Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Imani hiyo itapimwa na uchaguzi mdogo wa Tunduru maan nimeona kauli za makamu wa CCM zinaonekana kuleta fitina miongoni mwa wananchi kama ilivyo kuwa kule kwa Cheyo wakati ule . Yangu macho
 
Habari za leo ndugu wanaforum,

NImesikia Rais Kikwete amejitosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi na kisiasa huko Zimbabwe. Sasa sielewi, kwanini yeye jamani?? Soma Habari Kamili

JK ajitosa kusuluhisha Zimbabwe

61179480.WEF_7741.jpg

Rais Kikwete!!

Kutoka gazeti la 'wapinzani wetu' Tanzania Daima
na Prisca Nsemwa


ZIARA ya siku moja aliyoifanya Rais Jakaya Kikwete nchini Zimbabwe juzi, inaonekana kuzaa matunda kwani Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo, ameonyesha kulegeza msimamo katika msuguano na nchi za Magharibi.

Wakati wa ziara hiyo, Mugabe si tu alikiri kuwa hali ya uchumi wa nchi hiyo imefika pabaya, bali pia alikubali kushirikiana na Kikwete kutatua matatizo ya kiuchumi na kisiasa yanayoikabili nchi hiyo.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi kuhusu ziara hiyo.

“Rais wetu amefanya mazungumzo na Rais Mugabe na wamekubaliana kutatua matatizo ya kiuchumi na kisiasa yanayoikabili nchi hiyo na kusababisha maendeleo ya kiuchumi kupungua,” alisema Membe.

Alisema katika ziara hiyo Kikwete alimwelezea Mugabe kuhusu msimamo wa nchi za Ulaya ambazo amezitembelea hivi karibuni.

Aidha, Membe alisema Mugabe naye alitumia fursa hiyo kumweleza Kikwete hali halisi nchini Zimbabwe, hasa kuhusu tukio la Machi 12, mwaka huu lililohusisha kupigwa na polisi kwa wafuasi na viongozi wa vyama vya upinzani na kusababisha mfuasi mmoja wa chama cha MDC kupoteza maisha.

Alisema uchumi wa Zimbabwe hadi hivi sasa si mzuri kutokana na mgomo huo na kumekuwepo na mfumuko wa bei hadi kufikia asilimia 1700 hali ambayo inazidi kufanya maendeleo ya nchi hiyo kupungua.

“Nchi ya Zimbabwe inahitaji mazungumzo iweze kuwa na muafaka katika uchumi na siasa ili nayo ipige hatua katika maendeleo,” alisema Membe.

Akitoa mfano, Membe alisema kuwa licha ya kuwa maskini, Tanzania imepiga hatua katika maendeleo, na inawajibika kuisaidia Zimbabwe ili iondokane na migogoro iweze kujenga uchumi wake.

Membe alisema katika ziara yake ya hivi karibuni katika nchi kadhaa za Ulaya, Kikwete alijifanya balozi wa nchi hiyo na kuwaelezea viongozi wa nchi hizo kuwa iwapo wataendelea kuitenga Zimbabwe, nchi za Afrika nazo zinaweza kususa kuhudhuria mikutano inayoandaliwa na nchi hizo kama njia ya kuonyesha mshikamano.

Katika hatua nyingine, amesema kutakuwa na mkutano baadaye mwezi huu jijini Dar es Salaam kuzungumzia muafaka wa nchi hiyo.
 
Ni kwa sasabu ya cheo chake na nafasi ya Tanzania katika SADC.

.... kamati ... ya masuala ya usalama SADC.
 
Tanzania tulisaidia kwa hali na mali mpaka Rhodesia ya Kaskazini ikawa huru na kuitwa Zimbabwe. Kwa hilo tulifanikiwa kwa gharama tulizochangia chakula na wanajeshi).

ILA nina mashaka na siamini kama JK ana charisma kama ya Mandela au Kambarage kuweza kufit kama mshuluhishi wa mgogoro wa Zimbabwe ulioanzishwa na Mugabe against the west. Isitoshe JK would exercise cautious approach to address any warning against Mugabe's reign of terror vinginevyo atajikuta anasutwa naye ajitoe mboni jichoni mwake.. kwani ya Tunduru yanashabihiana na ya Zanzibar 2001 na 2005 ktk kila namna!
 
Kwanza ningelikuwa JK, ningemaliza kwanza mgogoro wa muungano,

suala hili la mahabusu, kukomesha unyanyaswaji wa wpinzani kunakotokna na POLISI, FFU KUPIGA WATU WAKATI WA KAMPENI. HUU UMEKUWA UTARATIBU WA TANZANIA KILA MARA UCHAGUZI UNAPOFANYIKA,

REF 2005, BUKOBA, MOSHI, TARIME TO MENTION BUT A FEW!!

WATANZANIA TUNAPENDA MISIFA KIBAO HUKU NDANI HAKUKALIKI.


MTAJIONEA WENYEWE TENA MWAKA 2010 NA 2015 JINSI WATU WATAKAVYOPIGWA NA POLISI WA CCM YETU!

MARA UTASIKIA MAKALA ANASEMA VIJANA WA CHI CHI EMU WAMEJIANDAA KUBALI WAHUNI ETC!

MARA OHOOO HUKO ZANZIBAR UTASIKIA VIJANA WA CHI CHI EMU WAKIJIITA JANJAWEED!!

YANGU MACHO
 
Urais wa Kikwete ni Wa kwake na Familia yake na marafiki zake au wa Wananchi... jamani waliolielewa swali langu msaada ndugu zanguni nifahamisheni nina ona kuna hali ambayo siyo yakawaida katika uongozi wa awamu ya nne, kuhusu yeye na maswahiba zake kuishi vizuri wakati wananchi wanatesheka na kusubiri ahadi zilizotolewa kwa magunia ya kilo 200 mia200 wakati wakampeni.

kuhusu Richimond kimya,Radar kimya, Ndege kimya, Ditto Pile ndiyo basi tena shashaaa Mapanki na walio husika kimya na mengine mengi tu je tunapelekwa wapi?

msaada jamani
 
Kikwete; tushike anayoyasema au anayoyatenda?
Kitila Mkumbo

KUNA kanuni kuu tatu katika ufundishaji, ambazo kila mwalimu mwenye kufuata kanuni za ualimu huzifuata pindi anapoingia darasani kufundisha. Kwanza, mwalimu atawaambia wanafunzi wake kile ambacho anataka kuwaambia katika siku hiyo. Pili, atawaambia kile ambacho alisema atawaambia. Tatu, anapomaliza kufundisha somo, atawaambia tena wanafunzi wake kile alichowaambia.

Kwa wanasiasa walio waadilifu, kuna kanuni tatu pia. Kwanza, mwanasiasa atawaambia wananchi wake kile ambacho amepanga kufanya na kwa nini anafikiri ni muhimu kufanya hicho kitu. Pili, atafanya kile alichowaambia wananchi wake kwamba atakifanya. Tatu, akishakukifanya, atawaambia kwamba amefanya kile alichofanya na kuonyesha mazao au matunda ya yale aliyoyafanya. kwa kanuni nyingine ya mafanikio kwa kiongozi wa siasa. Ili kiongozi wa siasa afanikiwe anahitaji awe na nia nzuri na uwezo. Ukiwa na nia tu bila uwezo haisaidii. Vile vile, ukiwa na uwezo bila nia, hiyo pia haisaidii; utakwama.

Ni wazi, kwa mfano, Rais mstaafu Benjamin Mkapa alikuwa na uwezo, lakini hakuwa na nia ya kuwaendeleza Watanzania. Yeye nia yake ilikuwa ni kuwafurahisha wakubwa wa kimataifa na nafsi yake mwenyewe. Ndiyo maana alizomewa nchini, lakini akashangiliwa nje ya nchi na wakubwa wa ubepari. Ndiyo maana aliamua kununua ndege na rada za anasa, huku mawaziri wake wakiwaambia walio na njaa wawe tayari kula majani!

Nimekuwa nikifuatilia kauli na matendo ya Rais Jakaya Kikwete tangu wakati wa kampeni ndani ya CCM hadi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu na sasa akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyo kwa Watanzania wengi, nimepata kumsikiliza Kikwete kupitia redio, televisheni na kumsoma kwenye magazeti.

Nimebahatika pia kumsikiliza ana kwa ana mara mbili alipofanya ziara nchini Uingereza. Katika mara zote hizi, nimeshindwa kumuweka Kikwete katika makundi niliyoyataja hapo juu. Lazima nikiri mapema kabisa kuwa, rais wetu amejaliwa ucheshi na haiba ya hali ya juu. Ukimuona utafurahi na ukimsikiliza lazima ucheke! Lakini, ukijiweka kama mwanafunzi na ukamweka Kikwete kwenye mizani ya ualimu, basi ujue ni wazi kabisa kwamba yeye hafuati kanuni za ualimu.

Hii ni kwa sababu utashtukia amemaliza kufundisha bila kujua alianzaje na amemalizaje! Hata hivyo sitaki kumlaumu kwa kutokufuata hizi kanuni za ualimu maana yeye kitaaluma si mwalimu; kwa hiyo ni kumuonea kama tutatarajia naye afanye kama wafanyavyo walimu wanaofuata maadili na taaluma yao!

Tatizo langu kubwa ambalo ndilo chimbuko la makala hii, ni kauli na matendo ya Rais Kikwete kama mwanasiasa. Kila anaposimama kuzungumza, amekuwa akiibuka na kauli zinazokinzana. Zaidi ya yote, haelekei kwamba yale anayoyafanya yanafanana na yale ayasemayo. Kuna kila dalili kuwa katika urais wake, Kikwete atasema yale asiyoyatenda na atatenda yale asiyoyafanya.

Ni wazi pia kuwa Rais Kikwete hataweza kutekeleza ahadi lukuki alizozitoa katika kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2005. Kisicho dhahiri ni sababu za Rais Kikwete kushindwa kutekeleza ahadi zake. Ni kwamba, hana nia, lakini ana uwezo? Au nia anayo, lakini hana uwezo? Au vyote hana? Nitatoa mifano michache kuthibitisha hisia zangu.

Moja ya ahadi kubwa alizotoa Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005 na hata baada ya kuapishwa kuwa rais, ni kupitia upya mikataba ya madini. Ahadi hii ilikuwa ni jibu kwa kilio cha muda mrefu kilichopuuzwa na utawala wa Rais Mkapa, kuhusu uporwaji wa madini unaofanywa na kampuni za madini katika migodi mbalimbali nchini.

Kikwete aliahidi kuwa serikali yake ingeipitia mikataba yote ya madini ili hatimaye sisi nasi tuanze kufaidika na madini yanayochimbwa katika migodi yetu. Akasema kuwa yeye alikuwa anataka ‘win-win situation’, yaani kila upande ushinde, kampuni na sisi wenye madini; kwa kuwa kampuni zina nyenzo za kuchimba madini, lakini madini haya yapo katika ardhi yetu, kwa hivyo ni kwetu.

Pamoja na onyo la Profesa Ibrahim Lipumba kuwa, Kikwete alikuwa ni mtu wa mzaha, haamanishi anachokisema, bado Watanzania walio wengi walimwamini, wakamchagua, tena kwa kura nyingi. Sasa Kikwete baada ya kukabidhwa nyenzo ya kupitia mikataba, amebadili kauli.

Akijibu swali la Mtanzania mmoja jijini London katika moja ya ziara zake nyingi, Kikwete kwa ujasiri mkubwa na bila aibu ya kusutwa na maneno yake ya nyuma, alisema kuwa, kwa hali halisi ilivyo katika mikataba ile, “that is the best we can get”, akimaanisha kuwa tunachopata ndiyo stahili yetu!

Akasema pia kuwa, mikataba ya madini ambayo Tanzania imeingia, ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa na yeye kwa kuwa anahangaika kuvutia wawekezaji, asingekuwa tayari kugeuka jiwe. Kikwete akasema kuwa anachofanya sasa ni kuwaomba hawa wenye kampuni wafupishe muda wa kutokulipa kodi ili waanze kulipa mapema zaidi kuliko ilivyoanishwa kwenye mkataba.

Alihitimisha jibu lake kwa kusema kuwa, wakati akifanya jitihada za kuwashawishi wenye kampuni kuanza kulipa kodi ya serikali, itabidi Watanzania tuendelee kuvumilia na ana imani kuwa hili litafanikiwa kufikia mwaka 2010! Ukimsoma vizuri Kikwete katika maelezo yake, ni kama vile ndiyo kwanza alikuwa anaielewa mikataba ya madini baada ya kuwa rais.

Na kwa mtu ambaye hakuwa Mtanzania na ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kumsikiliza katika mkutano ule, angefikiri kuwa rais anayezungumza, alishinda urais akitokea chama cha upinzani! Ingebidi uwe na ushawishi wa aina yake ili mtu huyo akuamini kuwa anayezungumza mambo hayo alikuwa waziri mwandamizi katika wizara mbalimbali za serikali zilizopita kwa zaidi ya miaka kumi na tano, tena nyingine zikihusika moja kwa moja na mikataba ya nishati na madini!

Nilizidi kushikwa na butwaa zaidi baada ya kusoma mazungumzo ya rais na mwenyeji wake nchini Norway. Pamoja na mambo mengine, kule Rais Kikwete aliibuka na kauli mpya ya aina yake kuhusu mikataba ya madini.

Akasema kuwa tatizo la mikataba mibovu lilisababishwa na ukosefu wa wataalamu wenye uwezo wa kujadili mikataba! Hii ni kauli mpya kabisa ambayo rais hakuwahi kuitoa kabla; kauli ambayo inaibua maswali mengi kuliko majibu.

Kwanza, iweje nchi hii katika miaka 45 ya uhuru isiwe na wataalamu wa kuelewa mikataba? Iweje nchi hii yenye idara kubwa sana ya Jiolojia pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani) na yenye wizara nzima inayohusu madini, isiwe na wataalamu wa kuelewa mikataba?

Inawezekanaje rais ateue kamati ya kupitia upya mikataba ya madini wakati akijua kabisa kuwa hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kujua hiyo mikataba yenyewe? Au ndiyo tuseme moja ya mang’amuzi ya kamati ile ni kuwa hatuna wataalamu wa kuelewa mikataba, wakiwemo wajumbe wa hiyo kamati?

Kwa maoni yangu, rais katudhalilisha. Tatizo la mikataba haliwezi likawa limesababishwa na ukosefu wa wataalamu. Limesababishwa na kukosekana nia safi ya kusimamia mali zetu asili. Limetokana pia na mwendelezo wa Serikali ya CCM ya kusimamia maslahi ya watu binafsi na wachache badala ya umma.

Ni ubinafsi wa Serikali ya CCM ndio umewafanya waifiche mikataba isijulikane hata kwa Bunge ambalo limejaa wabunge wa CCM! Ni vigumu kuelewa inakuwaje serikali hii inawaamini madalali wa kigeni kujadili mikataba kwa niaba yetu, lakini haiwezi kuwaamini wabunge waliochaguliwa na wananchi angalau waione tu mikataba hiyo, tena wabunge kutoka chama kinachotawala! Hii inaweza kutokea Tanzania tu!

Ahadi nyingine ambayo Rais Kikwete amekuwa akiitamka kwa sauti kubwa kuwa, ataitekeleza kwa dhati na kwa moyo mkunjufu, ni ujenzi wa demokrasia. Amekuwa akirudia kila mara, kwa mfano, kuwa hana nia ya kuvidhoofisha vyama vya upinzani na kwamba atazingatia utawala wa sheria na haki za binadamu na kudumisha uhuru wa watu kutoa maoni yao.

Hata hivyo, ukiangalia matendo ya serikali yake tangu aingie madarakani, ni rahisi kung’amua kuwa ayasemayo Rais Kikwete siyo anayoyatenda. Kwa mfano, kwa mara ya pili Mahakama Kuu imeharamisha sheria inayozuia wagombea binafsi.

Lakini Rais Kikwete, katika vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM akaweka msimamo wa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu katika Mahakama ya Rufaa. Na kweli, miezi kadhaa baada ya hukumu, tumeona Mwanasheria Mkuu wa Serikali - naamini kwa maelekezo na shinikizo kutoka CCM - akifungua rufaa hiyo katika Mahakama ya Rufaa.

Sasa haiingii akilini kwa rais aliyeahidi na anayehimiza ujenzi wa demokrasia kuendelea kung’ang’ania sheria ambayo inapingana na katiba ya nchi na ambayo ilipingwa vikali na hata mwasisi wa chama kilichomweka madarakani, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Ni serikali ya Kikwete pia ambayo imebuni mtindo mpya wa kuwarubuni viongozi wa upinzani kwa kuwaahidi kuwapa madaraka pindi wahamiapo CCM.

Anachokifanya Kikwete na serikali yake, ni kuwaonyesha wananchi kwamba upinzani haufai kiasi kwamba hata viongozi wao wanawakimbia. Ni aibu kwamba Kikwete na CCM wanajaribu kujenga uhalali na ufuasi wa chama chao kwa kujaribu kubomoa upinzani badala ya kutekeleza yale waliyoyaahidi katika uchaguzi uliowaweka madarakani!

Sasa yote haya yananifanya nijiulize hivi, Rais Kikwete unataka tuamini uyasemayo au uyatendayo? Pili, Rais Kikwete una nia na uwezo wa kuyafanya uliyoahidi? Kikwete ukitaka uache alama chanya katika utawala wako, fanya kama usemavyo. Kama kweli unataka kukuza demokrasia katika nchi yetu, onyesha hili kwa vitendo.

Ruhusu wabunge wetu wajadili mikataba yenye maslahi ya taifa kabla ya kutiwa saini. Ruhusu mjadala mpana wa mapungufu ya katiba yetu na muungano wetu. Tekeleza hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu mgombea binafsi. Vinginevyo, utaingia katika historia ya viongozi wanaohubiri wasiyoyaamini.

Mwandishi wa makala hii ni Mtanzania aliyepo masomoni nchini Uingereza. Anapatikana kwa barua pepe; kitilam@yahoo.com

Tanzania Daima: 28 Machi 2007
 
Hii makala ni sahihi kabisa. Rais anayosema na anayotenda au wasaidizi wake wanayotenda ni mambo mawili tofauti.

Rais alipoenda Denmark na kukutana na Waziri wa maendeleo wa kule akapigwa swali kuhusu ujenzi wa demokrasia na udhaifu wa vyama, akasema ooh, CCM inahitaji upinzani. Wakati anasema hivyo, Makamba Katibu Mkuu wake ananunua shahada za wapiga kura Tunduru kwa shs. 5000.
Huku sio kuua demokrasia?
Kama wanaamini katika demokrasia kwani nini pasiwe na uchaguzi huru na haki?

Ninamsikitikia sana Rais, matumaini ya watu yanashuka sana.
 
Chief - sijakupata hapo. Lakini, yeah, nataka kujua kama huyu "Zitto" ni Zitto Kabwe wa CHADEMA ili tumu-engage kama Mbunge wetu na kumpa messages ampelekee Bwana Mbowe azuke hapa.
 
Mugongo huwezi kunipata kirahisi ama kama umenipata basi hutaki kusema umenipa I wonder kwamba unaandika sawa kabisa na Mzee Es aliye tuaga hapa maana I smell the beef aliyonayo kwa Mbowe ila sasa wewe umekuja na njia tofautio kidogo ambaye inakuwa rahisi kwa kila mwana JF kujua what is going on .Prove me wrong
 
Chifu - kama uko hapa kutazama ni nani anaandika nini na maandiko yake yanafanana na nani, then I can't help you. Haka ka-ugonjwa ka watu wa CHADEMA ka kutaka kuchunguza ni nani anam-criticise Mbowe, badala ya kuangalia validity ya criticism yenyewe, ndiko kanawafanya muonekane hopeless humu. Hakuna conspiracy mjomba. Na kama unadhani mie Mzee ES, I take the compliment with humility.
 
