Huyu ni mdudu Tandu? ana madhara gani?

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Kila baada ya wiki kadhaa, nimekuwa nakumbana na mdudu huyu ndani ya nyumba. Uzuri mara zote nimekuwa namuwahi kumuua kabla hajanigusa.

Kuna mtu alikuwepo nymbani siku moja wakati anatokea akaniambia ana sumu kali.

Naomba nijue jina lake na mengine muhimu ninayotakiwa kujua.

PSX_20190319_032525.jpg

Vitu vichache nilivyoona kuhusu huyu mdudu:
  1. Ana kichwa kigumu sana. Unaweza kumpiga na kiatu hata mara nne bado akawa hai.
  2. Anatembea kwa kasi sana. Huyu wa kwenye picha ni kwamba nilikuwa tu kwenye alert ila alikuwa anakuja kwangu kwa kasi.
  3. Akiwa anatembea kwenye corridor, anatembea kwenye corner kabisa iwe ngumu kumpiga.
  4. Hauwezi kumkuta ametulia tu. Usipomuwahi anaweza kupotelea kwenye makochi huko.
 
Mkuu huyo ni tandu, anasumu kali sana ila wakiwa wadogo kiumbo wanatabia ya kuingia sikioni ukiwa umelala na kung'ata . (Hasa kwa watoto/w.wazima)

Unaweza changanyikiwa!

Btw kama wapo wengi chukua tahadhali maana sumu yake ni konk mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Baada ya King Kong kunipa jina nimecheki Google.

Wanasema wanasaidia kuua wadudu wengine kama mende na kwamba wanapokuuma unaweza pata maumivu ila yanaisha ndani ya siku mbili.

Wanasema specie hii ya wadogo hawana sumu ya kukuua!

Wanadai ni vizuri kuwaacha, unajua tena mambo ya mabeberu. Kumbe Wajapan wanawafuga kama pets.
 
Aisee

Hahaa mabeberu bwana dah !!! Ila kama unauwezo wa kumzuia ili asikung'ate basi unamtoa nje tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni tandu.... ana tabia kama za nyoka kwamba ukipishana naye na yeye anapishana na wewe..... anakula wadudu wadogowadgo na anapenda sehemu zenye joto...... hana sumu ya kuua lakini maumivu ni makali...... WAPO AINA NYINGI.... KUNA WAKUBWA AMBAO AKIKUOTEA UNAKUFA.
 
Huyo ni tandu. Anasumu kali sana.
Anapenda sana nyumba zenye uchafu.
Nyumba yako inaelekea ni chafu sana na kuna makorokoro mengi kama viatu vya zamani visivyo tumiwa nk.
Mwanamke gani wewe mchafu hivyo na huoni aibu ya kuanika uchafu wako.
Wanaume utaishia kukutana nao gesti na sahau ndoa kama huyajirekebisha.
 
Baada ya King Kong kunipa jina nimecheki Google.

Wanasema wanasaidia kuua wadudu wengine kama mende na kwamba wanapokuuma unaweza pata maumivu ila yanaisha ndani ya siku mbili.

Wanasema specie hii ya wadogo hawana sumu ya kukuua!

Wanadai ni vizuri kuwaacha, unajua tena mambo ya mabeberu. Kumbe Wajapan wanawafuga kama pets.
species tofauti mazee wale wa vyooni hawana madhara sana ila wale warefu tena ykikutana na yule aliyekomaa anaweza kukuua hasa hsa mtu akiwa alergic na bites za wadudu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni tandu. Anasumu kali sana.
Anapenda sana nyumba zenye uchafu.
Nyumba yako inaelekea ni chafu sana na kuna makorokoro mengi kama viatu vya zamani visivyo tumiwa nk.
Mwanamke gani wewe mchafu hivyo na huoni aibu ya kuanika uchafu wako.
Wanaume utaishia kukutana nao gesti na sahau ndoa kama huyajirekebisha.
Eh eh atakuja fuga nyoka....AF mbaya zaidi wanapenda sana vitanda visivyotandikwa.......ye anakwambia anataka watumia ka dawa ya mende utadhan anakaa chooni
 
Kila baada ya wiki kadhaa, nimekuwa nakumbana na mdudu huyu ndani ya nyumba. Uzuri mara zote nimekuwa namuwahi kumuua kabla hajanigusa.

Kuna mtu alikuwepo nymbani siku moja wakati anatokea akaniambia ana sumu kali.

Naomba nijue jina lake na mengine muhimu ninayotakiwa kujua.

View attachment 1048752
Vitu vichache nilivyoona kuhusu huyu mdudu:
  1. Ana kichwa kigumu sana. Unaweza kumpiga na kiatu hata mara nne bado akawa hai.
  2. Anatembea kwa kasi sana. Huyu wa kwenye picha ni kwamba nilikuwa tu kwenye alert ila alikuwa anakuja kwangu kwa kasi.
  3. Akiwa anatembea kwenye corridor, anatembea kwenye corner kabisa iwe ngumu kumpiga.
  4. Hauwezi kumkuta ametulia tu. Usipomuwahi anaweza kupotelea kwenye makochi huko.
Anafanana na tandu ila tandu ukimuua mara moja hafufuki na kurudi tena. Tandu wa kawaida anayo sumu endapo atakuuma na hupenda kuishi sehemu zenye udongo na unyevunyevu, hakikisha chumba chako unaweka sakafu na madirisha mapana yanayoingiza hewa na mwanga na kufanya chumba kiwe kikavu.
 
Usiue ovyo Viumbe hai, tambua kuwa kila kiumbe ana haki ya kuishi. Endapo kiumbe kaingia kwenye himaya yako usimdhuru bali mtoe na kumweka kwenye mazingira wezeshi ya yeye kuishi, ama la muite AFISA MALIASILI WA HALMASHAURI ndizo kazi zao za Uhifadhi. Zingatia ushauri huu ili tusitokomeze baadhi ya Viumbe. Nowdays hata kumuona kobe imekuwa nadra, mijusi, vippepeo, nyigu nk hiii yote ni kutokana na Elimu duni ya Viumbe tuliyonayo hasa Kuwaua viumbe pasipo kuwa na matumizi nao. Utakuta Watoto wanaua panzi, mijusi, ndege nk with no reason. Wizara husika imelala fofoooooo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom