Huyu ni mdudu Tandu? ana madhara gani?

Mkuu huyo ni tandu, anasumu kali sana ila wakiwa wadogo kiumbo wanatabia ya kuingia sikioni ukiwa umelala na kung'ata . (Hasa kwa watoto/w.wazima)

Unaweza changanyikiwa!

Btw kama wapo wengi chukua tahadhali maana sumu yake ni konk mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ana maumivu makali mnooo, ila sumu yake haijafika level ya kuleta madhara makubwa mno kwa mwanadamu.
 
Nkushauri fuga paka hapo nyumbani kwako. Paka ni kiumbe ambaye watu wanamchukulia poa sana ila anauwezo wa kupambana na kuua wadudu hatari kwa binadamu kuliko unavyofikiria, paka anauwezo wa kupambana na huyo centipede, anauwezo wa kupambana na nyoka, mijusi, nge, panya, na chochote kile ambacho ni strange na hatari kwa binadamu ambacho kipo ndani ya uwezo wake basi atahakikisha nyumba yako inakua safe 99%. Vuta picha upo mbali na maeneo ya home alafu centipede wakazaliana humo ndani kwa siri unadhani patalalika kweli? Asante Mungu kwa kutuumbia paka.

what-does-it-mean-when-cat-wags-tail.jpg
Aiiseee leo nimesikitika sana. Jana nimemsahau nyau wangu nje jamaa wamekuja kumuua asubuhi wameanza kumuona majirani amekufa daaaah kila mtu anemjua yule paka amesikitika sana.
Jamii itambue kwamba tunatofautiana sana, wengine tunapenda wanyama kama sehemu ya maisha yetu(pets) lakini wengine wakiona hivyo wanaanza kujenga hisia za kichawi eti oooooh paka gani hilo kama mtu, linaelewa kila kitu, halizururi hovyo, halidokoi na hata ukilipa chakula halisogei hadi mwenyewe alipe tena limetengewa sahani kama binadamu,sio bure yule anaroga kwa kutumia paka, aiseee nimeniuma sana.
R.I.P Mashal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila baada ya wiki kadhaa, nimekuwa nakumbana na mdudu huyu ndani ya nyumba. Uzuri mara zote nimekuwa namuwahi kumuua kabla hajanigusa.

Kuna mtu alikuwepo nymbani siku moja wakati anatokea akaniambia ana sumu kali.

Naomba nijue jina lake na mengine muhimu ninayotakiwa kujua.

View attachment 1048752
Vitu vichache nilivyoona kuhusu huyu mdudu:
  1. Ana kichwa kigumu sana. Unaweza kumpiga na kiatu hata mara nne bado akawa hai.
  2. Anatembea kwa kasi sana. Huyu wa kwenye picha ni kwamba nilikuwa tu kwenye alert ila alikuwa anakuja kwangu kwa kasi.
  3. Akiwa anatembea kwenye corridor, anatembea kwenye corner kabisa iwe ngumu kumpiga.
  4. Hauwezi kumkuta ametulia tu. Usipomuwahi anaweza kupotelea kwenye makochi huko.
Vijana wa siku hizi mna akiri finyu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ninawajua hawa wadudu kiasi chake kutokana na mahali nilipokulia.... Tabora Manispaa..

1. Tandu hafuati uchafu kabisa kama wengi mnavyosema maana tandu anakula wadudu wengine wadogo zaidi yake na sio mabaki ya chakula. Tandu anapenda mahali penye joto na unyevu kwa mbali ndo maana akiingia kwenye nyumba anapenda kujificha mahali paliko rough, kama nguo zilizo tupwa tupwa, au kujificha kwenye viatu hivi e.t.c. tofautisha kuwa mchafu na kuwa rough

2. Tandu hapendi mwanga kabisa ndo maana ukimuona mchana au kwenye mwanga muda wote utamuona yuko kwenye speed anatafta mahali ajifiche.

3. Tandu akiwa mdogo anakuwa na sumu ya kawaida tu ambayo inaleta maumivu au anaweza asiwe na sumu kabisa pia hawezi kuua, na mara nyingi akiwa mdogo anakuwa na rangi ya khaki au brown. Ila jinsi anavyozidi kuwa mkubwa ndo sumu inakuwa kali, ukikutana na tandu mweusi na ana atenna zenye njano hv, au hata akiwa tu hivyo hivyo mweusi bila hizo antenna huyo ana uwezo wa kuua kwa sumu yake. Mtoto wa jirani aliwahi kufa sababu ya kuumwa na tandu mweusi mkubwa!

4. Tandu hapendi hali ya hewa nzuri au upepo wa baridi, kama unahisi chumbani au sebuleni kuna tandu, fungua mapazia vizuri au toa kabisa mapazia acha hewa iingie, kama inawezekana washa kabisa na feni then kaa mahali kwa nusu saa utamuona mwenyewe anapita pita kwa speed akitafuta pa kujificha(hapo uwe umepanga na vitu vyako vizuri kuondoa msongamano wa nguo au vitu visivyo kwenye mpangilio). Au unaweza kupulizia sumu ya wadudu kidogo then fungua madirisha na mlango ili hewa safi iingie atatoka mwenyewe, ingawa wengi wanasema kuwa sumu ya wadudu haiui tandu bali inamfanya anadhoofu tu then anaendelea kujibana hapo hapo alipo so njia nzuri ni kuweka hewa safi ndani ya nyumba atatoka

Hivyo ndo ninavyomjua tandu kwa experience yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkikulia tabora manispaa mnapewa elimu ya tandu au connection ni ipi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiiseee leo nimesikitika sana. Jana nimemsahau nyau wangu nje jamaa wamekuja kumuua asubuhi wameanza kumuona majirani amekufa daaaah kila mtu anemjua yule paka amesikitika sana.
Jamii itambue kwamba tunatofautiana sana, wengine tunapenda wanyama kama sehemu ya maisha yetu(pets) lakini wengine wakiona hivyo wanaanza kujenga hisia za kichawi eti oooooh paka gani hilo kama mtu, linaelewa kila kitu, halizururi hovyo, halidokoi na hata ukilipa chakula halisogei hadi mwenyewe alipe tena limetengewa sahani kama binadamu,sio bure yule anaroga kwa kutumia paka, aiseee nimeniuma sana.
R.I.P Mashal

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah,
So sorry mkuu.

Asante sana. Hii ni summary nzuri. Ndiyo uzuri wa kuwa na wachangiaji tofauti tofauti. Wengine walikuwa wanapotosha nikawa nawaangalia tu!

Ila mimi hata huo urough sina kwa kweli. Nimejua kwa case yangu, 100% ni giza na hewa ndogo kwa sababu kama nilivyosema awali, mara nyingi hamna mtu na madirisha hata mapazia yanakuwa yamefungwa.
 
Aiiseee leo nimesikitika sana. Jana nimemsahau nyau wangu nje jamaa wamekuja kumuua asubuhi wameanza kumuona majirani amekufa daaaah kila mtu anemjua yule paka amesikitika sana.
Jamii itambue kwamba tunatofautiana sana, wengine tunapenda wanyama kama sehemu ya maisha yetu(pets) lakini wengine wakiona hivyo wanaanza kujenga hisia za kichawi eti oooooh paka gani hilo kama mtu, linaelewa kila kitu, halizururi hovyo, halidokoi na hata ukilipa chakula halisogei hadi mwenyewe alipe tena limetengewa sahani kama binadamu,sio bure yule anaroga kwa kutumia paka, aiseee nimeniuma sana.
R.I.P Mashal

Sent using Jamii Forums mobile app

pole sana mkuu one day wabongo wataelewa tu faida za huyu kiumbe cha Mungu
 
Mkuu unamfahamj swila au unamsikia? Swila akiingia ndani usiku hua anatafuta njia kwa kugonga gonga yaani kama ni jikoni basi utakuta kagonga masufuria hadi vikombe

Sent using unknown device
swila(cobra) simuogopi hata kidogo...... nyoka anayenitisha kidogo sana ni koboko(black mamba) kutokana tu na speed yake..... lakini mimi huwa siui wala kuogopa nyoka wa aina yoyote.
 
Aliwahi kunipanda ndani ya suruali,nilipogutuka na kuitikisa alidondoka chini bila ya kuniuma na alishafika usawa wa goti ndio nikastuka...
 
Huyo ni tandu. Anasumu kali sana.
Anapenda sana nyumba zenye uchafu.
Nyumba yako inaelekea ni chafu sana na kuna makorokoro mengi kama viatu vya zamani visivyo tumiwa nk.
Mwanamke gani wewe mchafu hivyo na huoni aibu ya kuanika uchafu wako.
Wanaume utaishia kukutana nao gesti na sahau ndoa kama huyajirekebisha.
Yote haya ya nn au unaugomvi nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila baada ya wiki kadhaa, nimekuwa nakumbana na mdudu huyu ndani ya nyumba. Uzuri mara zote nimekuwa namuwahi kumuua kabla hajanigusa.

Kuna mtu alikuwepo nymbani siku moja wakati anatokea akaniambia ana sumu kali.

Naomba nijue jina lake na mengine muhimu ninayotakiwa kujua.

View attachment 1048752
Vitu vichache nilivyoona kuhusu huyu mdudu:
  1. Ana kichwa kigumu sana. Unaweza kumpiga na kiatu hata mara nne bado akawa hai.
  2. Anatembea kwa kasi sana. Huyu wa kwenye picha ni kwamba nilikuwa tu kwenye alert ila alikuwa anakuja kwangu kwa kasi.
  3. Akiwa anatembea kwenye corridor, anatembea kwenye corner kabisa iwe ngumu kumpiga.
  4. Hauwezi kumkuta ametulia tu. Usipomuwahi anaweza kupotelea kwenye makochi huko.

Ninanachokiona mimi, kumjua huyu mdudu kwa jina haikusaidii wewe kujinkinga na madhara yake. Nashauri ukanunue dawa ya kuua wadudu na uwe unakaa nayo karibu muda wote. Unaweza kumuona Daktari pia akakushauri ni aina gani ya dawa ambayo ni sahihi kwa kumwangamiza, ila ninahisi kama insect killers hizi za kawaida, zinaweza kumuua lakini ili uwe na uhakika zidi unaweza ukaenda ukamuona Daktari akakuandikia the right prescription ambayo inaweza kum-handle kisawasawa, dawa ambayo possibly hata harufu yake tu inaweza kumuua.

Zaidi ni kuwa kuna mtu aliwahi kunishuhudia kuwa huyu mdudu wakati mwingine anakuwa associated na mambo ya kwenye ulimwenu wa roho, kwamba anaweza akatumwa kwako kwa ajili ya kuja kukudhuru. Huyu mtu alinipa pia evidence kadhaa za kutetea argument yake na hadi akanionyesha na mtu aliyewahi kumtuma kwake mdudu huyo na nilifikia hatua ya kumwamini kwa angalau 99% lakini imani yangu kuwa katika kiwango hicho hai-guarantee kwamba huyu mtu aliyenipa kisa hiki alikuwa sahihi!

Mwisho,kama wewe ni Mkristo, mwamuru mdudu huyo apotee milele kwenye nyumba yako kuanzia sasa na hata milele, kwa Jina la Yesu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom