Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

JK katika moja ya hotuba zake kubwa mwanzoni mwa uraisi wake alisema: Kama viatu vya uraisi havitamtosha, atajaza makaratasi. Makaratasi yenyewe ndiyo hayo yanaonekana sasa.....
 
Mkuyuga,

Tuko hapa kukemea mabaya tena kwa nguvu zote. Tunachokataa ni kufumba macho na kudai kuwa Nyerere alikuwa malaika wakati enzi zake mambo yalikuwa mabaya saaaana na laiti kama si Mzee Ruksa tungedidimia sana. Haya hayaonekani na badala yake Mzee Ruksa anakashifiwa na vijana ninyi ninyi ambao hamkuwa wakubwa wa kutosha kuona tofauti iliyotokea mwaka 1985. Ninyi acheni tu msitukumbushe mengi.

"APENDAE CHONGO HUITA KENGEZA"
 
Jizaledo said:
Mkuyuga,

Tuko hapa kukemea mabaya tena kwa nguvu zote. Tunachokataa ni kufumba macho na kudai kuwa Nyerere alikuwa malaika wakati enzi zake mambo yalikuwa mabaya saaaana na laiti kama si Mzee Ruksa tungedidimia sana. Haya hayaonekani na badala yake Mzee Ruksa anakashifiwa na vijana ninyi ninyi ambao hamkuwa wakubwa wa kutosha kuona tofauti iliyotokea mwaka 1985. Ninyi acheni tu msitukumbushe mengi.

"APENDAE CHONGO HUITA KENGEZA"
Nadhani hii ulikusudia kuiweka kule kwenye mada ya ukweli kuhusu JK Nyerere.. au sio?
 
Hapana, Kulikoni,

Hii ni ya hapa hapa na imelenga anayopayuka mkuyuga hapo juu kama ninavyomkariri hapa chini.

mkuyuga said:
humu tunajua wamo ambao wanataka serikali iendelee kufanya madudu ili wanufaike!

ndiyo maana sioni ajabu kwa mtu kuja hapa aksema eti kwa kuwa tulikuwa kimya wakati wa nyerere sasa tusiongee!!

Kwanza wengine tulikuwa wadogo saaaana!

cha maana hapa ni kuwa ingelitakiwa Mwniyo afanye VIZURI KULIKO NYERERE NA HAPO TUNGESONGA MBELE. NA PIA MKAPA ANGETAKIWA KUFANYA VIZURI ZAIDI KULIKO NYERERE NA MWINYI. NA KWA SASA TUNAMTAKA KIKWETE AFANYE VIZURI KULIKO WOTE TENA YEYE SASA ANAONGOZA WATANZANIA WENGI WAO WAKIWA NA MADGREE KIBAO! DIPLOMA USISEME!

SASA HUYO ANAYEKUJA NA UHNI WAKE ETI TUKAE KIMYA ANA MAANA GANI HUYO?!

HUMU WENGINE TUNAJUA MNTAKA UDINI UTAWALE ILI MUENDELEE KUPTA ULAJI AU MNATAKA UKABILA UTAWALE ILI MUENDELEE KUJINEEMESHA!

WAMO WAKWELI NA TUNAWAONA TU WAKITOA MAJAMBOSI HUMU!

SAS HIVI TUNATAKA KIONGOZI ANGALIE MBELE MBELE KWA MAENDELEO ZAIDI. PIA AREKEBISHE PALE AKINA NYERERE, MWINYI NA MKAPA WAMEHARIBU ILI TUSONGE MBELE!

WEWE UNAYETUTISHA ACHA UHNI WAKO!
 
Mzee Es,
Vipi mbona sikuona kitu? nasubiri hiyo PM....
Jamani haya maswala ya JKN nadhani hapa sii pake kwani kuna wengine akina sisi hatuwezi kabisa kuvumilia madongo kwa marehemu hali nyie nyote mnaweza kukaa, kuandika na pengine elimu yenu imetokana na mzee JKN. Kuna tofauti kubwa sana ya malezi ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano, kumi na yule aliyekwisha fikia barehe. Tanzania ilikuwa nchi changa ambayo ilihitaji malezi tofauti na haya ya leo. Kama tulikosa sukari na kupanga foleni bado haijambo kwani hakufa mtu kisha basi tuliambiwa sababu kuwa ni vita ya Uganda na tuliombwa tujifunge mkanda (uvumilivu) -Tukakubali.
Wakati wa Mwinyi na Mkapa watu wamekufa kwa njaa! wamekufa kwa usafiri wa hakika reli, meli acha mbali magonjwa madogo madogo kama Maleria. Miradi mipya hakuna zaidi ya kuuza ile aliyoianzisha mwalimu, naa bado mnamshikia bango mzee wa watu kama vile kuna mtu kasema Nyerere ni mtume wa Mungu. Nambieni hata rais mmoja Afrika ambaye kajenga reli, Kaanzisha shirka la meli la kitaifa, hotel za serikali za uhakika kama tulizokuwa nazo. Tiper (kwanza labda hamfahamu kwamba ni nchi chache sana Afrika zinazosafisha mafuta acha kujengwa na wakoloni). Nguvu za Umeme wa hydro leo hii mnachemsha na kuanza kulaumu JKN kama mlivyolaumu wakati wa Mwinyi kuwa Nyerere kawaachieni magofu.
Guys kama kuishi miaka hiyo ya Nyerere tulikuwepo na wengine sisi tumetoka mbali! toka maisha ya vijijini hadi mjini na tumekawa maalwatan.
Wakati wa Nyerere tuliponzwa na siasa ambayo wengi wetu hatukufahamu malengo yake. Na hii imetokana na kuwa wengi wetu tulikuwa na upeo mdogo wa kuangalia maendeleo (short term) kama tunavyoendesha maisha yetu ya kila siku. Starehe mbele na maisha ya kula mara tatu kwa siku na kulala saa nane mchana, chini ya hapo ni utumwa. Acheni nyie jamani acheni mzee wa watu apate pepo.
Swala hapa (mada hii) ni kama tunaweza kuendelea kumwamini JK!...huyu baba wa nne ambaye kamkuta mama wetu akiwa na mali kibao za urithi. Urithi ambao usingekuwepo leo hii kama baba wa kwanza JKN angeamua tujirushe hali bado tukiwa hatuna barehe kiuchumi!... Leo mmebarehe mnaanza kutafuta sababu za kutofanikiwa kwenu.. Loooh!
 
Jizaledo said:
Mkuyuga,

Tuko hapa kukemea mabaya tena kwa nguvu zote. Tunachokataa ni kufumba macho na kudai kuwa Nyerere alikuwa malaika wakati enzi zake mambo yalikuwa mabaya saaaana na laiti kama si Mzee Ruksa tungedidimia sana. Haya hayaonekani na badala yake Mzee Ruksa anakashifiwa na vijana ninyi ninyi ambao hamkuwa wakubwa wa kutosha kuona tofauti iliyotokea mwaka 1985. Ninyi acheni tu msitukumbushe mengi.

"APENDAE CHONGO HUITA KENGEZA"

Jizalendo nakuhesimu lakini hapa umeniangusha kidogo labda kwa vile hukutoa mchanganuo mzima wa tamatisho lako.

Kama ulikuwa ukifuatilia mwenendo mzima wa nchi, utagundua kuwa Mwinyi hakuleta lolote la maana katika Tanzania. Mabadiliko ya mwenendo wa Uchumi yalikuwa ni utekelzaji wa maelekezo ya IMF na World Bank ambayo yalikuwa yamefanyiwa kazi na na kukubalika na serikali ya Nyerere katika kipindi cha mwisho mwisho na yalianza kutekelezeka katikati ya mwaka 1985 hata kabla ya Mwinyi kuingia madarakani mwishoni mwa mwaka 1985. Asingeingia madarakani na papo hapo kuanza mazungumzo na IMF an World bank na papo hapo kupata mkopo.

Tofauti ya Mwinyi na Nyerere ni kwamba wakati anajadiliana na IMF kuhusu mikopo hiyo alikwa akiyachambua masharti yote kwa marefu na mapana na ndiyo maana zoezi zima lilichukua muda wa karibu miaka minne kukamilika. Mwinyi na wale waliomfuata walipoingia hawakuwa na muda kuchambua mambo wanayoambia na taasisi hizi na ndiyo maana leo wanalumiwa. Zaidi zaidi ni kwamba mikopo iliyotolewa na IMF iliishia mifukoni mwa wao wenyewe wachache na leo hii Tanzania imetelemka kuwa ya 4 kwa umaskini. Wakati Nyerere anaondoka aliiacha ikiwa ya 18 kutoka chini; at least nchi kama Rwanda, Burundi na Haiti zilikuwa hazitupiti.


Swala la Mwinyi na Nyerere kuhusu mabadiliko ya Uchumi ni kama swala la Mwinyi na Mkapa kuhusu ukusanyaji wa kodi. Baada ya Mwinyi kuvuruga pesa za wafadhali walimkalia koo aweke utaratibu mzuri wa ukusanyaji kodi. Ni kutokana na shinikizo hilo ndipo TRA ilipoanzishwa. Hivyo Mkapa alipoingia,. alikuta utaratibnu wa kukusanya kodi umekwisha tengenzwa lakini baadaye nimekuwa nasikia watu wakimsifia kuwa alileta utaratibu mzuri wa kukusanya mapato ya serikali wakati in fact hiyo ni kazi iliyofanywa mwinyi baada ya kubanwa na wafadhili na nadhani ilisimamiwa na World Bank

Tofauti kubwa ya Mwinyi, Mkapa na Nyerere ni kwamba Nyerere alikuwa too sensitive na masharti ya IMF na World Bank wakati Mkapa na Mwinyi walikuwa too loose na masharti hayo. Kutokana na looseness yao nchi imeporomoka kutoka ya 18 wakati wa Nyerere hadi ya 4 wakati huu, wakati sinsivity ya Nyerere ilisababisha nchi ichelewe kupata mkopo huo wa IMF ambao sasa unatutokea puani. Kumbuka kuwa mashirika yote ambayo yalikuja uzwa na Mkapa na Mwinyi yalianzishwa na Nyerere. Nyerere alisistiza kujenga Tanzania inayojitegemea, lakini wenzake walikuja na sera ya kujenga Tanzania isiyokuwa na chake. In general walikuwa dimaterically opposite.

Failure kubwa sana ya Nyerere siyo sensitivity yake kwa IMF na hivyo kuchelewa kupata mikopo na hivyo kuwa na bajeti finyu sana katika kipindi cha kuanzia mwaka 1980 (baada ya vita) mpaka mwishoni mwa mwaka 1984. Failure yake kubwa ni kuwaamini viazi wengi sana kama mawaziri wake. Watu kama Mkapa, Malecela, Mwinyi walikuwa mawaziri wake na ndio wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuiacha Tanzania ikiwa ya nne kutoka chini kwa umaskini duniani pamoja na kuwa na deposit nyingi sana ya madini, na envirnoment ya kichumi duniani ikiwa nzuri kuliko nyakati za Nyerere.

Nyerere alioperate katika mazingira ya cold war ambapo uchumi wa dunia kwa jumla ulikuwa umedumaa. Mara baada ya cold war wakati wa mwinyi na Mkapa, nchi nyingi zimeendela kiuchumi lakini a Tanzani imezidi kurudi nyuma tu. DJIA ya Marekani ilikuwa kutoka points 3400 hivi hadi kufikia points 11,400 katika kipindi baada ya vita baridi, lakini Tanzania haikufanya lolote. China na India zimekuwa kwa kasi sana katika hicho, na hata Uingereza kwa mama uchumi wao ulisimama vizuri wakati huo.
 
Kichuguu,

Hongera kwa utafutaji wa data. Haya ndiyo yanayotakiwa kujadiliwa. Halafu tukihitimisha takwimu ambazo ni takwimu tu tutowe inference yake ambayo hapa ni "maisha ya Mtanzania" kwa takwimu zote hizo. Mwalim JKN alitoka zero kwenye uchumi ingawa alifanya mengi ya ubinadamu:

1. Aliweka misingi ya usawa wa binadamu sio Tanzania tu bali popote binaadam alipo. Na alitekeleza hili kwa vitendo na hivyo gharama kwa taifa na uchumi wake. Haiyumkini sis kusambaza resources zetu Kusini mwa Afrika aili hali nyumbani tulikuwa tunakufa njaa. Baada ya nci hizi kukombolewa ni nini tumeambulia - ujamaa house pale maputo na Nyere Streets karibu kila nchi ya Kusini mwa Afrika. Kiuchumi hakuna tulichopata. Kisiasa - tunatakiwa kuwa na visa nchi zote isipokuwa kule ambako visa hatutakiwi kwa mfumo wa ukoloni wa Commonwealth. Afrika Kusini tunatakiwa hadi chnjo za yellow Fever kisha kwa kebehi. Ni nani mwengine aliyetumia mali za Taifa akaambulia haya. Wakenya na waSenegal ambao hawakutaka kujuwa kamwe vita hivi wanapendelewa kwa haya pamoja ya kuwa sio hata wanachama wa SADC. Kweli vita vile vilikuwa vinaangalia maisha ya Mtanzania? Labda niseme kuwa wakati mwengine ninajifariji kuwa tusingepigana vita hivyo labda hawa Makaburu wangesonga mbele hadi kutufikia na sisi kwa ubaguzi wao. Lakini mbona ninajirudi tena ninapoona bado wanafanya hivyo hivyo sasa hivi, asante bwana Mkapa.

Mwalim kwa urafiki wake na Milton Obote, alilaani Iddi Amin na mapinduzi aliyofanya Uganda immediately na kumfanya Idi Amin atuone maadui right from the beginning. Matokeo yake again mali na maisha yetu yakapotea kumtowa Uganda. Tumepata nini katika hicho kiuchumi - jibu ni hakuna.

Katika kuthamini ubinadamu Mwalim alikuwa msitari wa mbele sana lakini kamwe hakujali tahadhari yakujihusisha katika mambo ya watu wengine kwa uchumi wetu.

