Hivi watu huwa mnapata wapi ujasiri wa kujadili siasa hadharani? Mimi hata dereva wa bodaboda akichokoza mada huwa nakaa kimya kama sielewi chochote, kazini ndio kabisa
Hicho kiwanda 2015 kilikosa nishati au vipuri nini? Mbona tuligalagazwa mbaya? Kutojiamini kote kwa Magu ,uamuzi wa kurudisha bunge letu gizani na Magufuli kuamua kupiga kampeni kwa miaka mitano yalikuwa ni matokeo ya kugaragazwa,Kama haya yamesemwa na huyu mshona viatu no wonder ni mshona viatu,he is an empty head
Uliposema msafisha viatu kashusha nondo nikajua ni yule wa pale nje ya Wizara ya Ardhi maana naye ni walawale. Lakini sasa pale hakuna juice ya miwa wala barafu, na hata hizo unazoziita nondo nazo, dah!!!🙆♂️
Richard,
Hahahaaaa! We jamaaa hata hujielewi kabsa. Kwa hiyo Lowassa na Sumaye walienda kuzuga tu Chadema? Unashangaa Nini waziri mkuu mstaafu kutafuta uongozi kupitia chama kingine? Fatilia siasa za kiafrika ndo utajua,hiyo system unayojimwambafai kuijua sindo ilikuwa chini ya mchungaji Kipilimba, unajua kilichomtoa hapo kupelekwa ubalozini? Unajua kilichomtoa hapo naibu Mkurugenzi wa TISS ndugu Makungu kuwa Ras Tabora? Eti BASHITE unamjadili humu kuwa kaangushwa na wauza unga! Khaaaaa.
Richard,
Kama hufahamu tuu awamu zinakuwaje na zinabadilikaje, "saizi" yako ya uelewa ni hiyo hiyo ya vijiwe vya washona viatu.
UPUUZI MTUPU! Unamshindaje Lissu katika uchaguzi ambao hausimamiwi na TUME HURU, Serikali inahofia UWAZI na kuhakikisha kura zinahesabiwa hadharani?
Tia akili kichwani ili utafakari kwa kina kabla ya KUKURUPUKA.
Mkuu bado naamini kuwa upinzani ulikuwepo huko nyuma na si sasa.
Hakuna upinzani Tanzania.
Ask Mr Mbowe and co wanafahamu hiyo 100%
Wao waangalia kiasi gani chaingia benki na maisha yanaendelea.
Nimesema sana humu kwamba tulipokuwa "more active" kwenye harakati tulikuwa na matumaini, lakini kitendo alichofanya Mbowe cha kupokea fedha za Lowasa na kubadili gia angani na kumtosa Dr Slaa, mimi ndo nasimamia hapo na sitabadilisha uamuzi huo.
Ndo maana nimeona ni bora kuwa na serikali hii ambayo itatekeleza yaleyale tuloyokuwa tunayapigia kelele hapa tena tukitaja tunahitaji raisi dikteta.
Raisi JPM si dikteta ila baadhi yetu sisi khasa wa humu mitandaoni ndo tunamlazimisha kuwa dikteta.
Ila mpaka sasa bado raisi JPM hajawa dikteta ila tunamlzimisha awe dikteta halafu tupate sababu.
Sasa JPM hataki fujo si umeona hata raisi wa nchi jirani kaambiwa aongee na Johari kuhusu kuzuiwa ndege zao?
Sasa mnadai tume huru, sasa tume mbona mnakubali NEC ikitangaza matokeo ya vyama vya upinzani kwa majimbo wanayoshikilia?
Naomba nitajie tume huru yoyote ile katika nchi yoyote ile ambayo ipo na yafanya kazi zake "independently".
Hebu achana na alinacha zako Mkuu! Ni lini ulifanya utafiti? Na utafiti wako uliokuaminisha kwamba Tanzania hakuna upinzani uliufanya lini na katika mikoa ipi? Na ukubwa wa sample yako ulikuwa upi!? 😳😳
NIlianza kufuatilia Upinzani tangu ianzishwe NCCR-Mageuzi ya mazee akina Augustino Mrema, Marehemu Masumbuko Lamwai na Mabere Marando.
Hivyoi tangu upinzani uanze mwaka 1992 nimekuwa naufuatilia.
Kibaya zaidi nilipoona marehemu Oscar Kambona anaruhusiwa na Nyerere kurudi Bongo halafu nae acheze kidogo na mtindo wetu wa siasa za kitanzania.
Pia nilikuweo Mwembeyanga pale Dr Slaa alipotaja ile orodha ya mafisadi.
Nimeona mengi nimezunguka nchi nzima.
Nakubali zipo sehemu katika mikoa yetu Upinzani unakubalika Arusha, Mbeya, Mara, Kilimanjaro na sehemu zingine lakini ni rahisi sana kwa sasa upinzani kupoteza sehemu hizo kuliko ilivyokuwa kabla ya 2015.
Kakopa trilioni 40.5Kimchezomchezo JPM anamaliza awamu ya kwanza bila kuwasujudia mabeberu
Hichi kweli chuma #HAPANGIWI
Hizo ndio nondo? Mawazo ya zamani sana hayo!