Uchaguzi 2020 Huyu ni msafisha viatu kweli au ana kazi nyingine maalum? Amenichambulia siasa za Tanzania na kuahidi Tundu Lissu kushindwa vibaya

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,937
20,377
Moja kwa moja kwenye mada maana naona Tundu Lissu anajimwambafwai na hata sasa anaanza kuwachokoza watu wa kawaida kabisa hadi wasafisha viatu wa mjini Dar-es-Salaam.

Niliamua kujivinjari maeneo ya mjini Dar na nikapata nafasi ya kusafisha viatu vyangu kwa kuweka Kiwi.

Kwa kawaida mimi ni mchokoza mada sana na nilianza na suala la siasa za sasa zinezoendelea na ujio wa Tundu Lissu.

Msafisha viatu akajibu harakaharaka kwamba hiyo ni ni geresha tu Tundu Lissu hawezi kumshinda ngosha au Uncle Magu.

Jamaa akaendela "ngoja nikwambie kitu kimoja, System ndio wamemruhusu kurudi hapa nchini". Akaendelea, ila wamemuachia tu ajimwambafwai kabla ya CCM mashine haijashuka ianze kazi".

MImi nikakaa uzuri na kuagiza maji ya muwa na barafu kwa kipande cha ndimu na nikaendelea kumsikiliza msafisha viatu akishusha madini.

CCM si mashine ya unga wala karakana ndogo wala kubwa, bali CCM ni kiwanda kilichotapakaa nchi nzima.

Hata mjumbe wa nyumba 10 wa CCM au mwenyekiti wa serikali ya mtaa wote ni sehemu ya kiwanda hiki cha CCM.

Sasa CCM walianza na Augustino Mrema mwaka 1995 wakampa kazi ya kuwa mgombea wa upinzani na aliifanya kazi hiyo kwa moyo wote wa kujituma.

Mrema alikuwa ni mmoja wa walimu wazuri tu pale Kivukoni na hata kule Mbweni, hadi leo hii, Mrema atakuwa anajivunia kuwa ameacha kundi kubwa na wanafunzi wake wakiwa kazini.

Mwaka 2000 Mkapa hakuwa na kazi kubwa kama ya 1995 akapita maana upinzani tayari ulikwishaanza kulegezwa.

Hata alipokuja Kikwete mwaka 2005 kazi pia haikuwa kubwa na mtoto wa mjini akapita na msemo wake wa Hali Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya ulivuruga kabisa maipango ya upinzani na Mbowe akapigwa chini na wapiga kura wa kitanzania.

CCM imetawala nchi hii tangu uhuru na ndio chama dola ambacho kimeshika jeshi, vyombo vyote vya usalama na polisi, sasa iweje kisiwe na nguvu?

Kitengo ni moja ya nguzo za nyuma ya CCM na pamoja na kumpitisha raisi wa sasa John Magufuli (ambae anatarajiwa kupita tena uchaguzi wa mwaka huu) lakini alikuwa ni wa tatu kwenye tatu bora baada ya Amina Salum Ali na Asha Migiro.

Lakini kwa kuwa Amina alifanya mazunguzo na Edo kwamba yeye (Amina) akipitishwa basi Edo awe mgombea mwenza, Kitengo kikasema hio haiwezekani na kura zote za Amina zikaenda kwa Magufuli.

Hii nchi ni lazima iendeshwe kwa misingi ya usawa na kila mwananchi wa nchi hii ni lazima afaidi matunda ya uhuru.

Kulijitokeza makundi ambapo kundi moja lilijiona kuwa lenyewe tu ndilo lenye haki ya kupata kila rasilimali za nchi hii na kuzitapanya huku na huko.

Wananchi wa kawaida kabisa wakasahauliwa na kuishi maisha ya kishenzi sana.

Sasa John akapewa maono yaani Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na aitekeleze kwa kasi na umakini mkubwa.

Na hata alipoingia madarakani John Magufuli aliwaambia viongozi wote kwamba "jamani eeh kila mwenye mali ajitokeze aziorodheshe kabisa maana mimi nikianza kazi sitakuwa na simile"

Wengi walisikia yalomtokea mama Salma na wengine ambao biashara zao zilikuwa zinatumika kuficha jina halisi.

Ndo maana mzee wa kutabasamu yupo yupo tu maana huwa akumbuka ya Chamwino kwamba aliambiwa na Kitengo kwamba , "jina hapo ni JPM ndo final"

Watu wanalaumu tu jina limetokea mfukoni lakini hawafahamu chanzo halisi ingawa nimekieleza hapo juu.

Sasa Tundu Lissu ameanza kuropoka na kuwataja hadharani wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Anasema ana taarifa za vitisho na kwamba IGP Sirro na DG wa TISS lazima wawafuatilie watu wao, Yaani anamaanisha kwamba ana uhakika vitisho hivyo vinatoka kwa watu wa vyombo vya Usalama?

Huku si ni kujitafutia sababu ili kutengeneza sinema ya bure?

Vyombo vingi vya habari vya nje ambayo Tundu Lissu alijitahidi kuviaminisha na hata Steven Sakari wa BBC kumuuliza kwamba ana ushahidi wa tuhuma anazozitoa, navyo vimepigwa na butwaa na ukimya wa serikali ya Tanzania.

Vyombo hivyo pamoja na nchi za kibeberu na mashirika na makampuni ambayo yalifukuzwa nchini kwa kosa la kukwepa kulipa kodi na kuiba rasilimali za watanzania vilitarajia kuona Tundu Lissu anakamatwa pindi atakapofika Tanzania.

Ukimya huu umewashangaza hata wapinzani wenyewe ambao wengi walitegemea wafanye vurugu na sasa wamechiwa wafanye kampeni wakizunguka kwa kudai wanatafuta wadhamini wa Tundu Lissu.

Upinzani kwa sasa utapoteza kura nyingi sana kutokana na kwamba ACT ambayo nayo ilianzishwa kwa makubaliano kati ya Membe na Zitto ili kugawa kura za wakti ule.

Ndo maana Zitto hadi leo hajaweza kujibu sawasawa zile tuhuma za Chadema.

Sasa huko kuna Membe, kuna Nyalandu na wengine yaani Upinzani unaangaliwa tu sasa hivi.

Hebu fikiria, mtu ambae alikuwa waziri mkuu, au waziri wa wizara fulani leo hii aachie kiti hicho cha CCM na aende Upinzani?

Hivi Upinzani umewahi kukaa chini na kutafakari kuhusu ujio wa Lowasa au ujio wa Sumaye ambao ni mawaziri wakuu wa zamani wa nchi hii?

Yupo Maalim Seifu ambae aliitwa mjengoni kupewa mawili matatu kwamba Zanzibar ni kama kawaida na hakutakuwa na shida na watu wote muhimu kwa sasa wapo huko tangu January 2020.

Halafu kuhusu Makonda, wanadhani wamemkomoa kumbe wamejikomoa wenyewe.

Wajumbe wengi wa walopiga kura kwa Ndugulile wameishafanyiwa mahojiano na Kitengo na yalotoka hapo ni majibu yanayoshangaza sana kwamba nchi hii pamoja na uwepo wa serikali hii ya awamu ya tano bado kuna watu wana mioyo ya kuweza kuhonga kwenye uchaguzi wa kura za maoni ili tu Makonda asipite?

Wapo wafanya biashara, wauza unga na watu wengine ambao kwa kweli Makonda hakuwapa nafasi ya kupumua upepo mwanana wa bahari ya Hindi.

Msafisha viatu huyu akaanza kunishushia mafanikio ya JPM na matarajio yake pindi atakapotangazwa raisi wa Awamu ya tano ifikapo mwezi October 2020.

Pia akamtaja Paul Makonda kwamba anayo nafasi kabisa ya kuwa waziri katika serikali hiyo na huenda akapewa nafasi nyeti sana katika baraza la mawaziri.

Akamalizia kwa kusema raisi wa awamu ya tano Dr JPM atawashangaza sana watanzania kwa aina ya serikali atakayoiunda ya 2020-2025.

Kuja kuangalia muda nikajikuta nimekaa pale masaa mawili na nikamuomba msafisha viatu nimuache ili niwahi boat ya kurudi Zanzibar niwahi ugeni wa ACT Kisiwani humo.

Maana Membe na mshirika wake Zitto Kabwe kwa kiingereza twasema smooth operators na Maalim Seif wapo safarini visiwani.

Unaweza kufikiri watanzania wa maisha ya kawaida kabisa hawaelewi kinachoendelea lakini kumbe watanzani walo wengi wana uelewa kabisa wa siasa za Tanzania na wanazifahamu kwa kiwango kilichopitiliza.

NB: Habari imekatikakatika lakini wenye uelewa hawatopata shida
 
Richard,

Hahahaaaa! We jamaaa hata hujielewi kabsa. Kwa hiyo Lowassa na Sumaye walienda kuzuga tu Chadema? Unashangaa Nini waziri mkuu mstaafu kutafuta uongozi kupitia chama kingine? Fatilia siasa za kiafrika ndo utajua, hiyo system unayojimwambafai kuijua sindo ilikuwa chini ya mchungaji Kipilimba, unajua kilichomtoa hapo kupelekwa ubalozini? Unajua kilichomtoa hapo naibu Mkurugenzi wa TISS ndugu Makungu kuwa Ras Tabora? Eti BASHITE unamjadili humu kuwa kaangushwa na wauza unga! Khaaaaa.
 
Unaposema CCM bado haijaanza kazi kwani Chama gani kimeanza kazi? Kumbuka huyo ni Lissu anajipitia zake tu kutafuta wadhamini, na hapo tena mnachokiona na kusikia ni bahat mbaya tu sababu vyombo vya habari vimedhibitiwa kuonyesha mambo ya wapinzani.

Unaposema CCM bado haijashusha mashine zake kuanza kazi inaonekana hujui ukiongeacho sababu CCM ndiyo pekee ambao wamekuwa wakiruhusiwa kuafanya kazi muda wote katika awamu hii.
 
Nilipoanza kusoma hiki ulichokiita ‘madini ya msafisha viatu’ aya ya kwanza tu nimegundua mrengo wake wa kisiasa japo haikunifanya niache kusoma maana nilitegemea kukutana na madini I mean hoja nzitonzito za kufikirisha ila nasikitika nimepoteza muda wangu bure.

Msafisha viatu wako hana hoja yoyote zaidi ya mahaba ambayo hayatofautiani sana na ya mpishi wetu asiyejua ulimwengu wa kileo zaidi ya siasa za kizamani za akina Mrema.

Tukiyaacha hayo, Hivi watu huwa mnapata wapi ujasiri wa kujadili siasa hadharani? Mimi hata dereva wa bodaboda akichokoza mada huwa nakaa kimya kama sielewi chochote, kazini ndio kabisa japo wanafahamu sivutiwi na uongozi huu wa CCM.

Nyumbani kwangu ndiko hasa moto wa siasa huwaka, utadhani ni Congress ya Marekani jinsi tunavyopanga na kuchambua hoja, lol
 
Back
Top Bottom