tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Jana wakati nikifuatilia mdahalo wa uuzwaji wa UDA, Mkurugenzi wa Simion Group aliulizwa kwanini wamebadilisha matumizi ya Yard ya UDA na kuikodisha kwa TBL. Hapa swali lilikwepwa na kwenda kwenye malipo anayoyafanya, hapa alijifananisha na Manji anayelipa milion 20 kwa mwaka<ambaye ana eneo kubwa zaidi>, na yeye anayelipa milion 200 kwa mwaka. Kisena alihoji nani ni tapeli kati ya yeye na Quality Group? Nionavyo: Kisena hakujibu swali, pia utapeli wa mwingine haumfanyi yeye ashindwe kutapeli. Nawasilisha