ya matumizi na safari za nje zisizokwisha!!! Lini wataweka neno la "kupunguza matumizi" kwenye vocabulary zao? Kuna haya ya kupunguza mawaziri, makatibu wakuu na wasidizi wao, wakuu wa mikoa (imagine kama tungekuwa na majimbo badala ya kuwa na wakuu wa mikoa 25 tungeweza kuwa na wakuu wa majimbo watano au sita tu) n.k.
~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Books aren`t adding up at Treasury: Govt forks out 600bn/- to cover budget deficit




MOMENT OF GLORY: Ms. Evelyine Lupimo from St. Francis Secondary School of Mbeya who led a pack of 11 other high achievement during last year `O` Level exams, gets the proverbial pat on the back from President Jakaya Mrisho Kikwete at State House in Dar es Salaam yesterday.
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THERE is an apparent crisis in the national economy, forcing the government to reallocate over 600bn/- from its budget to cover-up a budget deficit that rose from six to 25 per cent within the past six months, it has been learnt.

Sources within the government confirmed that the Cabinet had since already directed all accounting officers to release ’extra money’ to the Pay Master General (Permanent Secretary, Ministry of Finance) who will reallocate it to the emergency budget.

’’The government discussed the issue (budget deficit) this week in a crucial meeting and realized that the economic prospects were murky. However, the problem is not one of tax collection but a sharp decrease in production,’’ said a source.

This year’s droughts and subsequent floods across the country had adversely affected agricultural production, key player in the national economy (45%), as were other sectors indirectly affected by severe climatic changes.

Among other things, the source said other factors weighing down on the 2006/07 budget is the increase in foreign debt, for which the government needs extra 275bn/-, the Rift Valley Fever (RVF) (no figure), while government spent an extra 38bn/- to cover the power crisis caused by drought.

’’Also there was oversight on government workers within the parastatal sector that cost the government 31bn/- -- which was not budgeted for in the 2006/07 budget. There is another 20bn/- needed on leaders’ trips,’’ said a source who works with the Treasury.

Other drains on the government budget include the Chimwaga University of Dodoma where the government spent about 31bn/-, while the floods that affected infrastructure and crops has also cost the government billions of money. The figure has not yet been established.

Shadow Minister of Planning and Economic Empowerment, Zitto Kabwe, said: ’’It’s shocking that our economy is dropping so fast �just where is that money going�? The Kigoma Urban MP (Chadema), further observes: ’’At the time of the budget, the Tanzania Revenue Authority was collecting 200bn/- a month, which has now gone up to more than 233bn/- a month, why a budget deficit?’’

Zitto said the reallocation raises serious unanswered questions -- such as why the Prime Minister’s Office slashed about 5.3bn/- from Parliament without consulting the Clerk to the National Assembly.

’’That’s why we are saying parliament and judiciary must be independent � they must have their own budget and the Clerk of the National Assembly and the Judicial Registrar must be accounting officers � enjoying the same status with permanent secretaries �they should also attend the Inter Ministerial Technical Committee,’’ said Zitto.

Earlier this year, the Permanent Secretary to the Ministry of Finance, Gray Mgonja, reportedly assured Tanzanians not to a ’anticipate a big budget deficit’ despite the current power supply and food crises throughout the country.

Last February alone, the government spent some 30bn/- in subsidies to the Tanzania Electric Supply Company, the country’s sole power supply firm, to buy electricity from private companies.

The country also spent 2.4bn/- ($2m) on procuring and delivering relief food to regions hard hit by the current drought.

Mgonja also assured Tanzanians that the country had the capability to deal with any eventuality of budgetary deficit not exceeding two per cent of the country’s gross domestic product.
 
Sisi CCM tunatesa nyinyi wana inji ama wadanganyika mnalia nini ? Si tulinunua kura mkala chenu ? Sasa ni muda wetu kurudisha chetu .
 
..... (a). presidents foreign trips (should we call these DUTY TRAVEL?) (b). Richmond Scandal (c). Lexus acquisition by the Prime Minister's Office - just a tip.

Katika (b) na (c) were the Public Procuremet Regulatory Authority consulted au walirukwa vihunzi? Kama ni hivyo wamefanya nini baada ya kugundua?
 
Back
Top Bottom