Huyu ni mtu wa kuogopwa kama ukoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ni mtu wa kuogopwa kama ukoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chamkoroma, Oct 19, 2010.

 1. C

  Chamkoroma Senior Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Mwalimu Nyerere na mbwa yule wa Manzese!

  Maggid Mjengwa
  Oktoba 13, 2010

  KESHO ni Siku ya Mwalimu. Huu ni wakati wa kuyakumbuka yale mema aliyoyafanya Mwalimu kwa nchi yetu. Mchango wake kwa taifa letu.

  Ama hakika, Mwalimu alikuwa na kipaji cha kuongea na bingwa hasa wa simulizi.

  Hotuba zake ziliwavuta wengi. Nakumbuka kuwa Mwalimu Nyerere alipata kusimulia kisa cha mbwa wa Manzese. Wakati huo nilikuwa bado kijana mdogo sana.

  Hiyo ilikuwa ni mwanzoni mwa miaka ya 80. Ni kwenye kilele cha sherehe za Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi. Sherehe zile zilifanyika pale Uwanja wa Taifa. Nilibahatika kuwapo uwanjani.

  Baadhi ya mabango ya wafanyakazi yaliyopita mbele ya Mwalimu siku ile yaliwakilisha ujumbe juu ya hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi; mishahara midogo na mengineyo.

  Wakati huo, Serikali ya Mwalimu ilikataa masharti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia pia. Hii ni kwa sababu, licha ya athari nyingine mbaya kwa masharti hayo kwa nchi yetu, uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu nao ulikuwa hatarini.

  Ilipofika wakati wa kutoa hotuba yake, Mwalimu Nyerere alisema; "Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

  Kwenye moja ya nyumba za huko Oysterbay akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini; huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay.

  Mbwa yule wa Oysterbay alinenepeana huku manyoya yake yakiwa yameteremka hadi machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese. Mbwa yule wa Manzese alionekana kukondeana huku masikio yake yakiwa yameteremka hadi shingoni.

  Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese; " Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!

  "Naam, miye ni mbwa kama wewe." Alijibu mbwa wa Manzese. "Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi."Mbwa wa Manzese akajibu; "Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!"

  Sitakisahau kamwe kisa kile alichosimulia Mwalimu Nyerere pale Uwanja wa Taifa. Naamini katika alichokisema Mwalimu. Nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani.

  Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Ingawa ni neno fupi sana, lakini neno uhuru lina maana kubwa. Asiye na uhuru ni mtumwa.

  Binafsi najiona ni mtu huru. Na siku zote nimepigania nibaki kuwa mtu huru. Kwa uhuru kabisa nakutana na kuongea na watu wengi; vijijini na mijini. Nakutana na kuongea na wasomi na wasio wasomi, matajiri na masikini. Nakutana na kuongea na watu wenye imani na itikadi tofauti.

  Na wala sioni aibu kuweka bayana kuwa naamini katika itikadi ya kijamaa. Maana, Ujamaa umejengwa katika misingi ya haki na usawa. Naamini, kuwa Ujamaa na Kujitegemea kama itikadi, bado ndio itikadi inayofaa kuongoza siasa ya nchi yetu. Bila shaka, Ujamaa na Kujitegemea unahitaji kufanyiwa marekebisho ya kimsingi ili uendane na wakati.

  Simulizi ya Mwalimu juu ya ‘Mbwa wa Manzese' imejengeka katika misingi ya Ujamaa na Kujitegemea. Taifa linalojitegemea linabaki siku zote kuwa taifa huru. Vivyo hivyo , kwa mwanadamu. Binadamu anayejitegemea ni binadamu huru.

  Nchi yetu inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu. Kinachoonekana dhahiri ni kukosekana kwa misingi ya kiitikadi katika kuendesha kampeni za kisiasa.

  Vyama vimejikita katika kutoa ahadi. Lakini, katika siasa, lililo kubwa ni itikadi. Kama chama kinafuata itikadi ya kibepari, basi, kuahidi kutoa elimu na afya bure kunakinzana na misingi ya itikadi husika. Katika ubepari hakuna cha bure.

  Ndio maana, Barack Obama alisemwa na wenzake wa chama cha Republican kuwa anataka kuwapeleka Wamarekani kwenye Ujamaa pale Obama alipopigania kupitishwa muswaada wa Huduma za Afya za bure kwa jamii.

  Hapa ina maana, kuna Wamarekani watakaolipa ili wenzao wanyonge wanufaike. Kwenye mfumo wa Kibepari, kuna wanaoliangalia hili kwa macho ya mashaka.

  Katika itikadi ya kijamaa, huduma za kijamii kama vile elimu na afya ni kawaida kutolewa bure au kwa gharama nafuu sana. Fedha za kugharamia huduma hizo hutokana na kodi inayokusanywa kutokana na shughuli za uzalishaji. Wajamaa wanaamini katika kuwatoza kodi zaidi wenye nacho ili kuwamegea wasio nacho.

  Hapa kwetu vyama na wagombea wameshindwa kujipambanua katika itikadi. Mgombea anayetokea kwenye chama chenye sera za kibepari anasikika kama anatoka kwenye chama cha kijamaa na kinyume chake.
  Wakati mwingine unaingiwa mashaka, kama kweli vyama vina itikadi zenye kueleweka. Inatokea pia, kuwa itikadi ya mgombea, mara nyingi haionekani wazi anapoongea.

  Huko nyuma niliainisha kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Si kazi ya mtu mmoja. Kelelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.

  Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma.

  Katika kampeni tunazokwenda nazo tunaona, kuwa baadhi ya vyama havina kabisa hazina ya makada. Kazi ya kuwahamasisha wapiga kura inapaswa kufanywa kwa kuanzia ngazi za chini kabisa, na huko chama kinahitaji makada wa kuifanya kazi hiyo. Hata kama uchaguzi huu utapita, vyama vijizatiti kuifanya kazi hiyo ili kujiandaa kwa chaguzi zijazo.

  Na hatari ya kukosekana itikadi za vyama zenye kueleweka, ni uwezekano wa kama tunavyoona sasa. Hali ya kujipenyeza kwa nguvu hasi zenye kutaka kuisukuma jamii kuelekea kwenye machafuko. Hawa ni wale wenye kutaka kuiingiza nchi yetu kwenye siasa za kidini na kikabila.

  Hawa ni watu hatari na wa kukemewa kwa nguvu zote. Baadhi yao wamediriki kutumia hata nyumba za ibada kuwaandaa Watanzania kufanya kile chenye maslahi yao binafsi na kuhatarisha maslahi ya taifa.

  Tujiadhari katika kufanya yale yatakayopelekea kuboboa misingi ya Umoja wetu wa kitaifa.

  Ni bahati mbaya sana siku hizi; unaposema au kuandika jambo kama nifanyavyo sasa, haraka kuna wanaokimbilia kutafuta kabati la kukupachika; CCM, CUF, CHADEMA, dini, kabila na mengineyo.

  Tumelisahau kabati muhimu sana, nalo ni kabati la Tanzania. Na hakika, katika kila tuyafanyayo, tutangulize kwanza maslahi ya nchi yetu.
   
 2. S

  So Perfect Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni bahati mbaya sana siku hizi; unaposema au kuandika jambo kama nifanyavyo sasa, haraka kuna wanaokimbilia kutafuta kabati la kukupachika; CCM, CUF, CHADEMA, dini, kabila na mengineyo. ni kweli kabisa hasa usipoweka ushabiki wako kwa CHADEMA utaonekana wewe CCM na Muislam, ni ujinga usio na msingi
   
 3. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  good observetion.
  Kunahitajika elimu ya kina mtu kuweza kujitambua na kujipambanua kwamba yeye ni nani na anawakalisha nini.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Hongera Maggid kwa hii makala yako lakini ningependa kufanya masahihisho mawili tu. Dhana ya kiitikadi Tanzania haipo kwa sababu katiba yetu tayari imekwisha kutulazimisha itikadi yetu ni ya ujamaa na kujitegemea.................Vyama vyetu vya siasa vimewekewa mipaka hiyo ya kisheria kwa hiyo wanachotofautiana ni sera za kuitekeleza azma hiyo ya kisheria. Kwa hiyo kauli yako hii hapa chini siyo sahihi:-

  La pili ni kuhusu mgawanyiko wa utaifa wetu haukuanzia kwenye chaguzi la hasha. Unaloliona kwenye chaguzi ni mwendelezo tu wa siasa za kibaguzi ambazo CCM imekuwa ikiziendeleza miaka nenda rudi.

  Ubaguzi huu umejitokeza katika ajira serikalini na utoaji wa zabuni za serikali kufuata misingi ya udini na ukabila.


  Jamii inawaangalia viongozi waliopo madarakani kama wapo wote wakiona wanawabagua basi laana hiyo hiyo hujionyesha katika chaguzi zetu kwa sababu viongozi ndiyo wanaoongoza katika dhuluma yenye misingi ya kibaguzi.

  Hivyo kosa ambalo wewe unalifanya ni kukwepa kuwalaumu CCM kwa kutufikisha hapa tulipo na umenaswa kwenye mtego wao wa kulaumu upinzani kwa makosa yao.

  Kauli yako hii hapa chini inaficha ukweli na inalenga kulaumu wasio paswa kulaumiwa.

   
 5. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ndo mjengo bana
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hatujua anafanya kazi gani kwenye CCM lakini inaonekana Mambo yakiwa mabaya atakimbilia Nordic Countries...
   
 7. M

  Mboko JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ofcoarse huyu jamaa Mjengo sijui anajiita nani sitaki kufahamu zaidi ni kwamba huwezi kumuelewa yu wapi maake kakaa kama CCM vile au Cafu any way atajiju na kweli kama jamaa alivyosema kikilipuka atakuwa hapa Sweden sijui ni Malmo au Gotenborg au wapi he know himself:A S thumbs_down:
   
Loading...