Huyu ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hapo 2015

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,815
2,000
Salaam wana JF.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, watu wenye umri zaidi ya miaka 18, ndio wanaoruhusiwa kupiga kura

Kati ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wapo ambao wana vyama na ambao hawana vyama;

Kati ya wale wenye vyama (kwa ujumla wao) na wasio na vyama, wengi ni wale wasio na vyama maalum.

Katika wale wenye vyama, linapokuja suala la urais, wanaweza kumchagua rais kutoka chama chao, au kama ikitokea mtu mwingine kutoka chama kingine mwenye ushawishi mkubwa, wanaweza kumchagua vile vile.

Hata hivyo hata kama ikitokea watu wa chama fulani wote wakamchagua rais kutoka chama chao ila watu kutoka nje ya chama hicho wasimchague, bado hawezi kuwa rais kwa kuwa hakuna chama chenye wanachama wengi kuliko wale wasio na chama.

Hivyo basi, kuelekea uchaguzi 2015, atakayeshinda nafasi ya urais, ni yule tu atakaye weza kushawishi akawa anakubalika ndani ya chama chake na nje ya chama chake.

Ikumbukwe kwamba katika uchaguzi wa 2005, Rais kikwete alishinda vibaya kutookana na kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka ndani ya chama chake, kutoka vyama vingine na kutoka kwa watu wasio na vyama.

Huo ndio ukweli. Anayetaka na autumie apate njia aende zake.
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Tunamtaka kiongozi atakaeweza kusimamia mabadiliko ya kimfumo! Mfumo ungekuwa unaruhusu sasa hivi prof Lipumba angekuwa waziri wa fedha! Lisu angekuwa waziri wa katiba na sharia, Mbowe angekuwa PM, Mnyika angekuwa waziri kamili wa nishati na madini, January angekuwa waziri wa sayansi na technolojia, Dr Slaa angekuwa waziri wa mambo ya ndani...Mchechu angechukua nafasi ya magufuli....
 
Ni mfumo gani sasa ambao unaweza kuliwezesha hilo practicaly? ni nani anayeweza kuuweka mfumo huo? kutaka tu bila kufuata itifaki kanuni na mifumo iliyopo ya kiutawala,kisheria na hata kiasili , tutabakia kutaka tu lakini hatutafikia lengo kamwe.
 
vyuku

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
501
225
Tunamtaka kiongozi atakaeweza kusimamia mabadiliko ya kimfumo! Mfumo ungekuwa unaruhusu sasa hivi prof Lipumba angekuwa waziri wa fedha! Lisu angekuwa waziri wa katiba na sharia, Mbowe angekuwa PM, Mnyika angekuwa waziri kamili wa nishati na madini, January angekuwa waziri wa sayansi na technolojia, Dr Slaa angekuwa waziri wa mambo ya ndani...Mchechu angechukua nafasi ya magufuli....

We unachekesha sana,unataka kumpa mtu uwaziri wa katiba na sheria wakati ndio mtu wa mwanzo kuvunja katiba??huyo mbowe ukimpa u PM si ndo kuwajaza wachaga wenzake ktk serikali??hapana mpa mchaga nafasi kubwa,ataiba na kwenda kujenga nyumba za kifahari dubai na kuchukua mademu na kufanya ufudka.
 
Mushobozi

JF-Expert Member
Aug 20, 2007
543
225
Salaam wana JF.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, watu wenye umri zaidi ya miaka 18, ndio wanaoruhusiwa kupiga kura

Kati ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wapo ambao wana vyama na ambao hawana vyama;

Kati ya wale wenye vyama (kwa ujumla wao) na wasio na vyama, wengi ni wale wasio na vyama maalum.

Katika wale wenye vyama, linapokuja suala la urais, wanaweza kumchagua rais kutoka chama chao, au kama ikitokea mtu mwingine kutoka chama kingine mwenye ushawishi mkubwa, wanaweza kumchagua vile vile.

Hata hivyo hata kama ikitokea watu wa chama fulani wote wakamchagua rais kutoka chama chao ila watu kutoka nje ya chama hicho wasimchague, bado hawezi kuwa rais kwa kuwa hakuna chama chenye wanachama wengi kuliko wale wasio na chama.

Hivyo basi, kuelekea uchaguzi 2015, atakayeshinda nafasi ya urais, ni yule tu atakaye weza kushawishi akawa anakubalika ndani ya chama chake na nje ya chama chake.

Ikumbukwe kwamba katika uchaguzi wa 2015, Rais kikwete alishinda vibaya kutookana na kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka ndani ya chama chake, kutoka vyama vingine na kutoka kwa watu wasio na vyama.

Huo ndio ukweli. Anayetaka na autumie apate njia aende zake.

hapo kwenye red ni vipi???????????/ au na mimi niende zangu kama ulivyosema kwa asiyetaka kukubaliana na wewe???????///
 
gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,062
2,000
Tunamtaka kiongozi atakaeweza kusimamia mabadiliko ya kimfumo! Mfumo ungekuwa unaruhusu sasa hivi prof Lipumba angekuwa waziri wa fedha! Lisu angekuwa waziri wa katiba na sharia, Mbowe angekuwa PM, Mnyika angekuwa waziri kamili wa nishati na madini, January angekuwa waziri wa sayansi na technolojia, Dr Slaa angekuwa waziri wa mambo ya ndani...Mchechu angechukua nafasi ya magufuli....

Weka mbali huyo msaliti,
huyo kengeza umpe u pm halafu wake zetu wataponea wapi?
 
Daffi

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
3,829
2,000
Ni nani sasa anayefaa kuwa rais 2015 kwa mujibu wa vielelezo ulvyoviweka!?
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,224
2,000
Tunamtaka kiongozi atakaeweza kusimamia mabadiliko ya kimfumo! Mfumo ungekuwa unaruhusu sasa hivi prof Lipumba angekuwa waziri wa fedha! Lisu angekuwa waziri wa katiba na sharia, Mbowe angekuwa PM, Mnyika angekuwa waziri kamili wa nishati na madini, January angekuwa waziri wa sayansi na technolojia, Dr Slaa angekuwa waziri wa mambo ya ndani...Mchechu angechukua nafasi ya magufuli....

Eti mbowe PM duuh!mapenzi kitukibaya
 
manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,536
2,000
Rais angekuwa manning Waziri mkuu Juliana Shonza waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba............jazi wengine waliobaki
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,815
2,000
Ni nani sasa anayefaa kuwa rais 2015 kwa mujibu wa vielelezo ulvyoviweka!?
Ni yeyote anayeweza kushawishi akakubalika ndani ya chama chake, kwenye vyama vingine, na kwa watu wasio na vyama.Inawezekana kwa sasa yupo au hayupo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom