungumzia sasa. Alikuwa kwenye serikali ya ccm ambacho ndicho kilichoshika dola kwa sasa na ndicho chama ambacho kimelea rushwa na ufisadi kwa muda mrefu. Kimekuwa kikipalilia mianya ya rushwa na ufisadi kwa muda mrefu!
  Kwa hiyo, leo hii anaposema kuwa serikali ina wajibu wa kudhibiti mianya ya rushwa wakati serikali yetu ndiyo hiyohiyo ambayo ni ya chama kilichokuwa kikilea rushwa na ufisadi tangu yeye(Sumaye ) akiwa madarakani hadi leo sisi watanzania tunashindwa kumwelewa Sumaye. Wakati huo huo Sumaye ni kada wa ccm anayetegemewa kukipigia debe chama chake ambacho ni chama kinacholinda ufisadi ambao umewafanya watanzania walio wengi kuwa maskini na wale wachache kuwa matajiri. Je, kwa hali hiyo tumemwelewe vipi huyu mheshimiwa leo?
  Kwa hakika kauli ya Sumaye haina dhamira ya kweli katika harakati za kuikomboa nchi mikononi mwa hao wakoloni wachache walioko madarakani ambao wameshindwa kudhibiti mianya ya rushwa kwa sababu inagusa maslahi ya wakubwa. Ni wazi kuwa Sumaye ameshaanza kampeni ya kutaka kuchaguliwa tena kuwa kiongozi wa ngazi ya juu serikalini. Mtu wa namna hiyo hafai kuwa kiongozi wetu kwa kuwa alishawahi kuwa kiongozi tena wa ngazi ya juu serikalini na tunajua muda wa uongozi wake hakudhibiti rushwa na ufisadi. Wakati huo alikuwa kama vile hakujua kama rushwa ni adui wa haki na maendeleo na kwamba ni kikwazo kwa maendeleo ya nchi kwani inawanufaisha watu wachache kwa maslahi binafsi. Ndio tuseme wakati akiwa waziri mkuu, Sumaye hakuyaona mianya ya ruswa? Mbona rushwa haikuanza awamu ya nne ya urais? Kama Sumaye angekuwa na dhamira ya dhati kuwakomboa watanzania mikononi mwa utawala wa kinyonyaji, anapaswa kuondoka ndani ya ccm na kujiunga na chama cha upinzani au kubaki kuwa mtu asiye na chama. Kwa sababu haiwezekani Sumaye ajioneshe kuwa anachukia rushwa kwa kuwa ni adui wa haki na maendeleo wakati bado anakipigia debe chama kinacholea mianya ya ufisadi na rushwa. Haiwezekani! Lazima tuwe makini na mtu huyu asituhadae akidhani kuwa sisi tumesahau historia.
  Viongozi wote ndani ya ccm wamenaswa na matope ya rushwa na ufisadi kiasi kwamba hata wale ambao walikuwa na msimamo imara wa kupinga rushwa na ufisadi wameshalishwa limbwata la kisiasa. Sasa wanaficha maovu ya serikali. Wamebaki kuwa watetezi na walinzi wa chama chao. Wanatanguliza maslahi ya chama chao mbele badala ya maslahi ya taifa!
  Wako tayari kutumia polisi kudhibiti maandamano ya wanyonge wanaodai haki zao badala ya kudhibiti mafisadi wakubwa na walarushwa wanaotumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao. Wana hasira kali dhidi ya wanyonge wanaodai haki zao, ndio maana wanawaua raia wasio na hatia kwa kuwatumia polisi wanaotumia silahi zilizonunuliwa kwa kodi za wanyonge, sasa wamefungia gazeti la mwanahalisi kwa kuwa linaanika maovu ya watawala. Wanawafungulia kesi waandishi wa habari ambao wanaandika habari zinazogusa maslahi ya watawala na wanatishia kuvifuta vyama vya siasa vinavyotoa elimu ya uraia kwa watanzania na kuwatia hamasa ili waamke kudai haki zao. Hii ni hatari ilioje? Wanadhani wana uwezo wa kudhibiti na kutuliza hasira za watu waliochoka na unyonyaji na unyanyasaji?
  Wakati akiwa waziri mkuu, Sumaye na rais Mkapa waliweza kudhibiti bunge. Bunge iliwekwa mfukoni mwa wakubwa. Hawakuruhusu bunge kujadili masuala ya rushwa na ufisadi. Bunge likageuzwa kuwa sehemu ya serikali iliyokuwa ikificha masuala ya rushwa na ufisadi na kuipalilia mianya ya rushwa. Leo Sumaye ana maana gaini zaidi ya kupiga kampeni na kujisafisha kwa watanzania?
  Aidha Sumaye akiwa waziri mkuu katika serikali ya rais mkapa, serikali iliwahi kusema kupitia waziri moja kuwa bora wananchi wale nyasi ili ndege ya rais inunuliwe. Sumaye alikuwa sehemu ya serikali ambayo iliwakejeli na kuwasahau watu wake. Alikuwa kwenye serikali iliyodhibiti uhuru wa maoni ya watu kupinga maovu yaliyokuwa yanagusa maslahi ya wakubwa kama ilivyo sasa wakati huu wa awamu ya nne ya urais. Bora hata Mkapa ametulia zake maana hataki kujiaibisha. Ni bora na Sumaye akatulia badala ya kujifanya mtetezi wa wanyonge wakati si kweli.

  Hebu tumulize Sumaye maswali haya: Je, wewe ulipokuwa waziri mkuu kwa nini hukudhibiti mianya ya rushwa? Kwa nini serikali yenu wewe na Mkapa iliwadhibiti watu ili wasipinge rushwa na kutoa maoni yao yanayogusa maslahi ya watawala? Kwa nini ulidhibiti bunge ili lisijadili masuala ya rushwa na ufisadi? Na je, wewe ni Sumaye mpya au wa zamani?

  0784195782
  Baruapepe; bbukhu@gmail.com
   
 2. m

  malaka JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mh. Hii inaitwa boya au kinyago. Yaani wakati unakaribia walipo matrafki unamwacha mtu akuovertake then wewe unakwenda nyuma yake.

  Nina maana umetumwa kupima upepo wa wanaCDM humu kama tunaweza kuagree ujio wake au? Maana hana pa kwenda tena huyo!!!
   
 3. Peter jaluo

  Peter jaluo JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2014
  Joined: Nov 10, 2013
  Messages: 1,765
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mkuu cmwelewi sumaye cjui kakumbuka nini kutaka urais au alisau kuchukua chake mapema
   
Loading...