Huyu ndio firauni

Kwani allah kasemaje mkuu juu ya firauni.

Naomba uninukulie aya..

Soma Surat Yunus anza aya ya 90-92.

Hapo kwenye aya ya 91 utaona ahadi ya Allah juu ya Firauni pale adhabu ilipokuwa ikimshika akasema; amantu innahu laa illaha illa ladhii amanat bihi banu israil wa anaa minalmuslimin, yaani; "nimemuanini hakika hakuna Mungu ila yule ambaye wana wa Israeli wana muamini na mimi ni miongoni waliojisalimisha".

Sasa soma aya ya 92 usikie Allah akiahidi nini atafanya juu ya mwili wa huyo Firauni.
 
Mkuu nimeomba uweke aya hapa,sio unielekeze ipo wapi.

Kama hili ombi langu halina maana yeyote kwako mkuu naomba tukomee hapa.
 
Mkuu nimeomba uweke aya hapa,sio unielekeze ipo wapi.

Kama hili ombi langu halina maana yeyote kwako mkuu naomba tukomee hapa.
Screenshot_20210714-211549.png
 
Kama firauni huyu ndie yule wa kwenye Qurani wa nabii mussa basi hapa uhakika tumepigwa hasaa.
Wanazuoni wetu wakubwa wanakataa ya kuwa huyu si yule aliye zungumziwa katika Qur'aan na kwamba ayahifadhiwa,sababu walio kusudiwa ili wuone ni wale wale Waisraeli wa zama hizo na wali muona na ikawa ushahidi kwao.

Hakuna anaye weza kuthibitisha ya kuwa huyu ni yeye na kumnasibisha na aya ya Qur'aan ni uchachefu wa maarifa. Shaykh Ibn 'Uthaymiin (Allah amrehemu) ameliezea hili kwa upana.

Ziada ya maneno kuhusu mwili wa Firaun,ni baada ya wana wa Israeli walikuwa wana shaka juu ya kifo cha Firaun,ndiyo maana Allah akaimrisha bahari imteme,na kweli walikuja kumuona na kusadiki,haya ameuasema swahaba Ibn Abbas,rejea Tafsir Ibn Kathir. Kadhalika maelezo ya Imamu Mujaahidi.

Kadhalika rejea Tafsir ya Ibn Ashuuri iitwayo "Tahriri wa Tanwiir".
 
safuher.

Huu ni miongoni mwa muujiza wa Qur'an tukufu kwamba ni kitabu kilichotoka kwa Allah, leo hii sisi (watu tuliokuwa) nyuma ya mwili huo, watu tulikuja baada ya miaka takriban 4000 leo tunaweza kwenda kushuhudia ishara ya Allah aliyoitaja ndani ya Qur'an, watu tunakwenda kuona mwili wa Firauni aliyekuwa jeuri na mwenye kibri aliyempinga Nabii wa Allah--- Maneno na ahadi za Allah kamwe haziwezi kuanguka.
 
Mapharao wote walifanyiwa mumyfication ila kuna wanaodanganya watu kuwa pHarao alilaaniwa na mungu fvck mpaka lini watu wataendelea kushikiwa akili

Unachosema ni kweli kwamba Mafarao wote miili yao ilikuwa mumified (kukaushwa) na hii ilikuwa ni jadi au mila yenye fahari kubwa sana kwao, lakini katika hao Mafarao aliyekuwa Jeuri na Katili na kibri ni huyo Farao wa Musa (the pharaoh of oppression/Marenpth), huyu alikulia nyumba moja ya kifalme pamoja na Musa, kipindi hicho Baba yake ndiye alikuwa Farao, hivyo Nabii Musa alikuwa anamjua vizuri sana tabia za huyo Firauni of oppression.

Musa alipokimbia nchi pale alipoua mtu kwa ngumi baada ya miaka kupita yule Firauni aliyewalea Musa na huyo Marenptha akafariki ndipo Marenptha akawatawazwa kuwa Farao na Musa akapata hizo habari akiwa ukimbizini kwamba Marenptha kawa Farao, na kama utasoma Qur'an utaona jinsi Musa alivyomjibu Mungu akiwa na khofu kwamba atawezaje kumpelekea ujumbe wa Mungu kwamba kuna Mungu mwingine na sio yeye Firauni na pia huyo Mungu anataka kuwachukua wana wa Israeli na aindoke nao, Musa alikuwa anamjua toka walipokuwa watoto
jinsi Pharao Marenptha alivyokuwa Jeuri na kibri.

Kifupi ni kwamba, ni Farao marenptha ndiye aliyekuwa katili na jeuri na ndiye huyo aliyejiita Mungu na akataka aabudiwe na Mungu akamuadhibu kwa kumzamisha majini huku akitubu na kumkiri Mungu wa Musa--- ndipo Mungu akasema atauhifadhi mwili wake ili iwe ishara kwa watu wajao, mwili unapokuwa majini unaweza kuharibika au kuliwa na samaki nk, lakini Mungu alitaka Mwili wa huyo Firauni upatikane na ufanyiwe Mumification ili iwe ishara kwetu kwamba alipita mtu mmoja mwembamba, jeuri, katili, kibri aliyejifanya Mungu na alipingana na Nabii wa Mungu.
 
Imeshindikana kupata torati ya mussa aje kupatikana huyo firauni

Jambo hiwezekani kabisa akawa firauni huyo.
Mungu aliahidi kuuweka mwili wake kama ukumbusho mpaka siku ya mwisho,lakini hakuahidi kuiweka torati(kitabu halisi alichoshushiwa Mussa na watu wake)
 
Mungu aliahidi kuuweka mwili wake kama ukumbusho mpaka siku ya mwisho,lakini hakuahidi kuiweka torati(kitabu halisi alichoshushiwa Mussa na watu wake)
Nipe aya inayosema mpaka siku ya mwisho Mungu aliahidi kumuweka firauni.
 
Mkuu hii aya imesema

"..walio nyuma yako "

Yaani watu ambao tayari wapo katika wakati huo.

Na aya haokusema "watakaokuja baadae"

Makusudio ya aya ni wale ambao waliokuwepo wakati wa firauni na sio mpaka akina sisi wa hivi leo.

Aya haikushindwa kusema ".watakaokuja baada ya firauni..."

Lakini makusudio kama ilivyo aya inavyosema haigusii watu wa baadae.

Hivyo huyo atabaki kuwa firauni feki wa kibiashara mkuu.
 
Kwa hiyo ile aliyoweka mokaze bado haitoshelezi?
Haitoshelezi kwa mujibu wa atavyotaka yeye.

Aya inatosheleza kwa mujibu wa ilivyosema yenyewe.

Mkuu hii aya imesema

"..walio nyuma yako "

Yaani watu ambao tayari wapo katika wakati huo.

Na aya haokusema "watakaokuja baadae"

Makusudio ya aya ni wale ambao waliokuwepo wakati wa firauni na sio mpaka akina sisi wa hivi leo.

Aya haikushindwa kusema ".watakaokuja baada ya firauni..."

Lakini makusudio kama ilivyo aya inavyosema haigusii watu wa baadae.

Hivyo huyo atabaki kuwa firauni feki wa kibiashara mkuu
 
Sasa hapo firaunj anahusika vipi?

Hiyo ni moja ya aya zinazomzungumzia Firauni jinsi alivyogharikishwa na alivyoomba mkiri Allah na Allah alivyo ahidi kile angemtendea, angalia moja ya aya hii ya juu yake inavyosema:-
Screenshot_20210714-232915.png
 
Hiyo ni moja ya aya zinazomzungumzia Firauni jinsi alivyogharikishwa na alivyoomba mkiri Allah na Allah alivyo ahidi kile angemtendea, angalia moja ya aya hii ya juu yake inavyosema:-
View attachment 1854125
Mkuu hakuna aya inasema kwamba firauni atabaki milele mpaka siku ya mwisho iyo aya haipo.

Huyu firauni wakati aya hiyo inashika kwa Mtume ambae kaja baada ya firauni mtume hakufasiri kwamba eti firauni yupo kwa zama zile.

Hii tafsiri ya kwamba yupo tokea zama zile hakufundisha mtume.

Na mtume ndo kashushiwa Qurani.

Na sisi tunamjua firauni kupitia Qurani.
.hivyo madai ya firauni huyu yanabaki kuwa ni madai yanayokosa uthibitisho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom