Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Salaam wana JF.
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, watu wenye umri zaidi ya miaka 18, ndio wanaoruhusiwa kupiga kura
Kati ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wapo ambao wana vyama na ambao hawana vyama;
Kati ya wale wenye vyama (kwa ujumla wao) na wasio na vyama, wengi ni wale wasio na vyama maalum.
Katika wale wenye vyama, linapokuja suala la urais, wanaweza kumchagua rais kutoka chama chao, au kama ikitokea mtu mwingine kutoka chama kingine mwenye ushawishi mkubwa, wanaweza kumchagua vile vile.
Hata hivyo hata kama ikitokea watu wa chama fulani wote wakamchagua rais kutoka chama chao ila watu kutoka nje ya chama hicho wasimchague, bado hawezi kuwa rais kwa kuwa hakuna chama chenye wanachama wengi kuliko wale wasio na chama.
Hivyo basi, kuelekea uchaguzi 2015, atakayeshinda nafasi ya urais, ni yule tu atakaye weza kushawishi akawa anakubalika ndani ya chama chake na nje ya chama chake.
Ikumbukwe kwamba katika uchaguzi wa 2005, Rais kikwete alishinda vibaya kutookana na kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka ndani ya chama chake, kutoka vyama vingine na kutoka kwa watu wasio na vyama.
Huo ndio ukweli. Anayetaka na autumie apate njia aende zake.