Hebu jaribu kufanya uchunguzi kwa Wananchi wa kawaida, ambao ndio wanaomatter hapa wakuambie ni awamu ya Raisi yupi maisha yao yalikuwa na nafuu; na ninakuhakikishia Mzee Ruksa chati yake utaiona iko juu kiasi gani.
 
Jizalendo, tunamshuru saaaaaaaana mzee mwinyi kwa kuletea unga ambao umesaidia sana vijana wetu kufaika na huo uchumi wake!!


kuna vijana wetu wamefungwa Pakstani, wengine greece, Italy etc,

Ametutengezea alikaida ndiyo maana vijana wetu kama kufungwa huko marekani.

wakati wake wapasitani walizunguka nchi nzima wakihubiri dini!!

Wakati wa mwinyi alikuza saaaaaaaaana uchumi hadi watu wakawa wanabeba hela kwenye magunia!!

Uchumi wake ulikuwa sana akawa na maduka ya vito arabuni, je unjua kwa nini bodyguard wake alikufa huko arabuni?


Hongera mwinyi kukuza uchumi wa tanzania, hadi wanya wetu sasa wanauzwa nje, pia tausi walipewa kwa maswahiba wake(ref, bungeni).

ngoja niishie hapa sitabishana tena na wewe maana wewe unaoneka unataka kuvuruga umoja wetu humu kwa kugawa watu katika makundi ya dini!

wanabodi kuweni makini na huyu mtu.!
 
Mzee Mkandara(Bob), Mkuyuga na Kichuguu maneno yenu mazito heshima zenu wazee .I will never and I cannot today trust JK .
 
unajua sababu iliyomfanya mwalimu aingie kwemye siasa ilikuwa ni moja tu,
nayo ni kupinga ukoloni,ubeberu na unyanyaswaji wa mtu mweusi.
ndio maana mwalimu alipoulizwa ilikuwaje ukaingia kwenye siasa na yeye akajibu,
nilikuwa mwalimu kwa kuchagua na siasa ilikuwa kama ajari(a teacher by choice and politician by accident)
na alipohojiwa kuhusu sera zake za ujamaa,
mwalimu alitoa maelezo ambayo kwa mtu mwenye utashi hasa mtanzania usingeweza kumlaumu,
akitetea sera za ujamaa mwalimu alieleza kuwa miaka michache baada ya kupata uhuru akaona kuwa kuna aina mpya ya ubaguzi umeingia tanzania,kulikuwa kuna matabaka yameanza kuonekana kati ya watu maskini na watu tajiri,viongozi walianza kuwa wakoloni weusi dhidi ya weusi wenzao maskini,yeye akasema kuwa uhuru ule tuliopata ulikuwa sio tu kwasababu ya kumuondoa mkoroni kwasababu alikuwa ni mtu mweupe, bali ulikuwa ni ukombozi kamili kwa watanzania wote,ndipo hapo alipokuja na siasa ya ujamaa na kujitegemea na nguvu zilipelekwa vijijini ambako asilimia kubwa ya watanzania ambao ni maskini waliishi huko.
mwalimu aliendelea na siasa za ukombozi si tu tanzania bali kusini kwote mwa afrika na wala hakutaka malipo yeyote,
yeye alielewa zaidi kuwa hii mipaka yote tuliyonayo afrika ilichorwa na wakoloni tena nchini ujerumani ,
nyerere aliamini afrika ni moja ndio maana alishiriki kikamilifu katika harakati za kuundwa umoja wa nchi huru za afrika, na lengo ilikuwa ni kuunda taifa moja la afrika,lakini kutokana na ujinga wa afrika wengi kama akina mobutu seseko ambao walikuwa wakitumiwa na westerners malengo hayakufanikiwa,
hapa nyumbani kama mnavyoona huu muungano wa tanganyika na zanzibar na ule wa afrika mashariki ni yeye ndiye alikuwa kiranja mkuu,
muungano wa zanzibar ndio muungano pekee auliobaki hapa afrika,
alipokuja dictor idd amin,kuwatesa waganda na kutishia amani ya tanzania mwalimu hakusita kumfundisha adabu na kumfukuzia mbali kiasi kwamba mpaka leo hata waganda wanasema nyerere ni mkombozi wao, kwamaneno mengine historia ya uganda haijakamilika bila ya julius nyerere na yeye hakuitaji malipo yeyote yale kutoka kwa waganda.
ukienda kule morogoro maeneo ya mzumbe utakuta kuna makambi ya wanaharakakti wa afrika kusini,yaani mapamambo dhidi ya ukaburu wa afrika kusini alikuwa yanatokea tanzania,we must be proud of it,hatuhitaji malipo yeyote kutoka kwa waafrika kusini lakini tumepigania haki.
 
Hatuwezi kumlaumu Jk kwa kila kitu kwani kuna mgawanyo wa madaraka.One thing iwapo haya yaliyojitokeza ni kweli Jk lazima amwajibishe mtu.
 
kichuguu said:
Jizalendo nakuhesimu lakini hapa umeniangusha kidogo labda kwa vile hukutoa mchanganuo mzima wa tamatisho lako.

Kama ulikuwa ukifuatilia mwenendo mzima wa nchi, utagundua kuwa Mwinyi hakuleta lolote la maana katika Tanzania. Mabadiliko ya mwenendo wa Uchumi yalikuwa ni utekelzaji wa maelekezo ya IMF na World Bank ambayo yalikuwa yamefanyiwa kazi na na kukubalika na serikali ya Nyerere katika kipindi cha mwisho mwisho na yalianza kutekelezeka katikati ya mwaka 1985 hata kabla ya Mwinyi kuingia madarakani mwishoni mwa mwaka 1985. Asingeingia madarakani na papo hapo kuanza mazungumzo na IMF an World bank na papo hapo kupata mkopo. .........................

Mzee Kichuguu, hii analysis uliyotoa safi sana!
 
Tanzania sasa tunakabiliwa na tatizo jingine kubwa sana nalo ni TZ MEDIA kuwaficha wananchi Uozo na ufisadi unaoendelea ndani ya serikali zetu.TZ MEDIA sasa wanaangalia maslahi yao binafsi badala ya nchi.Tusiopolikemea hili tatizo naamini tufafikia mahali pabaya zaidi.Kwa sababu sikuzote serikali inanyooshwa kutokana na maoni kutoka kwa Trade Unions na NG'S ambazo tanzania ni kama hakuna; Pili opposition party, na tatu MEDIA.TZ MEDIA badala ya kuikemea serikali na kufichua huozo viko busy kuifagilia serikali ya JK hata pale pasipowezekana kufagilika. Siku hizi wamezua mchezo kila JK akiharibu wanasema "KASHAURIWA VIBAYA". Huu wimbo kashauriwa vibaya utaisha lini.?Yeye (JK) hana akili mpaka kila siku ashauliwe vibaya? Vinginevyo waandishi wanataka tuamini JK ni kilaza. TZ MEDIA lazima wajue kwamba "la kuvunda halina ubani". JK alishavunda siku nyingi. Kuchoma Ubani na kupulizia Utuli kunakofanywa na TZMEDIA hakuta saidia kitu ni sawa na kuipiga maiti konzi.
 
mkuyuga,

Haya ndiyo aliyoyalete Mzee Mwinyi? Hivi ndivyo unavyoamini kwa dhati ya moyo wako?


mkuyuga said:
Jizalendo, tunamshuru saaaaaaaana mzee mwinyi kwa kuletea unga ambao umesaidia sana vijana wetu kufaika na huo uchumi wake!!


kuna vijana wetu wamefungwa Pakstani, wengine greece, Italy etc,

Ametutengezea alikaida ndiyo maana vijana wetu kama kufungwa huko marekani.

wakati wake wapasitani walizunguka nchi nzima wakihubiri dini!!

Wakati wa mwinyi alikuza saaaaaaaaana uchumi hadi watu wakawa wanabeba hela kwenye magunia!!

Uchumi wake ulikuwa sana akawa na maduka ya vito arabuni, je unjua kwa nini bodyguard wake alikufa huko arabuni?


Hongera mwinyi kukuza uchumi wa tanzania, hadi wanya wetu sasa wanauzwa nje, pia tausi walipewa kwa maswahiba wake(ref, bungeni).

ngoja niishie hapa sitabishana tena na wewe maana wewe unaoneka unataka kuvuruga umoja wetu humu kwa kugawa watu katika makundi ya dini!

wanabodi kuweni makini na huyu mtu.!
 
Haya leo tunasema tulipanga foleni kununua sabuni na dawa ya meno wakati wa mwalimu...fast forward miaka thelathini ijayo kutoka sasa,tutasema umeme ulikuwa wa mgao! Wakati ule tunapanga foleni,hakuna mtu angetegemea kuwa baada ya miaka 30 tutakuwa hatuna umeme,wacha dawa ya meno!
Tumwache mzee wa watu apumzike jamani,ameifanyia makubwa sana hii nchi and we will forever be indebted to him.
 
ManjiMakuti, Kwani hujui,

kuwa wakati huo ndiyo madawa ya kulevya na unga vilianzA kujitokeza?

Mbona mengi aliyosema Mkuyuga yako wazi?

Ni ni ambacho unakibishia kwa mfano?

(1) Loliondo unaijua?

(2) Hujui wakatyi wa mwinyoi hela zilikuwa za kumwaga mifukoni? layman akiona hivyo basi uchumi safi sana!

etc.
 
mkuyuga na kiruma,

Mimi huwa msomaji mara nyngi na si aghalabu nikachangia mada na wala sikutaka kuchangia mada hii. Lakini ninaona waziwazi kuwa yanaletwa mabo ya kutugawa na anayefanya hivyo si Jizalendo bali ni huyu huyu Mkuyuga na kundi lake. Ninaona wale wanaotahadharisha udini ndio wao wao waliojaa udini na ukweli unaposemwa basi njia ya kukimbilia ni kudai udini na kutaadharisha watu eti tuwe macho na mtu fulani atatuchanganya, na hao wengine eti tunashangilia "tahadhari" hizi ambazo inaonekana wazi yeye yule anayezitowa ndiye anayenuka udini. Hatukugawanywa na upendeleo wa dhahiri wanaopewa baadhi ya taasisi za dini na kunyimwa nyingine tutagawanywa kwa hizi mada ambazo ni za kuweka vitu wazi na ambazo zinatakiwa zitowe ukweli, ziepuke dhana na kashfa zisizokuwa na ushahidi hata chembe.

Kwanini tuogope kusema ukweli. Mwalim Nyerere ni BABA WA TAIFA LA TANZANIA, hiyo ni hadhi aliyonayo ambayo anyang'anyiki kwa sababu zilzo wazi - alijitowa muanga na kutojali mshahara wa ualimu aliolipwa na wakoloni katika jitihada za kutukomboa. Alikuwa mwanaharakati kutetea wanyonge na pia kuikomboa Afrika na mimi ninamueshimu sana kwa hadhi aliyotuletea taifa letu. Aliplay his part pamoja na ufanisi na makosa.

Mzee Mwinyi naye vivyo hivyo aliplay part yake kadri awezavyo na katika kufanya hivyo alijaribu kurekebisha makosa ya Mwalim na kudumisha mazuri yake, na pia alifanya makosa yake. Bali kuna makosa ambayo ni magumu kuyarekebisha na inakuwa siuungwana kumpambikizia makosa hayo wakati tunajuwa chanzo chake alikuwa ni Mwalim Nyerere. Pia si uungwana kumkebei mmoja na kumsifu mwengine kwa misingi ambayo mtu anaijuwa mwenyewe. Hapa tunaangalia pande zote.

Sasa tuchambuwe haya malawama ambayo Mkuyuga anampambikiza nayo Mzee Mwinyi kijumlajumla bila ya ushahidi wala muelekeo:

1. Kuanguka kwa shillingi ya Tanzania:

Shillingi ya Tanzania ilianza kuanguka tangu miaka ya sabini na kufikia mwaka 1975 tayari ilikuwa ni sawa na senti 50 za kenya nakaribu Tsh 15 kwa US$1. Kutoka hapo ikachukuwa plunge za ajabu ukilinganisha na US$ mara 22, mara 35 mara 45, mara 60 na ikapiga mbio hadi shillingi 120 na ikawa inabebwa kwa makapu tayari ingawa makapu hayo yalibidi yafichwe sana. Mwaka 1984 Edward Sokoine akaleta jambajamba na makapu ya shillingi yakafurika kutupwa kama njugu na ole wako kama ungechelewa kuyatupa yako. Na wakati wote huu Mwinyi hakuwa Raisi wa Tanzania. Tangu Mwinyi aondoke madarakani shilligi ndio imedidimia ile mbaya kiasi ambacho kama hapo nyuma iliitaji makapu metaphorically (and I hope that is what you meant) sasa hivi inahitaji magunia. Hivyo si Mwinyi wakulaumiwa kwa kuanguka shillingi, wakulaumiwa ni yule aliyeifanya ikaanza safari hiyo na si mwengine bali Mwalim Julius Kambarage Nyerere.

2. Rushwa:

Tulipopata uhuru neno rushwa halikujulikana lakini siasa za Mwalim Nyerere nazo zikatuletea hili. Baada ya kupata shida za kuishi alizozisasababisha Mwalim kwa tutaifisha kila kitu kikubwa bila ya kujali mwenye kitu hicho alikipataje na kuwalipa watu mishahara peanuts kiasi ya kutokumudu kujipatia chakula, wabongo wakagundua njia za kujikimwi njaa kwa kupokea hongo, na hongo vilipowapunguzia njaa wakagundua kuwa kumbe wanaweza kujipatia mapesa for doing nothing, hivyo wakaanza kudai rushwa. Matokeo yake tunayavuna leo, rushwa babu kubwa imekita mizizi kila mahali na ambayo imekuwa inakuwa out of proportion hadi kufikia akina Nkapa kuuza nchi pamoja na taasisi zile zile vilivyotaifishwa kwa wageni kwa njia ambazo zinaashiria rushwa. Leo hii rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo yetu. Ni nani alipanda mizizi ya rushwa hiyo - Jibu Mwalim Julius Kambarage Nyerere. Mwinyi, Mkapa na Kikwete wao wameikuta tu wapigane nayo na kupachikwa malawama wakati muanzilishi wake anasifiwa.

3. Ujambazi:

Maisha duni yalifanya watu wajiingize kwenye wizi na ubadhirifu ambavyo sasa hivi vinachangamshwa na utandawazi. Dunia nzima sasa hivi ina wauza madawa ya kulevya na ni vipi mtandao wa dunia apambikizwe nao mtu mmoja vinashangaza. Kwa mara ya kwanza ujambazi wa kutumia silaha hapa nchini ulitendeka kwenye Barclays Bank tawi la Market, Tanga mwaka 1969 ambapo shilingi laki tano zililambwa na majambazi yaliyokimbilia kwenye misitu ya kuelekea Kenya. Sehemu kubwa ya jeshi lilipelekwa huko kuwasaka na sidhani kama waalipatikan. Kwa hiyo ujambazi nao ulianza zamani. Na wakati huo vijana wengi tu walizamia melini nje ingawa hali haikuwa harsh kama sasa. Ubaharia ulihesabiwa kama kazi yenye kulipa sana.

Ni nini hasa lilikuwa tatizo la Baba wa Taifa? Huyu mzee hakuwa original katika mambo yake mengi kwa hiyo alikuwa anaigaiga mambo tu kwa kucharuka na akishaiga conviction yake haiteteruki.

a) Mfumo wake wa siasa na uchumi ni muigo wa China.

Hili ni kuanzia Arusha Declaration lenyewe, kutaifisha mali za watu, kuanzisha vijiji vya ujamaa, mfumo wa nyumba kumi kumi, jinsi alivyovaa nguo zake na hata vile alivyotaka tugutiane. Yeye alikuwa "Mwalim" kama vile Mao alivyokuwa "Mwenyekiti" na wengine wote tulikuwa "ndugu" kama vile Wachina wote walivyokuwa "comrades". Alijaribu kulable kuiga huko eti ni African Socialism lakini hamkuwa na uafrika hata chembe humo. Waafika ni socialists bali sio kwa mtazamo wke yeye. Muafrika alithamini kuwa na kitu chake mwenyewe iwe shamba, iwe nyumba ambavyo aliviudumia kwa jasho lake bali hakusita kushare matunda ya vitu hivyo na jamaa zake na hata wageni. Ndio maana hapo zamani ungeweza kuchuma ndizi kwenye shamba la mtu ukala bila ya kuulizwa neno. Cha msingi ni kuwa walitaka ijulikane kuwa vitu hivyo ni vyao. Chini ya Mwalim walinyang'anywa fahari hii kwa kupambikizwa mashamba ya vijiji ya pamoja yasiyojulikana mwenyewe hasa ni nani.

b) Umoja na ukombozi wa Afrika

Hii nayo ilikuwa ni adhima ya Kwame Nkrumah ambaye Waghana walimshtukia akapinduliwa. Kuanzia hapo Mwalim akalivalia njuga.
Bali si hivyo tu yeye hakuwa na itikadi inayoeleweka kwani WaBiafra walipotaka kujitenga kutoka Federation ya Nigeria yeye aliwaunga mkono!! Ieleweke kuwa karibu Biafra yote ni Wakristo kisha Waroman Catholic. Je dini ilikuwa ni kigezo hapa? Hata hivyo Nigeria ni moja hadi leo!!

c) Mwalim alikuwa fundi wa kuiga kwa kutafsiri kazi za wengine, hasa zile za William Shakespear. - i) Mabepari wa Venisi, ii) Julius Caesar.

Swali ni kuwa ni mangapi mengine ambayo Mwalim alikuwa akiigaiga tu. Na nini zimekuwa athari zake kwetu?

Haya niliyoyataja bayana hapo juu kuhusu Mwalim sio dhana ni mambo factual bali haya yenu ya Mzee Rukhsa ninaona ni hatihati tupu ambazo ni wazi zina udini ndani.

Quote:
Originally Posted by mkuyuga
Jizalendo, tunamshuru saaaaaaaana mzee mwinyi kwa kuletea unga ambao umesaidia sana vijana wetu kufaika na huo uchumi wake!!


kuna vijana wetu wamefungwa Pakstani, wengine greece, Italy etc,

Ametutengezea alikaida ndiyo maana vijana wetu kama kufungwa huko marekani.

wakati wake wapasitani walizunguka nchi nzima wakihubiri dini!!

Wakati wa mwinyi alikuza saaaaaaaaana uchumi hadi watu wakawa wanabeba hela kwenye magunia!!

Uchumi wake ulikuwa sana akawa na maduka ya vito arabuni, je unjua kwa nini bodyguard wake alikufa huko arabuni?


Hongera mwinyi kukuza uchumi wa tanzania, hadi wanya wetu sasa wanauzwa nje, pia tausi walipewa kwa maswahiba wake(ref, bungeni).

ngoja niishie hapa sitabishana tena na wewe maana wewe unaoneka unataka kuvuruga umoja wetu humu kwa kugawa watu katika makundi ya dini!

wanabodi kuweni makini na huyu mtu.!



kiruma said:
ManjiMakuti, Kwani hujui,

kuwa wakati huo ndiyo madawa ya kulevya na unga vilianzA kujitokeza?

Mbona mengi aliyosema Mkuyuga yako wazi?

Ni ni ambacho unakibishia kwa mfano?

(1) Loliondo unaijua?

(2) Hujui wakatyi wa mwinyoi hela zilikuwa za kumwaga mifukoni? layman akiona hivyo basi uchumi safi sana!

etc.
 
ManjuMakuti,
kwanza karibu kijiwe hiki na itabidi ukafanye utafiti wa nguvu kuweza kutuvuta.
Ningependa tu kukuuliza maswali mawili ambayo yamekita ktk kila hoja yako...Hii ALIYEANZA..
Aliyeanza kuanguka kwa shilingi, sijui Rushwa na Ujambazi ni Nyerere imetoka wapi?... Mbona vyote hivyo vilikuwepo toka dunia iumbwe na labda labda kwa urahisi zaidi niseme toka mkoloni! je, tumlaumu Mungu au mkoloni kwa kuwepo vitu hivyo?
Nyerere hakutoa mishahara midogo laah hasha. Graduate wa UDSM alikuwa akichukua Tsh.1750/- mwaka 1975 hali nyumba ya msajili bada ya utaifishaji ni chini ya Tsh. 200 sijui (that's about 10% ya mshahara..damn!). Uliona wapi dunia hii! haya kima cha chini kilikuwa 450 kwa hiyo nao waliweza kuapnga chumba kimoja...Achaa mzee Ukiruka hadi mwaka 1980 mishara ilipanda hadi kufikia kitu kama Tsh. 2040/- kwa graduate. Maisha nayo yalipanda lakini bado wasomi waliweza kuyakabiri maisha.
Na ushahidi mkubwa ni kwamba wazazi wetu sisi wote humu wanazo nyumba zao yaani waliweza kujenga nyumba kwa kutegemea ajira wakati wa Nyerere!...(hata iwe ya vyumba sita). Walioshindwa kujenga walikuwa wamelemazwa na nyumba za bure za serikali. Acha mbali maswala ya usafiri wa UDA wa shilingi 1, kila idara na mashika yake walikuwa na usafiri wao. Jangwani hakuna kabisa kuona mfanyakazi anayekatisha kwa mguu. Leo hii mshikaji kukatiza jangwani imekuwa ibada ya kila mfanyakazi.
Kisha swali la Pili ni hii KUIGA..
Mshikaji ELIMU ya kitu sio KUIGA, jaribu kutofautisha vitu hivi. Hivi kweli dunia ya leo unaweza kuanzisha kitu ambacho hakikugusiwa na mtu yeyote kabisa!.. yaani wewe ndio uwe mwanzilishi, sidhani tena dunia ya tatu mmmh!..ndoto.
Hakuna kati yetu anayeweza zuka na mfumo wa siasa, uchumi, sayansi wala dini ambayo haijawahi kuandikwa sehemu. Huo utakuwa ni UTUME tena.
Vyote tunasoma vitabu na ku-apply haina maana tunaiga. Ujamaa hakuuanzisha Mao nae kaukuta. Hao akina Shakespear na Caesar, wametumiwa na viongozi kibao wa dunia hii ktk hotuba zao, mifumo ya bunge,senate ktk uongozi n.k. Hii sio kuiga mshikaji sidhani Mwinyi alikuja na zake kama sii kufuta akina Kandoro na Shaaban Robert.
Nakuomba usome kitabu cha Nyerere kinachoitwa UJAMAA na utakuta tofauti nyingi sana na huyo MAO.
Mwache mzee wa watu wewe dollar tumebadilisha sisi na tunafahamu kabisa kwamba mwaka 1975, bei za mazao yetu zilishushwa mara mbili na hao westerners hali bidhaa zao ikiwa ni pamoja na mafuta (OIL) vilipanda bei mara mbili. Kwa hiyo hata kama uchumi wetu ungekuwa mzuri kiasi gani... pingamizi zilikuwa nyingi sana mbali kabisa na ukame, vita, vikwazo vya kiuchumi n.k.
Vita baridi mshikaji ilikuwa kuwaangusha wote waliokuwa wakifuata UJAMAA na TZ haikuwa tofauti na nchi nyinginezo.
 
nimegundua watu wanasema yale yanayo wajia mwalimu kama mtu kafanya mengi mazuri na machache mabaya kwa hiyo mwacheni apumzike kwa amani mzee wa watu ni hero wa Tanzania na Patriotic hakuna Kiongozi kama yeye kwa hili hapa tanzania kwa sasa .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom