Huyu ndiye Rafael Caro, achana na Pablo Escobar

khamis kilo

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,049
1,192
Rafael Caro Quintero

Achana na Pablo Escobar, kuna huyu gwiji mwingine wa kuuza madawa ya kulevya kutoka Mexico, huyu anaitwa Rafael Caro Quinteto maarufu kama "Narco of Narcos" au ukipenda muite "Chapo" (Jina la Chapo lilianzia kwake). Alizaliwa October 3 1952 huko Badiraguato, Sinaloa nchini Mexico.

Rafa alipokuwa mdogo taratibu alianza kupanda zao la bangi kwenye shamba la kaka yake Jorge Luis. Sio chini ya miaka 5 na yeye akafanikiwa kununua mashamba kadhaa na kuanza kujikita zaidi kwenye biashara hiyo.
Lakini baadae serikali ya huko Sinaloa ilifanya msako mkali na kuchoma mashamba yote ya bangi huko Sinaloa. Hali hiyo ilipelekea Rafa pamoja na washirika wenzake akiwemo Miguel Angel Felix Gallardo kuhamia kwenye jimbo la Guadalajara ili kuendeleza biashara yao. Baada ya kufika huko kazi ya kupata connection za madoni mbalimbali wa biashara hiyo ilikuwa chini ya usimamizi wa mtaalamu Miguel Gallardo, huku Rafa yeye akijikita zaidi kwenye kilimo cha bangi.

Rafael alifanikiwa kupata mahali ambapo palikuwa na asili ya ukame na ni mbali kwa maaskari kupadhania wala kufika, eneo lililokuwa na zaidi ya hekari 2500. Na eneo lote hilo likajaa kwa zao hilo la bangi!!! Wakishirikiana pamoja na Gallardo wakaanzisha kundi lao la Guadalajara Cartel huku wakisambaza mihadarati Mexico yote mpaka nchini Marekani!

*Hii ni sehemu ya kwanza, ngoja sehemu ya pili*
593d16e27aea41d7f3b1323cf4eed732.jpeg
 
bwege wewe.
kwa taarifa yako hakuna asiyejua habari za el chapo. hiyo sehemu ya pili wala usijisumbue kuleta jf. baki nayo hukohuko.
Huyo ni RAFA....sio el chapo unaemjua wewe.....kipind hicho el chapo alikua bado hajawa famous....hao kina Rafa chini ya kina Miguel Felix Gullardo ndo walikua wana run mexico kipindi hicho

So punguza ujuaji dogo acha mtoa mada akufunze
 
Huyo ni RAFA....sio el chapo unaemjua wewe.....kipind hicho el chapo alikua bado hajawa famous....hao kina Rafa chini ya kina Miguel Felix Gullardo ndo walikua wana run mexico kipindi hicho

So punguza ujuaji dogo acha mtoa mada akufunze
safiiii, kuna watu hawaelewi
 
Achana nae huyo haelewi kitu, watu kama hao siyo wa kubishana nao
Hivi unaanzaje kumtukana mtu usiyemjua? Huyo El chapo unaemsemea ni huyo uliemtazama kwenye maigizo netflix unakuja kupingana na facts za watu wanotaka kuelimisha jamii?
Dogo kuwa makini aise.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom